Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa wa kijerumani  Bernd Leno amekubali kujiunga na Arsenal akitokea timu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa mpya wa Arsenal Bernd Leno

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea Bayer Leverkusen michezo zaidi ya 230 katika misimu saba aliyokuwa na timu hiyo ya kijerumani.

Alianza soka akiwa na timu ya  Stuttgart, Leno alijiunga na Leverkusen mwaka 2011 na mwaka huo huo mwezi wa tisa alikuwa aliweka rekodi ya kuwa golikipa mwenye umri mdogo zaidi kucheza katika ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa na umri wa miaka 19 na siku 193, wakati timu yake ya Leverkusen ilipocheza na Chelsea katika hatua ya makundi.

Katika mechi za kimataifa,Bernd aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na ameishaichezea timu hiyo katika michezo 6, mwaka jana alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la mabara.

Baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Tumefurahi ya kwamba Bernd Leno amejiunga nasi, amekuwa akicheza kwa kiwango kwa juu na kuwa kipa wa kwanza wa Leverkusen kwa muda mrefu katika ligi kuu ya Ujerumani katika miaka 7 iliyopita.Wote tuna furaha kubwa ya kwamba Bernd amechagua kujiunga na timu ya Arsenal, na tunategemea kuanza kufanya naye kazi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya ”.

Kipa huyo mpya bado hajapewa namba,ambayo itatangazwa muda mfupi ujao.

Karibu Arsenal Bernd Leno

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Lehman aondoka

*Steve Bould abaki

Arsenal imeendelea na wimbi la mabadiliko ambapo leo imetangaza benchi jipya la ufundi litakalomsaidia kocha mkuu Unai Emery.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

Benchi jipya la ufundi litakalokua chini ya Unay Emery(pichani) limetangazwa

Katika mabadiliko hayo Unai atakuwa na jopo la ufundi litakaloundwa na kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Juan Carlos Carcedo,kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Steve Bould; Kocha wa kikosi cha kwanza, Pablo Villanueva,Mkurugenzi wa mtendaji wa kikosi cha kwanza, Darren Burgess,Kocha wa mazoezi ya kujenga mwili na viungo Julen Masach;Kocha wa makipa, Javi Garcia; Kocha wa makipa, Sal Bibbo na mtunza kumbukumbu za video Victor Manas.

Katika orodha ya hapo juu kuna watu watatu ambao walikuwa kwenye timu ya Arsene Wenger ambao ni Steve Bould, Sal Bibbo na Darren Burgess.

Waliobaki wote wamekuja na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Lehman atimka

Wakati huo huo asilimia kubwa la jopo la ufundi lililokuwa chini ya Wenger wameondoka akiwemo mchezaji wa zamani wa Arsenal Jens Lehman.

Wengine waliiondoka ni makocha wa kikosi chakwanza,  Neil Banfield, Tony Colbert, Jens Lehmann, Gerry Peyton na Boro Primorac; Mkuu wa kitengo cha utabibu (daktari mkuu wa Arsenal) , Colin Lewin; Daktari wa saikolojia Andy Rolls na Ben Ashworth; Daktari wa mifupa Dr Philippe Boixel na mratibu wa safari za Arsenal, Paul Johnson .

Tunapenda kuikaribisha timu mpya na kuwatakia mafanikio mema katika zama mpya za Arsenal na pia tunapenda kusema asante kwa kuitumikia Arsenal na kwa heri kwa wale wote walioondoka.

Tetesi Arsenal kutangaza usajili wa Bernd Leno kesho

Kwa zaidi ya wiki sasa kumekuwa na tetesi za kwamba Arsenal inatafuta golikipa mpya na pia kuna tetesi ya kwamba tayari wameshakubaliana na Bernd Leno ili kuja kuichezea timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Tetesi Arsenal kutangaza usajili wa Bernd Leno kesho

Wiki iliyopita jarida la Bild liliandika ya kwamba Arsenal na Bayer Leverkusen walikuwa wameshafikia makubaliano juu ya uhamisho wa mchezaji huyo ambapo walikuwa wakihitaji kati ya paundi milioni 20 na 25 na Arsenal walikuwa tayari kulipa kiasi hicho cha pesa.

Baada ya kufanikiwa kumsajili Lukas Hradecky, timu hiyo inayoshiriki katika ligi kuu ya Ujerumani walisema ya kwamba kipa wao mpya ndiye atakayekuwa anaanza hali iliyosababisha Leno aanze kutafuta timu mpya.

Timu nyingi zilikuwa zilikuwa zinatafuta nafasi ya kumsajili mchezaji huyo zikiwemo Napoli na Atletico Madrid , lakini kwa sasa inaonekana ya kwamba Arsenal imeshinda vita hivyo.

Jioni hii mwandishi wa bild Christian Falk, anadai ya kwamba kila kitu kimekamilika na usajili huo utatangazwa kesho.

 

Tetesi za usajili-Napoli wanamtaka Petr Cech kwa mkopo

Timu ya Napoli inayoshiriki katika ligi kuu ya Italia imetuma maombi ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mlinda mlando mkongwe wa Arsenal Petr Cech kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mwandishi wa habari kutoka Italia Di Marzio ameandika katika tofuti yake ya kwamba waitaliano hao wana mpango wa kumsajili kipa huyo baada ya mipango yao ya kumsajili Bernd Leno kushindwa kuzaa matunda (Leno anakuja Arsenal).

