Arsenal yafungwa 3-2 na Aston Villa

Arsenal ilifungwa goli 3-2 na timu ya Aston Villa katika mchezo wa kirafiki uliofanyika nyuma ya pazia katika uwanja wa Emirates.

Arsenal yafungwa 3-2 na Aston Villa

Katika mchezo huo wa kujiandaa ya ligi kuu ya Uingeleza inayotegemewa kuanza jumamosi ijayo magoli yote mawili ya Arsenal yalifunga na nahodha wake Pierre Emerick Aubamayang.

Kufungwa kwa Arsenal katika mchezo huo sio jambo la ajabu kwani timu ilichezesha kikosi mchanganyiko wa wachezaji wakongwe na vijana huku wachezaji 9 wa kikosi cha kwanza wakikosa mchezo huo kutokana na kuwa na majukumu na timu zao za taifa.

Arsenal ilicheza mchezo mwingine wa kujipima nguvu jumanne iliyopita na kuifunga timu ya Queens Park Rangers kwa jumla ya goli 4-3.

Katika mchezo wa jana kiungo wa Arsenal Mesut Özil alicheza, ikumbukwe ya kwamba Özil alikuwa hajaichezea Arsenal tangu ligi ianze upya kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Pia mchezaji Willian aliyesajiliwa msimu huu akitokea Chelsea, Dani Ceballos ambaye juzi alitangazwa kurudi Arsenal pia walicheza katika mchezo wa jana.

Kwa mujibu wa mwandisha wa habari Charles Watts kutoka Goal.com Villa ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata goli baada ya Douglas Luiz kufunga goli la kuongoza na zikiwa zimebaki dakika chache kwenda mapumziko, Aubamayang aliisawazishia Arsenal.

Villa walipata goli la pili kupitia kwa Jacob Ramsey kabla ya Aubamayang kuisawazishia tena timu ya Arsenal kupitia mkwaju wa penati.

Dakika chache baadaye Ramsey aliifungia Astoni Villa goli la tatu na la ushindi katika mchezo huo.

 

Tupia Maoni Yako Hapo Chini