Arsenal vs Wolves-mambo matano niliyoyaona

Arsenal vs Wolves-mambo matano niliyoyaona

Juzi Arsenal ilicheza na timu ya Wolves na kufanikiwa kutoka sare ya kufungana goli 1-1,katika mchezo huo ambao Arsenal haikucheza vizuri kuna mambo mengi yalitokea na haya timu mambo matano ambayo mimi niliyaona na naamini yalichangia kwa kiasi kikubwa matokeo hao.

Mambo matano niliyoyaona

Bernd Leno alionesha ubora wake

Kila mtu anajua ya kwamba Bernd Leno ni bora linapokuja suala la kucheza mpira kwa miguu, lakini katika mchezo wa juzi alionesha pia ustadi wake katika kuzuia mashuti, kwangu mimi yeye ndiye aliyekuwa mchezaji bora katika mchezo huo, bila ya kudaka vizuri Arsenal ilikuwa inafungwa mchezo ule.

Mesut Ôzil alicheza nafasi tofauti

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, vituo vingi vya luninga vilimuweka mchezaji huyo kama namba 10 katika mfumo wa 4-2-3-1, lakini dakika chache baada ya kuanza mchezo huo nilimuona Mesut akicheza nyuma zaidi kama kiungo wa kati na si kiungo mshambuliaji kwangu mimi mfumo ulikuwa kama 4-2-1-3,naamini kocha alifanya mabadiliko hayo ili kuwadhibiti Wolves wakati wakifanya mashambulizi ya kustukiza, kitu ambacho alifanikiwa ila pia iliifanya timu ya Arsenal ishindwe kutengeneza nafasi za kufunga.

Upande wa kushoto ulivuja

Nimeangalia tena mchezo huo na nimeona ya kwamba mashambulizi mengi ya Wolves yalipitia upande wa kushoto wa Arsenal, Kolasinac ambaye sio mzuri sana kwenye kukaba na Aubamayang alikuwa hamsaidii sana, hivyo mara nyingi Kolasinac alikuwa akikabana na wachezaji wawili wa Wolves na kufanya Arsenal kupokea mashambulizi mengi kutoka upande huo.

Kubadilika kwa mifumo

Suala la kuvuja kwa upande wa kushoto lilionwa na kocha Unai Emery na kutokana na kutokuwa na wachezaji wa kuziba upungufu huo akaamua kubadili mfumo, akamtoa Iwobi na kumuingia Matteo Guendouzi na kubadilisha mfumo kutoka 4-2-3-1 na kwenda 4-3-1-2, Torreira akiwa kati, kushoto akacheza Xhaka na kulia Guendouzi na hali hii ilisaidia kukata mashambulizi upande wa kushoto kwa Arsenal.

Baada ya kuingia kwa Ramsey na Mkhitryan alibadili mfumo tena na sasa kucheza 4-2-2-2, huku wachezaji hao wakicheza kama viungo washambuliaji,kazi yao kubwa ilikuwa ni kucheza kwenye mashimo waliyokuwa wakiacha Wolves ambao walikuwa wakilinda goli lao na wachezaji saba.

Mabadiliko hao yalizaa matunda baada ya Ramsey na Mkhitryan kuungana na kusaidia kupatikana kwa goli la kusawadhisha.

Safu ya Ushambuliaji Ilikuwa butu

Kama kuna siku safu ya ushambuliaji iliiangusha Arsenal, juzi ilikuwa ndiyo hiyo siku, Wolves walikuwa wanakaba hadi kivuri na safu ya ushambuliaji ya Arsenal ilishindwa kabisa kupata nafasi za kufunga.

Kama kumbukumbu zangu hazinidanganyi nafasi kubwa ambayo Arsenal walipata ilikuwa ni ile ambayo Aubamayang aligongesha mwamba.

Katika mchezo huo Arsenal ilitengeneza nafasi za kufunga tano tu ndano ya dakika 90, Wolves walienda Emirates wakiwa na mkakati kabambe wa kuifunga Arsenal na kidogo wafanikiwe.

Neno la mwisho

Najua Arsenal wana mechi tatu za ligi kuu bila kushinda na kuna baadhi ya mashabiki wa Arsenal wameanza kuwa na wasiwasi lakini ikumbukwe pia ya kwamba hii timu bado ndiyo inasukwa na ina michezo 15 bila ya kufungwa. Kwa sasa wachezaji wengi wameshajiunga na timu zao za taifa.

Speak Your Mind

*