Andreas Georgeson ajiunga na Arsenal

Kocha mtaalamu wa mipira iliyokufa, Andreas Georgeson amejiunga na Arsenal kuchukua nafasi ya kocha aliyeondoka Freddie Lgungberg.

Andreas Georgeson ambaye pia ni raia wa Sweden, anaaminika kuwa ni mmoja ya makocha bora kabisa linapokuja suala la mipira iliyokufa, tayari ameshaanza kazi jumamosi iliyopita.

Arsenal wameamua kusajili mtaalamu wa mipira iliyokufa baada ya kufungwa magoli 12 msimu uliopita, ukilinganisha na Brentford iliyofungwa magoli 1o tu katika msimu mzima.

Kazi kubwa ya Georgeson itakuwa ni kukaa jukwaani na kuangalia mchezo kwa mtazamo mwingine na sio kukaa katika benchi ya ufundi la Arsenal. Ni kama vile vile alivyokuwa anafanya Freddie.

Hii si mara ya kwanza Arsenal kuchukua kocha kutoka Brentford kwani mwezi wa 12 Arsenal ilimchukua aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo Inaki Cana.

Inaki Cana ndiye sababu kubwa ya makipa wa Arsenal kupanda kiwango hasa Emi Martinez ambaye alikuwa shujaa wa Arsenal katika kombe la FA.

Pia kocha wa kocha mwingine wa makipa wa Arsenal Sal Bibo ameondoka Arsenal na kuna tetesi za kwamba mkongwe Dennis Bergkamp atakuja kuchukua nafasi yake.

Comments

  1. Ni vizuri ili tupate changamoto nyingine maana arsenal tumepoteza mwelekeo

Tupia Maoni Yako Hapo Chini