Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Arsenal imetangaza kikosi cha wachezaji 25 ambao watasafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki ili kujiandaa na msimu ujao.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Wachezaji wengi wa Arsenal walianza mazoezi tangu mwanzoni mwa mwezi huu, na sasa wataungana na wachezaji wengine ambao walitolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia,Mesut Ozil, Mohamed Elneny na Alex Iwobi.

Timu itaondoka London jumapili na itaelekea Singapore ambapo itashiriki katika kombe la International Champions Cup, dhidi ya Atletico Madrid, alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu na dhidi ya Paris Saint Germain, jumamosi tarehe 28 ya mwezi huu.Michezo yote itaanza saa 7:30 kwa saa za Singapore.

Wachezaji wapya Bernd Leno, Sokratis na Matteo Guendouzi wote wanasafiri na kikosi , pia wachezaji waliokuwepo msimu uliopita kama  Pierre-Emerick Aubameyang, Hector Bellerin, Petr Cech, Calum Chambers, Rob Holding, Alexandre Lacazette, Ainsley Maitland-Niles, Henrikh Mkhitaryan, Shkodran Mustafi na Aaron Ramsey nao pia wanasafiri.

Katika kikosi hicho mchezaji Jeff Adelaide ameachwa huku kukiwa na tetesi za kwamba anaenda kwa mkopo,Chuba Akpom pia ameachwa kwani kuna tetesi ya kwamba anakaribia kuhamia timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la paundi milioni 2.

Kikosi kamili ni kama kinavyoonekana kwenye picha.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

 

 

Speak Your Mind

*