Arsenal yaifunga Cardiff City goli 3-2

Arsenal jana iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya Cardiff City kwa jumla ya magoli 3-2.

Arsenal yaifunga Cardiff City goli 3-2

Arsenal ambao wamekuwa wakipata matokea mabovu wanapocheza katika viwanja vya ugenini jana walihitaji kufanya kazi ya ziada kuwafunga Cardiff City ambao walicheza kwa kujituma sana.

Katika mchezo huo tulishuhudia Unai Emery kwa mara ya kwanza akiwaanzisha pamoja Alexandre Lacazette na Aubamayang na pia katika mchezo huo tulishuhudia Mesut Özil akianza mchezo huo baada ya kukosa mchezo dhidi ya West Ham kutokana na kuwa majeruhi.

Alikuwa ni beki wa Arsenal Shkodran Mustafi aliyeipatia Arsenal goli la kuongoza baada ya kupiga kwa kichwa kona iliyopigwa na Granit Xhaka.Lakini Cardiff walifanikiwa kusawazisha sekunde kadhaa kabla ya kuisha kwa kipindi cha kwanza baada ya Victor Camarasa kuifungia goli la kusawazisha.

Hadi mapumziko Cardiff City 1-1 Arsenal.

Katika kipindi cha pili Arsenal walipata goli la pili kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang akimalizia pasi ya kisigino ya Lacazette lakini goli hilo halikudumu sana kwani kwa mara nyingine tena Cardiff walisawazisha safari hii kupitia kwa Danny Ward.

Alikuwa ni mshambuliaji Alexandre Lacazette aliyewainua vitini mashabiki wa Arsenal katika dakika ya 81 baada ya kuifungia goli la tatu na la ushindi.

Hadi mwisho wa mchezo huo Cardiff City 2-3 Arsenal.

Lacazette ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Unaweza kuangalia magoli ya mchezo huu hapa chini.

 

Speak Your Mind

*