Arsenal yaipiga mkono Fulham

Arsenal jana ilipata ushini mwingine baada ya kuifunga timu ya Fulham kwa jumla ya magoli 5-1 na rasmi kuingia ndani ya nne bora.

Arsenal yaipiga mkono Fulham

Kulikuwa na mambo mengi ya kufurahisha katika safari hiyo ya Craven Cottage, cha kwanza kilikuwa ni jinsi Unai Emery alivyoibadilisha timu na kuwaacha baadhi ya wachezaji muhimu nje.

Mesut Ôzil alikosa mchezo huo kutokana na kuwa na maumivu ya mgongo, Aubamayang na Aaron Ramsey walianzia katika benchi la wachezaji wa timu ya akiba.

Arsenal walikianza kipindi cha kwanza taratibu,na ilipata goli la kwanza kupitia kwa Alexandre Lacazette ambaye alipata mpira ndani ya eneo la hatari na kufanikiwa kugeuka na kufunga.

Ikiwa imebaki dakika moja kwenda mapumziko beki wa Arsenal, Nacho Monreal alifanya kosa na kupoteza mpira ambao ulimkuta Schurlle aliyewafungia Fulham goli la kusawazisha na kufanya timu hizo kwenda mapumziko 1-1.

Kipindi cha pili Arsenal walibadilika na kucheza soka la hali ya juu mno, Lacazette alifunga goli la pili kwa shuti la mbali ambalo golikipa wa Fulham alishindwa kulizuia.

Mambo yalibadilika zaidi baada ya Aubamayang na Ramsey kuingia, sekunde chache baada ya kuingia Ramsey alianzisha mpira kutokea upande wa beki wa kulia wa Arsenal na kuumalizia kwa bonge la goli, goli la Ramsey ni moja ya magoli bora kabisa kuwahi kufungwa na Arsenal.

Auba alifunga magoli mengine mawili na kuifanya siku ya jana kuwa moja ya siku bora kabisa kwa mashabiki wa Arsenal.

Hadi mwisho wa mchezo huo Arseanal 5-1 Fulham.

Baada ya mchezo huo  kutakuwa na mapumziko ya wiki mbili ili kupisha michezo ya kimataifa na mchezo unaofuatia wa Arsenal ni dhidi ya Leicester City utakaofanyika jumatatu ya tarehe 22 ya mwezi huu.

 

Speak Your Mind

*