Arsenal vs Brentford-mtazamo wangu

Ndani ya muda mchache ujao timu ya Arsenal itacheza na timu ya Brentford katika mchezo wa kuwania kombe la Carabao, zifuatazo ni baadhi ya dondoo na mtazamo wangu kuhusu mchezo huu.

Brentford ina rekodi nzuri inapokutana na Arsenal

Kwa wale waliokuwa hawajui huu utakuwa ni mchezo wa kwanza Arsenal kucheza nyumbani katika michuano rasmi dhidi ya Brentford tangu mwaka 1947.

La ajabu zaidi ni kwamba timu hiyo ya daraja la kwanza ina rekodi bora linapokuja suala la michezo baina ya timu hizo mbili, timu hizo zimecheza mara 12,Brentford ameshinda mara 5, Arsenal ameshinda mara 4 na mara 3 wametoa sare.

Pia ikumbukwe ya kwamba mwaka huu kuna tetesi ya kwamba timu hizo zilicheza mchezo wa kirafiki kwa siri na Arsenal kufunga 2-1, ambapo inadaiwa ya kwamba Bernt Leno alifanya makosa yaliyosababisha magoli hayo na ndiyo sababu za kutokuwa kwenye kikosi cha kwanza.

Brentford siyo timu ya kuibeza Unai Emery anatakiwa apange kikosi kizuri na wachezaji wacheze kwa kujituma ili kuondoa aibu.

Pamoja na kwamba timu hiyo ya daraja la kwanza wana rekodi nzuri dhidi ya Arsenal, naamini kikosi cha Arsenal ni kipana na kina uwezo wa kupata ushindi bila ya matatizo makubwa.

Kwa upande wa kikosi kitakachocheza leo nategemea kuona kikosi kile kile kilichoanza katika mchezo wa Europa League kikiwa na mabadiliko mawili tu.

Eddie Nketiah akichukua nafasi ya Pierre Emerick Aubamayang na kinda mwingine Emile Smith Rowe akichukua nafasi ya Henrik Mkhitaryan.

Hiki ndicho kikosi ninachoamini kinaweza kuanza leo na kuleta ushindi.

Arsenal vs Brentford-mtazamo wangu

Utabiri Arsenal 3-0 Brentford, Nketia na Iwobi kufunga

Speak Your Mind

*