Arsenal yaifunga Qarabag 3-0

Emile Smith Rowe, Matteo Guendouzi na Sokratis walifunga kwa mara ya kwanza dhidi ya timu ya Qarabag na kuipa Arsenal ushindi wa goli 3-0.

Arsenal yaifunga Qarabag 3-0

Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli la Soktratis dhidi ya Qarabaq hapo jana.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery alipanga kikosi kizito katika mchezo huo ambapo wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza walianza ama kukaa katika benchi la wachezaji wa akiba.

Alikuwa ni beki Mgiriki Sotratis aliyekuwa wa kwanza kuipatia Arsenal goli la kwanza baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Nacho Monreal baada kufuatia kona iliyopigwa na Mohamed Elneny.

Sokratis anakuwa mchezaji wa kwanza ambaye hajafundishwa na Arsene Wenger kuifungia Arsenal goli katika mechi ya ushindani toka mwezi wa tano mwaka 1996.

Baada ya goli hilo Qarabaq waliamka na kuanza kishambulia Arsenal kwa nguvu, lakini umakini wa mlinda mlango wa Arsenal, Bern Leno ulisaidia kuwafanya Arsenal waende mapumziko wakiongoza kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kufanya mabadiliko, ambapo Nahodha wa jana Nacho Monreal alitolewa na Nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Lucas Torreira.

Kuingia kwa Torreira kulibadilisha hali ya mchezo na Arsenal ilianza kutawala mchezo huo hasa sehemu ya kiungo.

Arsenal walifanikiwa kupata goli la pili baada ya Alex Iwobi kuwahadaa wachezaji wa Qarabaq na kumpasia Emile Smith Rowe ambaye bila kukosea aliukwamisha wavuni.

Goli hilo lilikuwa ni goli la kwanza kwa kinda huyo kuifungia timu ya wakubwa ya Arsenal na linamfanya awe mchezaji wa kwanza aliyezaliwa baada ya mwaka 2000 kuifungia Arsenal goli katika mechi ya ushindani.

Alikuwa ni kinda mwingine Matteo Guendouzi aliyeifungia goli la tatu baada ya kupokea mpira kutoka kwa Alexandre Lacazette na kupiga shuti lililoenda moja kwa moja wavuni.

Hilo lilikuwa goli la kwanza la Guendouzi katika jezi za Arsenal na pia ni goli lake la kwanza tangu aanze kucheza soka la ushindani.

Hadi mwisho wa mchezo Arsenal 3-0 Qarabag.

Ushindi huo unaiweka Arsenal kileleni mwa kundi lake na unaifanya timu iwe katia nafasi nzuri ya kushika nafasi ya kwanza katika kundi.

Arsenal itacheza tena jumapili mchana dhidi ya Fulham katika ligi kuu ya Uingeleza kabla ya kupumzika kwa wiki pili kupisha mechi za kimataifa.

Magoli na sehemu muhimu za mchezo wa jana unaweza kuangalia katika video iliyopo hapo chini. #COYG

Comments

  1. Ajelly Israel says:

    Congratulation to Arsenal

Speak Your Mind

*