Rasmi Jeff Reine-Adelaide ajiunga na Angers

Mchezaji kiungo wa Arsenal Jeff Reine-Adelaide, amejiunga na timu ya Angers, inayoshiriki ligi ya Ufaransa Ligue 1, ambayo aliichezea kwa mkopo msimu ulioisha.

Rasmi Jeff Reine-Adelaide ajiunga na Angers

Katika taarifa rasmi ya Arsenal, hawajasema mchezaji huyo ameuzwa kwa kiasi gani cha pesa lakini inasemekana timu hiyo ya Ufaransa imetoa dau la paundi milini 2 ili kumpata mchezaji huyo.

Jeff aliachwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichopo Singapore kucheza michezo yake ya kirafiki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Arsenal mwezi wa saba mwaka 2015 mwezi wa saba akitokea timu ya ligue 2, Racing Club ambayo aliichezea katika timu za vijana na za wachezaji wa akiba.
Jeff aliichezea Arsenal katika michezo nane ya kikosi cha kwanza kwa miaka mitatu aliyokaa katika timu.Katika msimu wa mwaka 2016/17 alicheza michezo mitatu kati ya minne katika michuano ya kombe la ligi kabla ya kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 23.

Mwishoni mwa msimu huo alipata majeraha ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa karibu mwaka mzima na aliporudi akaenda kwa mkopo na inaonekana ameshindwa kumshawishi kocha mpya Unai Emery na hivyo Arsenal kuamua kumuuza.

Sisi kama mashabiki wa Arsenal tunamtakia Jeff kila la heri katika timu yake mpya .

 

Mechi za kirafiki-Arsenal 1-1 Atletico Madrid

Arsenal imeendelea kucheza mechi za kirafiki kujiandaa na msimu ujao baada ya leo kucheza na timu ya Atletico Madrid ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 na Arsenal kufungwa kwa mikwaju ya penati.

Mechi za kirafiki-Arsenal 1-1 Atletico Madrid

Arsenal ilicheza mfumo wa 4-3-3, Rob Holding Mustafi,Kolanasic na Bellerin waliunda mabeki wanne, Ramsey,Gendauzi na Emile Smith Rowe waliunda safu ya kiungo na Lacazette,Reiss Nelson na Auba waliunda safu ya ushambuliaji.

Arsenal waliuanza mchezo huo kwa kasi huku kiungo kinda Emile Smith Rowe akionesha umahiri wa hali ya juu,ambapo mara nyingi alionekana kuwasumbua wachezaji wa Atletico Madrid.

Baada ya dakika ya 25 Atletico walianza kucheza vizuri huku Arsenal wakionekana kuanza kupunguza moto,Lacazette alikaribia kufunga mara mbili katika kipindi cha kwanza lakini walikuwa ni Atletico Madrid waliopata goli ya kuongoza baada ya Vietto kupiga mpira wa kichwa na kumuacha golikipa wa Arsenal Bernd Leno akiruka bila ya mafanikio.

Smith Rowe ambaye alicheza vizuri katika kipindi cha kwanza alianza vizuri kipindi cha pili baada ya kifungia Arsenal goli la kusawazisha baada ya kuwapiga chenga wachezaji watatu wa Atletico Madrid na kuachia kombora ambalo golikipa wao alishindwa kulitoa.

Baada ya hapo timu zote zilifanya mabadiliko makubwa na kuufanya mchezo huo kupoa na hadi mwisho wa mchezo ilikuwa Arsenal 1-1 Atletico Madrid.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare, zilipigwa penati ambapo Arsenal walikosa penati 3 (waliokosa ni Mkhitaryan,Nketiah na Joe Willock na hivyo Arsenal kufunga 3-1 kwenye penati.

Katika mchezo huo wachezaji walionivutia zaidi ni Matteo Gendauzi na Emile Smith.

Arsenal itaendelea na michezo ya kirafiki jumamosi ambapo itapambana na timu ya PSG kutoka Ufaransa.

Atletico Madrid v Arsenal-maandalizi ya msimu ujao yanaendelea

Arsenal itamenyana na Atletico Madrid leo mchana katika mechi ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa kwa msimu ujao.

