Arsenal vs Wolves-Mtazamo wangu

Leo katika uwanja wa Emerates kutakuwa na mchezo kati ya Arsenal na Wolves, huu ni mchezo unaokuja baada ya Arsenal kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Sporting Lisbon Alhamisi iliyopita.

Kwa sasa Arsenal inashika nafasi ya tano kwenye ligi na wapinzani wao wa karibu Chelsea, Liverpool, Totenham na Manchester City wote wana mechi nyepesi hivyo ushindi katika mchezo huu ni muhimu ili kuendelea kuwafukuza wapinzani kwa karibu.

Arsenal vs Wolves-Mtazamo wangu

Taarifa za majeruhi

Danny Welbeck alipata majeraha na anaweza kuwa nje kwa msimu mzima, Nacho Monreal amepona ila sidhani kama atacheza leo.Stephan Lichtsteiner ana matatizo ya msuli na anaweza akakosa mchezo wa leo.Mohamed Elneny, Laurent Koscielny na Dinos Mavropanos bado ni majeruhi.

Kuhusu Wolves

Pamoja na kwamba Wolves ni timu iliyopanda daraja msimu uliopita, si timu ya kubeza, kwani chini ya kocha Nuno Espiritu Santo wamekuwa wakicheza vizuri na kwa kasi.

Timu hiyo ambayo inacheza soka la Kireno (wamiliki na wachezaji wake wengi ni wareno) ni timu ambayo imekuwa ikizisumbua timu kubwa, ikimbukwe ya kwamba waliweza kutoka sare na Manchester City na wiki iliyopita kidogo wawaaibishe Totenham, hivyo Arsenal itabidi icheze kwa umakini mkubwa ili kuweza kushinda mchezo wa leo.

Pamoja na yote hayo Wolves hawana rekodi nzuri katika uwanja wa Emerates kwani hawajashinda katika michezo 15 ambapo wametoa sare mitatu na kufungwa 12, pia Arsenal ina rekodi nzuri linapokuja suala la kucheza na timu ambazo zimetoka kupanda daraja.

Kikosi

Hiki ndicho kikosi ninachotegemea ya kwamba kitaanza katika mchezo wa leo.

kikosi

Utabiri

Wolves ni timu nzuri, ina kocha na wachezaji wazuri lakini naamini ya kwamba baada ya Arsenal kushinda mchezo mmoja tu katika michezo minne, ni wakati wa kurudi kwenye ushindi hivyo naamini ya kwamba Arsenal itashinda 3-1,Auba na Laca kufunga.

Je wewe unatabiri matokeo ya aina gani? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*