Arsenal yakamilisha usajili wa Beki Gabriel Magalhaes

Arsenal imekamilisha usajili wa beki wa kati raia wa Brazil, Gabriel Magalhaes akitokea katika timu ya Lille ya Ufaransa.

Gabriel

Gabriel pichani juu ambaye ni beki wa kati anayecheza upande wa kushoto amesajiliwa na Arsenal katika usajili unaokadiliwa kufikia paundi milioni 27 ( Euro millioni 30) na amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu ya Arsenal.

Mchezaji huyo alitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal mida ya saa 12 jioni kupitia video iliyowekwa katika ukurasa ramsi wa Arsenal katika Youtube kabla ya kutangazwa katika mitandao mingine ya kijamii na tovuti ya Arsenal.

Mchezaji huyo hataanza mazoezi na wachezaji wenzake hadi wiki ijayo kwani kufuatia mlipuko wa virusi vya Korona anatakiwa akae peke yake siku 14 kabla hajaanza kuchanganyika na wachezaji wengine.

Gabriel anakuwa mbrazil wa pili kujiunga na Arsenal msimu huu akiufuatia Willian ambaye alijiunga na Arsenal mwezi uliopita akitokea Chelsea.

Karibu katika chama la wana Grabriel

COYG

Tupia Maoni Yako Hapo Chini