Atletico Madrid v Arsenal-maandalizi ya msimu ujao yanaendelea

Timu hizo mbili zilipambana miezi mitatu iliyopita katika nusu fainali ya kombe la Europa League ambapo Atletico walishinda kwa jumla ya magoli 2-1 na kuingia fainali na hatimaye kubeba kombe hilo.

Emery tayari ameshaiongoza Arsenal katika michezo miwili dhidi ya Boreham Wood  na Crawley Town, lakini huu utakuwa ndiyo mchezo wake wa kwanza mkubwa na nje ya Uingeleza.

Katika mechi hiyo itakayofanyika mchana wa leo,Arsenal inategemewa kutumia wachezaji wake wote, akiwemo Mesut Ozil ambaye amejiunga na timu hivi karibuni akitokea likizo baada ya kushiriki kombe la dunia.

Pia nategemea kuona katika mchezo huu wachezaji vijana kama Reiss Nelson na Smith Rowe wakipewa nafasi ya kuonesha ufundi wao.

Atletico Madrid ambaye inafundishwa na Muargentina Diego Simeone nayo itakuwa bila ya wachezaje wakali baada ya kushiriki katika kombe la Dunia,wachezaji ambao hawatacheza mchezo huo ni Antoine Griezmann, Diego Costa, Diego Godin, Jose Gimenez na Sime Vrsaljko.

Mchezo huo utaoneshwa moja kwa moja na ukurasa wa Arsenal.com au kwenye app ya Arsenal,vyote viwili ni bure kutumia.

Reiss Nelson-Wachezaji vijana wanaweza kufanikiwa chini ya Unai Emery

Mchezaji wa Arsenal Reiss Nelson,amesema ya kwamba kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery amewaaminisha wachezaji vijana wa timu hiyo ya kwamba wanaweza kufanikiwa chini ya uongozi wake.Nelson alisema hayo katika mahojiano yaliyoandikwa katika mtandao wa standard.co.uk.

Reiss Nelson, mwenye umri wa miaka 18, ni mmoja ya wachezaji vijana waliopo kwenye kikosi kiichopo nchini Singapore kwa ziara ya mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.

Reiss Nelson kushoto na Wilock wakiwa mazoezini

Reiss Nelson kushoto na Wilock wakiwa mazoezini

Nelson alicheza michezo 16 msimu uliiopita, lakini alishindwa kuonesha kiwango kama anachoonesha katika timu za vijana,lakini hii inaweza ikatokana na kucheza nafasi tofauti.
Mashabiki wengi wa Arsenal wanadai ya kwamba Reiss Nelson ni mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika chuo cha soka cha Arsenal cha Hale End tangu Jack Wilshere.
Kwa sasa Nelson ana imani ya kwamba kocha mkuu atampa nafasi ya kucheza ili aweze kuonesha uwezo wake.

“Mazoezi yamekuwa mazuri na Emery amekuwa akitusaidia katika sana katika uwanja wa mazoezi,”  Nelson alisema.

“anategemea kuwatumia wachezaji vijana na kuwasaidia ili wacheze vizuri ili wafikiri ya kwamba wanaweza kufanya vizuri chini ya utawala wa kocha mpya.”

Nelson sio mchezaji kijana pekee aliyesafiri na timu hiyo wachezaji wengine vijana waliopo kwenye kikosi hicho ni, Konstantinos Mavropanos,Eddie Nketiah na Emile Smith Rowe

Tetesi-Ivan Gazidis kutimkia AC Milan

Mtendaji mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis yupo mbioni kujiunga na timu ya AC Milan akiwa kama mtendaji mkuu wa timu hiyo.

Tetesi-Ivan Gazidis  kutimkia AC Milan

Taarifa kutoka Italia zinaelezea ya kwamba kampuni ya kimarekani iitwayo Elliott Management, imechukua umiliki wa timu hiyo ya Italia baada ya mmiliki wake wa zamani Li Yonghong kushindwa kulipa deni la paundi milioni 28.

Mwandishi wa habari Gianluca Di Marzio na kituo cha luninga cha Sky Italia wanahabarisha ya kwamba baada ya mkutano jijini London jumatatu hii.Mtendaji mkuu wa Roma Umberto Gandini atajiunga na timu hiyo kama Meneja wa timu.

