Arsenal kucheza na MK Dons leo usiku

Arsenal itacheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki leo usiku ikicheza na timu ya MK Dons kama sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Arsenal kucheza na MK Dons leo usiku

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa ni mchezo wa kwanza wa Arsenal katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambapo jumamosi ijayo watacheza na timu ya Liverpool katika kugombea ngao ya jamii.

Katika mchezo wa leo kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta anategemewa kupanga kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji makinda na baadhi ya wakongwe.

Arsenal walianza mazoezi mazoezi ya kujiandaa kwa msimu mpya jumamosi iliyopita ikiwa ni wiki mbili tu tangu kumalizika kwa msimu uliopita.

Ligi kuu ya uingeleza itaanza rasmi tarehe 12 ya mwezi wa tisa wakati Arsenal itakapokuwa ujenini kucheza na timu ya Fulham katika uwanja wa  Craven Cottage.

Mchezo wa kwanza wa Arsenal nyumbani utakuwa dhidi ya West Ham United wiki moja baadaye.

Unaweza kuangalia mchezo huo kupitia tovuti rasmi ya Arsenal https://www.arsenal.com/ kuanzia saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini