Arsenal Yavunja mkataba wa Henrikh Mkhitaryan

Arsenal Yavunja mkataba wa Henrikh Mkhitaryan

Timu ya Arsenal imevunja mkataba wa kiungo Henrikh Mkhitaryan na sasa atajiunga na timu ya Roma ya Italia kwa msimu ujao wa ligi.

Kuvunjwa kwa mkataba huo kumefikiwa baada ya mchezaji huyo na wakala wake kukaa na Uongozi wa Arsenal, katika makubariano hayo mchezaji huyo ataondoka Arsenal bila ada ya uhamisho na Arsenal haitamlipa mchezaji huyo posho ya kumaliza mkataba ( Arsenal huwalipa posho ya kumaliza mkataba wachezaji wote wanaomaliza mikataba yao).

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Armenia alikiunga na Arsenal mwezi wa kwanza mwaka 2018 na katika mchezo wake wa kwanza alipiga pasi za mwisho tatu na kuisaidia Arsenal kuifunga Everton 5-1.

Katika kipindi chote alichoichezea Arsenal,Henrikh Mkhitaryan alifunga magoli tisa na kutoa pasi za mwisho za magoli 13 akiisaidia Arsenal kufikia fainali ya kombe la Europa League mwaka 2019.

Kutokana na mchezaji huyo kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza aliondoka na kujiunga na timu ya Roma kwa mkopo wa mwaka mmoja lakini sasa atajiunga na timu hiyo ya Italia moja kwa moja.

Mkhi alikuwa anavaa jezi namba 7 Arsenal amabayo kwa sasa inavaliwa na kinda Bukayo Saka.

Kila la heri AHenrikh Mkhitaryan

Tupia Maoni Yako Hapo Chini