Mbrazil Leonardo atajiunga na timu hiyo kama mkurugenzi wa Ufundi na Ivan Gazidis, atajiunga kama mtendaji mkuu wa timu hiyo.

Kwa sasa Gazidis yupo nchini Singapole akiwa na kikosi cha Arsenal katika michezo ya kirafiki kujiandaa na msimu ujao.

Gazidis ndiye aliyesimamia mageuzi ya Arsenal baada ya kuondoka kwa kocha mkongwe Arsenal Wenger na baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 10 ndiye kiongozi wa ngazi ya juu aliyekaa muda mrefu katika timu, hivyo kuondoka kwake kunaweza kuifanya Arsenal kuteteleka.

Mimi binafsi siamini kama Gazidis ataondoka kwani yeye ndiye aliyefanikisha mipango ya kumuondoa Arsene Wenger, na kapata madaraka aliyokuwa anayataka, sioni sababu ya kuhamia AC Milan, kwani kwa sasa Arsenal ni timu kubwa na ina pesa zaidi kuliko Milan.

 

 

Mesut Ozil ajiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani

Kiungo wa Arsenal,Mesut Özil, ametangaza kuachana na soka la kimataifa baada ya kutangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani.

Mesut Ozil ajiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani

Ozil ambaye alitupiwa gunia la misumari baada ya timu ya taifa ya Ujerumani kutolewa katika hatua ya makundi ameandika wakala mrefu unaoelezea matukio yaliyopekea kufikia uamuzi huo.

Katika wakala huo aliandika  “Kwa moyo mzito na baada ya kufikiria kwa muda mrefu baada ya matukio yaliyotokea hivi karibuni, sitaki kuendelea kuichezea nchi ya Ujerumani katika mechi za kimataifa baada ya kufanyiwa vitengo vya ubaguzi na kukosewa heshima.

“Nilikuwa navaa jezi ya ya timu ya taifa kwa furaha na heshima kubwa.

“Ilikuwa ni vigumu kufikia uamuzi huu kwa sababu mara zote nimejitolea kwa moyo wote kuwasaidia wachezaji wenzangu, makocha na watu wema wa Ujerumani.

“Lakini baada viongozi wa ngaji ya juu wa chama cha soka cha Ujerumani kutonitendea vyema, kudharau asili yangu ya Uturuki na kwa manufaa yao wenyewe na kuingiza siasa katika mambo ya soka nimeona ni bora nipumzike kwa sasa.

“Mimi ni mchezaji wa soka na sintokaa niangalie bila kujibu.

“Ubaguzi wa rangi haukubailiki”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameshaichezea Ujerumani katika michezo 92, ameifungia magoli 23 katika miaka 9 aliyoichezea timu hiyo.

Alikuwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichotwaa kombe la Dunia mwaka 2014, nchini Brazil.

Sisi kama mashabiki wa Arsenal tunaunga mkono uamuzi wa Mesut Özil,kwani tunaamini mwaka 2018 huwezi kumbagua mtu kwa ajili ya sehemu ya kuzaliwa,rangi ya ngozi yake au dini yake.

Tetesi za usajili Arsenal-Yann Sommer-Kingsley Coman-Ospina na Akpom

Wakati Arsenal kesho ikitegemewa kusafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki,Vyombo vingi vya habari vimeendelea kuihusisha Arsenal na usajili wa wachezaji mbalimbali.Katika tetesi za usajili wa Arsenal leo tunakuletea taarifa kuhusu Yann Sommer,Kingsley Coman, David Ospina na Chuba Akpom.

Yann Sommer

Yann Sommer

Yann Sommer yupo katika mazungumzo na Arsenal

Gazeti la Marca linaandika ya kwamba Arsenal wapo katika mazungumzo ya kumsajili golikipa kutoka Uswisi,Yann Sommer.

Habari hizo zinakuja huku tayari Arsenal ikiwa imeshamsajili Bernd Leno kwa dau la paundi milioni 19, huku ikiwa na makipa wengine watatu.Martinez,Ospina na Cech.

Sioni Arsenal ikisajili kipa mwingine labda Ospina na Cech wauzwe, pia Barcelona inasemekana inataka kumsajili golikipa huyo wa kimataifa wa Uswisi.

