Arsenal kucheza dhidi ya Leicester City raundi ya tatu ya kombe la Carabao

Ratiba ya raundi ya pili na ya tatu ya kombe la Carabao imetoka na timu ya Arsenal imepangiwa kucheza ugenini dhidi ya timu ya Leicester City.

Arsenal kucheza dhidi ya Leicester City raundi ya tatu ya kombe la Carabao

Kwa kuwa timu zote mbili zitashiriki katika kombe la Europa League, timu hizo hazikupangwa katika raundi ya pili na zitaanzia harakati zao katika raundi ya tatu.

Msimu uliopita Arsenal ilitolewa katika raundi ya nne ya kombe la Carabao  baada ya kutoka sare ya goli 5-5 na Liverpool ambapo Arsenal walifungwa kwa penati 5-4.

Msimu wa mwaka juzi Arsenal ilitolewa katika hatua ya robo fainali na timu ya Totenham Hotspurs baada ya kufungwa goli 2-1. Arsenal haina rekodi nzuri sana katika michuano hii.

Raundi ya tatu ya kombe la Carabao itafanyika katikati ya wiki inayoanzia tarehe 21 ya mwezi wa tisa, na utakuwa baada ya kucheza na West Ham na kabla ya kucheza ugenini dhidi ya Liverpool.

Kutokana na mchezo dhidi ya Liverpool kuwa siku tatu tu baada ya mchezo huu, kuna uwezekanio mkubwa wa kwamba kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kuchezesha wachezaji wengi wa akiba katika mchezo huu.

 

Tupia Maoni Yako Hapo Chini