Arsenal vs Watford-Huu ni mchezo muhimu sana

Arsenal leo inacheza na Watford katika mchezo wa ligi kuu ya Uingeleza.Arsenal ambayo kwa sasa inafanya vizuri inategemewa kushinda mchezo huo na kuendelea kupaa katika mshimamo wa ligi.

Arsenal vs Watford-Huu ni mchezo muhimu sana

Watford wanashika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Uingelea baada ya kushinda michezo minne na kutoa sare katika mchezo mmoja msimu huu. Mchezo pekee waliopoteza ulikuwa ni ule waliocheza na Manchester United na pia ikumbukwe ya kwamba hii timu ilimfunga Totenham, hivyo Arsenal wanatakiwa kucheza kwa tahadhari kubwa.

Pia naamini huu ni mchezo mgumu zaidi ukilinganisha na timu nyingine 6 ambazo Arsenal hivyo ushindi katika mchezo wa leo sio tu utaifanya Arsenal iwe jii ya Watford, pia utasaidia kujenga hali ya kujiamini zaidi kwa wachezaji.

Pia ikumbukwe pia ya kwamba mwaka jana baada ya Arsenal kufungwa na Watford, nahodha wao Troy Deeney alisema ya kwamba timu ya Arsenal imekosa ”COJONES”, hivyo ni muhimu mno kwa wachezaji kujituma na kushinda mchezo huu ili wamuoneshe Deneey ya kwamba wana COJONES.

(kwa wale wasiojua COJONES ni neno la kiispania linalomaanisha PUMBU kwa kiswahili).

Taarifa ya majeruhi

.Sokratis Papastathopoulos amepita vipimo vya afya na anategemewa kucheza leo, kuna taarifa ya kwamba Emile Smith Rowe ana majeraha ambayo aliyapata katika mchezo wa Carabao Cup.

Kolasinac tayari yupo fiti,Jenkinso ameshaanza mazoezi,Dinos Mavropanos,Niles na Koscienly bado ni majeruhi na hawatahusika kabisa na mchezo huo, wachezaji waliobaki wote wapo fiti.

Kikosi kitakachoanza

Kwa kuwa  Sokratis Papastathopoulos yupo fiti, sitegemei mabadiliko kwenye kikosi kilichomfunga Everton wiki iliyopita.

Mtazamo wangu

Nategemea ya kwamba mabeki wa Arsenal watakuwa na vita kali ya kuwazuia Deeney na Gray ambao wana wanasifika kwa kutumia nguvu nyingi na kucheza rafu za mara kwa mara.Janmaat ataukosa mchezo huo kutoka na kuwa majeruhi, hivyo itawafanya wapangue kikosi chao kwa mara ya kwanza msimu huu na jambo hilo linaweza kuwasaidia Arsenal.

Iwapo Arsenal wataanza kwa kasi na kuepusha makosa ya kijinga naamini kabisha ya kwamba Arsenal itapata ushini wa saba na kuingia katika nne bora kwa mara ya kwanza msimu huu.

Utabiri

Naamini ya kwamba Arsenal ina kikosi bora na chenye uwezo wa kuifunga Watford, bado sina imani sana na safu ya ulinzi, ila naamini leo ushindi ni kwa Arsenal.

Utabiri wangu ni kwamba Arsenal watashinda mchezo huu kwa 3-1. Auba na Lacazette kutupia.

Je wewe mtazamo wako ni upi na unatabiri matokeo ya aina gani? tupia mawazo yako hapa chini.

Speak Your Mind

*