Kingsley Coman

Inasemekana ya kwamba Arsenal ipo sokoni kutafuta winga mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kukokota mpira,na jina la Kingsley Coman, linaendelea kutajwa.Vyombo vingi vya habari vinadai ya kwamba tayari Arsenal imetuma ofa mbili za kumsajili mchezaji huyo lakini zote zilikataliwa na timu yake ya Bayern Munich.

David Ospina

Inavyoonekana ni kwamba siku za David Ospina kuwa golikipa wa Arsenal zimefikia ukingoni,magazeti mengi ya kiingeleza yanahabarisha ya kwamba anakaribia kutua Besiktas, huku pia kukiwa na taarifa ya kwamba timu za Fulham na Tigres ya Mexico zinamuwania golikipa huyo.

Chuba Akpom

Mshambuliaji wa Arsenal, Chuba Akpom yupo karibu na kujiunga na timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la uhamisho linalokadiliwa kufikia paundi milioni 2.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Nigeria ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal, na hayupo katika kikosi cha Arsenal kinachosafiri kesho kuelekea Singapore.

Baada ya kuchezea timu nyingi kwa mkopo inaonekana kwa sasa Arsenal wanampango wa kuachana naye moja kwa moja.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizopata kwa siku ya leo, zingine tukijaaliwa.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Arsenal imetangaza kikosi cha wachezaji 25 ambao watasafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki ili kujiandaa na msimu ujao.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Wachezaji wengi wa Arsenal walianza mazoezi tangu mwanzoni mwa mwezi huu, na sasa wataungana na wachezaji wengine ambao walitolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia,Mesut Ozil, Mohamed Elneny na Alex Iwobi.

Timu itaondoka London jumapili na itaelekea Singapore ambapo itashiriki katika kombe la International Champions Cup, dhidi ya Atletico Madrid, alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu na dhidi ya Paris Saint Germain, jumamosi tarehe 28 ya mwezi huu.Michezo yote itaanza saa 7:30 kwa saa za Singapore.

Wachezaji wapya Bernd Leno, Sokratis na Matteo Guendouzi wote wanasafiri na kikosi , pia wachezaji waliokuwepo msimu uliopita kama  Pierre-Emerick Aubameyang, Hector Bellerin, Petr Cech, Calum Chambers, Rob Holding, Alexandre Lacazette, Ainsley Maitland-Niles, Henrikh Mkhitaryan, Shkodran Mustafi na Aaron Ramsey nao pia wanasafiri.

Katika kikosi hicho mchezaji Jeff Adelaide ameachwa huku kukiwa na tetesi za kwamba anaenda kwa mkopo,Chuba Akpom pia ameachwa kwani kuna tetesi ya kwamba anakaribia kuhamia timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la paundi milioni 2.

Kikosi kamili ni kama kinavyoonekana kwenye picha.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

 

 

Wachezaji vijana wa Arsenal na nafasi yao katika msimu ujao

Wakati Arsenal ikiendelea kujiandaa na msimu mpya wa ligi, kuna baadhi ya wachezaji vijana ambao wameonesha matumaini makubwa ya kwamba wanaweza kuwa kwenye mipango ya kocha Unai Emery katika ligi kuu na michezo mingine,leo nakuletea wachezaji  vijana wa Arsenal na nafasi zao katika timu.

Konstantinos Mavropanos

Beki huyu mwenye umri wa miaka 20 alisajiliwa mwezi wa kwanza mwaka huu, mipango ilikuwa ni kumpeleka kwa mkopo, lakini alifanikiwa kumvutia Wenger katika mazoezi na kumfanya abadili mawazo na kumbakisha kikosini.

Tayari ameshaichezea Arsenal katika michezo mitatu ya ligi kuu ya Uingeleza,Alicheza vizuri tulipofungwa na Manchester United,pia alicheza vizuri tulipowafunga Burnley goli 5-0 na alipewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Leicester.

Ni kijana mwenye nguvu na kipaji cha hali ya juu,ila sidhani kama yupo tayari kucheza katika kikosi cha kwanza,Kama Koscienly atapona mapema na ukichukulia ujio wa Sokratis,Uwepo wa Chambers na Mustafi anaweza kuwa chaguo la tano ama la sita (akishindana na Rob Holding).

