Arsenal yamsajili mtoto mwenye kipaji kikubwa Jayden Adetiba

Wakati dirisha la usajili likiwa limefungwa, Arsenal imeendelea kuwa bize katika kutafuta wachezaji wa kuichezea timu hiyo kwa sasa ama miaka ijayo baada ya kukamilisha usajili wa Jayden Adetiba, mtoto mwenye umri wa miaka 9 kutosa Afrika ya Kusini.

Arsenal yamsajili mtoto mwenye kipaji kikubwa Jayden Adetiba

Jayden Adetiba, ambaye alizaliwa nchini Nigeria lakini amekuwaa akiishi nchini Afrika ya kusini kwa miaka miwili sasa amesajiliwa na chuo chwa soka cha Arsenal baada ya kufanya majaribio ya wiki tano jijini London.

Adetiba ambaye pia amewahi kuishi nchini Uingeleza amekuwa akiichezea timu ya shule ya soka ya SuperSport United Soccer School ya mjini Cape Town.

Mchezaji huyo anayetokea katika familia inayochipukia kisoka kwani kaka yake mkubwa tayari anaichezea timu ya chuo cha soka ya Blackburn Rovers kwa mwaka wa tatu sasa.

Adetiba ambaye ni shabiki wa Arsenal alisema ya kwamba kujiunga na timu hiyo ni kutimia kwa ndoto zake.

” Asante Mungu na Wazazi wangu kwa hili,” mchezaji huyo alinukuliwa na gazeti la  The Sun. “Nina furaha kubwa. Nitafanya mazoezi mara tatu kwa wiki na nitakuwa nikicheza mechi za ushindani mwishoni mwa juma.

“Kitu cha kufurahisha ni kwamba, Siku zote nimekuwa shabiki wa Arsenal na nitafanya juhudi kubwa ili nimeze kucheza katika kikosi cha kwanza.”

Hakika huu ni usajili kwa ajili ya miaka mingi ijayo, je dogo atatimiza ndoto zake za kukichezea kikosi cha kwanza cha Arsenal? ni suala la kusubiri muda ndiyo utatoa jibu la hili swali.

Speak Your Mind

*