Arsenal yakamilisha usajili wa Stephan Lichtsteiner

Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji kutoka Juventus,Stephan Lichtsteiner. Mchezaji huyo ambaye alikuwa amemaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Italia anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Arsenal yakamilisha usajili wa Stephan Lichtsteiner

Beki huyo wa kimataifa wa Uswisi anasajiliwa akiwa na uzoefu mkubwa kwani amekuwa nahodha wa nchi yake na pia ameshindwa ubingwa wa ligi kuu ya Italia mara saba katika miaka saba aliyoichezea timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye ni beki wa kulia mwenye uzoefu mkubwa  aliichezea Juventus katika michezo zaidi ya 250, pia ameichezea timu yake ya taifa katika michezo 99 pia amekuwa nahodha wa timu yake ya taifa tangu mwaka 2016.

Stephan Lichtsteiner ambaye atavaa jezi namba 12 katika kikosi cha Arsenal msimu ujao ni mtu wa kazi ambaye ataleta changamoto na uongozi katika timu hasa sehemu ya ulinzi ambayo ilionesha kuyumba sana katika msimu uliopita.

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery alisema “Stephan analeta uzoefu na uongozi katika timu yetu, ni aina ya mchezaji mwenye uwezo mkuwa na anajituma sana uwanjani,Stephan atatufanya tuwe bora nje na ndani ya uwanja ”.

Karibu katika chama la wana Stephan Lichtsteiner.

 

Speak Your Mind

*