Sinoni akipata nafasi katika kikosi cha kwanza ila naamini ataacheza sana kwenye Europa league na mmoja wapo kati ya Mustafi au Holding.

Na kama Koscienly atapona kabla ya kuanza mwaka mpya mmoja wapo kati yake na Holding ataenda kwa mkopo katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza.

Reiss Nelson

Na yeye ni kama  Mavropano, mashabiki wa Arsenal walikuwa na matumaini makubwa na nafikiri hajacheza kwa kiwango kikubwa kama mashabiki wengi wa Arsenal walivyotegemea.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anauwezo wa kucheza kama winga na kama kiungo mshambuliaji wa kati, nafasi ya kiungo mshambuliaji hawezi kuipata kwani pale kuna Mesut Özil, Aaron Ramsey na Mkhitaryan.

Nafasi ya winga mpaka sasa haieleweki nani atacheza, Kuna Iwobi,Mkhitaryan,Welbeck  na Lucas Perez,nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ni finyu.

Kama Mavropanos, nategemea atapata nafasi ya kucheza katika hatua ya makundi ya kombe la Europa League na kama atafanya vizuri kuliko Iwobi na Welbeck anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Iwapo atashindwa kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya Europa League anaweza akatolewa kwa mkopo kwenda kwenye timu ya daraja la kwanza mwezi wa kwanza mwakani.

Jeff Reine-Adelaide

Jeff alianza vizuri kuichezea Arsenal, lakini majeraha ya mara kwa mara yamemfanya ashindwe kuonesha kiwango chake, pamoja na kuwa na umri mkubwa kumzidi Nelson (Jeff ana miaka 20), kwa sasa Nelson ni bora kuliko Jeff, labda afanye vizuri sana kwenye mechi za kirafiki, sioni nafasi ya Jeff kwenye kikosi cha sasa.

Eddie Nketiah

Mchezaji huyo alijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya kufunga magoli mawili yaliyoisaidia Arsenal kushinda dhidi ya Norwich.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kwa sasa ni mshambuliaji wa nne katika timu ya Arsenal, akiwa nyuma ya Auba,Lacazzete na Danny Welbeck.

Welbeck anaingia katika mwaka wake wa mwisho, na kuna tetesi za kwamba anatakiwa na Everton,akiondoka Welbeck kuna mambo mawili yanaweza kutokea, moja Arsenal wanaweza kusajili mshambuliaji mwingine au mbili Unai Emery anaweza kubaki na Nketiah kama mshambuliaji wa akiba.

Ainsley Maitland-Niles

Huyu haendi kokote, mwaka jana alicheza michezo 28 na mwaka huu nategemea atacheza idadi kama hiyo ama zaidi, amepewa mkataba mpya na amebadilisha jezi na kupewa namba 15,ni dhahiri ya kwamba yupo kwenye mipango ya mwalimu.

 

Emile Smith Rowe

Akiwa na umri wa miaka 17 Emile Smith Rowe, huu unaweza ukawa ni mwaka ambao dogo huyu akaichezea timu ya wakubwa.

Alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichoifunga Boreham Wood na pia alicheza katika mchezo wa juzi wa kirafiki, na kuna taarifa ya kwamba atakuwemo kwenye kikosi kinachoelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kombe la kimataifa.

Smith Rowe alikuwa katika kikosi cha timu ya vijana wa Arsenal iliyofika fainali ya kombe la FA kwa timu za vijana, ambapo alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri kabisa katika michuano hiyo.

Wachunguzi wa manbo ya soka wanadai ya kwamba mchezaji huyo ni muunganiko wa Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamberlain kutokana na uwezo wake wa kupasua ukuta wa timu pinzani kwa kupiga pasi zenye macho na pia ana uwezo mkubwa wa kukimbia akiwa na mpira.

Sioni nafasi yake kwenye timu, ila naamini ya kwamba mkopo kwenda kwenye timu yenye ushindani hasa katika nusu ya kwanza ya msimu ujao.

Hao ndio wachezaji vijana wa Arsenal ambao wanaweza kufanya vizuri msimu ujao wakiwa na timu ya wakubwa, wengine nawaona wakibaki katika timu ya vijana, ama kutolewa kwa mkopo.

Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N’Zonzi na Golovin

Arsenal inaendelea na kujiandaa na msimu ujao wa ligi ambapo jana ilicheza na timu ya Crawley town na kuifunga goli 9-0,na wiki iliyopita kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery, alisema ya kwamba kikosi chake kimekamilika.

Lakini kutokana na kuwa katika kipindi cha usajili bado Arsenal inahisishwa na kusajili wachezaji wapya.Katika tetesi za usajili leo tunakuletea habari zilizoandikwa na magazeti kuhusu wachezaji Kingsley Coman ,N’Zonzi na Golovin ambao wamehusishwa na usajili wa Arsenal.

Kingsley Coman

Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N'Zonzi na Golovin

Kingsley Coman

Arsenal imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa mchezaji Kingsley Coman kutoka Bayern Munich na kulikuwa na tetesi ya kwamba Arsenal walituma ofa ya paundi milioni 50 ambayo ilikataliwa na wakarudi tena na ofa ya paundi milioni 55 ambayo ilikataliwa pia.

Sababu kubwa ya Bayern Munich kuzikataa ofa za Arsenal ni kuwa wanamuona mchezaji huyo kama sehemu kubwa ya safu yake ya ushambuliaji hasa ukichukulia wachezaji kama Frank Ribery umri umeshawatupa mkono na Kingsley Coman atachukua nafasi yake siku si nyingi.

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Kituo cha Sky Sports kimeandika katika tovuti yake ya kwamba Arsenal wanaendelea mazungumzo na Sevilla kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji Steven N’Zonzi. Mchezaji huyo ambaye amewahi kufanya kazi na Unai Emery anaweza kucheza kama kiungo mkabaji na anaweza kuja kuongeza nguvu katika kiungo cha Arsenal.

Aleksandr Golovin

Arsenal ilikuwa inamtaka Aleksandr Golovin, na Arsenal inaelekea kumkosa mchezaji huyo ambaye ameamua kujiunga na Chelsea.

Inasemekana ya kwamba mchezaji huyo alikuwa tayari kujiunga na Arsenal lakini baada ya Arsene Wenger kuondoka Arsenal ameamua kubadili uamuzi wake kwani alikuwa ni shabiki mkubwa wa kocha Wenger.

Hizo ndizo tetesi za usajili za Arsenal tulizozipata kwa siku ya leo,usisahau kushare na mashabiki wengine wa Arsenal.

Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0

Arsenal leo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Crawley town na kufanikiwa kuifunga timu hiyo kwa jumla ya goli 9-0.

Katika mchezo huyo uliofanyika ndani ya viwanja vya mazoezi vya Arsenal,London Colney.Ulifanyika kwa siri na hakuna mashabiki wala waandishi wa habari walioruhusiwa kuuona.

Habari za mchezo huo zilivuja baada ya wachezaji wa Arsenal kuweka picha katika mitandao ya kijamii, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Jeff Adelaide ambaye aliweka picha kwenye ukurasa wake akishangilia moja ya magoli hayo ambaye yeye alifunga.

Mchezaji mwingine ambaye alifunga katika mchezo huo alikuwa ni Henrik Mkhitaryan ambaye pia aliweka picha kwenye mitandao ya kijamii ikionesha  akishangilia goli.

Taarifa tulizopata ni kwamba kikosi kilichocheza ni kile kile kilichoifunga Boreham Wood goli 8-0, Pia katika mchezo huo golikipa mpya wa Arsenal Bernd Leno alidaka kwa mara ya kwanza.

Kwa sasa hatuna taarifa kamili ya wafungaji wala video ya mchezo huo, ila tumefanikiwa kupata baadhi ya picha za mchezo huo  ambazo tukakuwekea hapa chini.

Wafungaji
Timu ya kwanza (walicheza dakika 60)
Reine adelaide: 1
Perez: 2
Lacazette: 2
Mkhitaryan: 1
 
Timu ya pili (walicheza dakika 30)
Aubameyang:1
Nketiah:1
Nelson:1

 

Leno akidaka katika mchezo dhidi ya Crawley town

Leno akidaka katika mchezo dhidi ya Crawley town

 

Jeff akishangilia goli katika mchezo dhidi ya Crawley town

Jeff akishangilia goli katika mchezo dhidi ya Crawley town

Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0 Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0