Taarifa hiyo inahabarisha zaidi ya kwamba, Napoli wana mpango wa kumsajili kipa kutoka PSG  Alphonse Areola, lakini mabingwa hao wa Ufaransa hawataki kumuuza kipa huyo kitu ambacho kimewafanya wakali hao kutoka Italia waanze kuangalia uwezekano wa kumpata Cech.

Habari hizo za kutakiwa kwa Cech kwa mkopo ni za kushangaza kidogo kwa sababu kubwa mbili. Moja ni kwamba Petr Cech amebadili kutoka jezi namba 33 na kupewa jezi namba moja, mchezaji anayetaka kuondoka huwa habadili namba, sababu ya pili ni kwamba Petr Cech mwenye umri wa miaka 36 anaingia katika mwaka wake wa mwisho, akienda kwa mkopo ina maana wakati mkopo wake unaisha tayari atakuwa mchezaji huru, kitu ambacho naamini kwa Arsenal itakuwa bora kumuuza kuliko kumtoa kwa mkopo.

Mara nyingi Arsenal inatuma wachezaji wake vijana kwa mikopo katika mwaka wao wa mwisho ili kuwapa nafasi ya kucheza na wakati huo huo kutafuta timu kama walivyofanya kwa  Marc Bola na Tafari Moore kabla ya kuwaacha katika usajili wa msimu ujao.

Inawezekana ikawa timu inataka kufanya hivyo kwa Petr Cech ukichukulia ya kwamba hawatapesa pesa nyingi kwa kumuuza mchezaji huyo kutokana na umri wake kusogea mbele.

Ukweli unabaki pale pale iwapo Leno atatua kuna makipa wawili itabidi waondoke kati ya Cech, Ospina na Martinez.

Rasmi Granit Xhaka asaini mkataba mpya

Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka amesajili mkataba mpya ambao utamfanya aendelee kuichezea Arsenal kwa miaka mitano ijayo.

Rasmi Granit Xhaka asaini mkataba mpya

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa ni mchezaji pekee wa Arsenal kucheza michezo yote 38 ya Arsenal msimu uliopita ambapo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwa kupiga pasi nyingi ndani ya msimu mmoja katika ligi ya Uingeleza baada ya kupiga pasi 3,116 msimu wa 2017-2018.

Ameishaichezea Arsenal katika michezo 94 na alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichoshinda kombe la FA mwaka jana.

Pia mchezaji huyo ameishaichezea timu yake ya taifa ya Switzerland katika michezo 61 na kwa sasa yupo na timu hiyo wakishiriki katika kombe la dunia nchini Urusi.

Mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huyo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema ya kwamba ana furaha kubwa ya kwamba Granit Xhaka ameongeza mkataba wake wa kuichezea Arsenal kwa sababu ni mmoja ya wachezaji muhimu wa timu na pia bado ni kijana mdogo hivyo kuna nafasi ya kuimalika zaidi katika siku za usoni.

Granit Xhaka atavaa jezi namba 34 msimu ujao namba ambayo iliachwa wazi na Coquelin aliyehamia Valencia katika majira ya usajili ya msimu wa baridi.

Je unaonaje habari hizi za Xhaka kusaini mkataba mpya ? tupia maoni yako hapa chini.

 

Tetesi za usajili Arsenal-Ospina-Torreira-Gotze-David Luiz

Wakati kombe la Dunia limeshaanza na jana wenyeji Urusi kuwafunga Saudi Arabia kwa goli 5-0, bado kuwekuwa na tetesi nyingi zikiwahusihwa wachezaji wanaotaka kuhama ama kuhamia Arsenal.

Katika tetesi za usajili leo tunakuletea taarifa zilizoandikwa na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu David Ospina, Lucas Torreira, Mario Gotze na David Luiz.

Mario Gotze

Inasemekana ya kwamba Mario Gotze anataka kuhamia katika ligi kuu ya Uingeleza na Arsenal ni moja ya timu zinazofuatilia muenendo wake na kuangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.

Gotze, ambaye ndiye aliyefunga goli lililowapa lililowafanya Wajerumani wawe mabingwa wa Dunia miaka minne iliyopita amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara hali iliyomfanya asiwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kinachotetea ubingwa wake nchini Urusi.

Gazeti la The Mirror  linahabarisha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaa mpango wa kuhamia katika ligi kuu ya Uingeleza na timu za Arsenal,Everton,West Ham ,Leicester na Newcastle zinataka kumsajili mchezji huyo.

Lucas Torreira

Arsenal wameshakamilisha usajili wa kiungo kutoka Uruguay, Lucas Torreira, Katika taarifa iliyoandikwa na vyombo vingi vya habari na kuzibitishwa na watu wengi tunaowaamini ni kwamba mchezaji huyo ni mali ya Arsenal na anaweza kutangazwa siku yeyote kuanzia sasa.

David Luiz

Tetesi za usajili Arsenal-Ospina-Torreira-Gotze-David Luiz

Le10Sport  wameandika ya kwamba Arsenal wamepeleka ombi la kumsajili beki wa kati wa Chelsea kwa dau la paundi milioni 20, dau ambalo lilikataliwa na Chelsea.

Luiz ambaye amekuwa hapati namba katika timu ya Chelsea , inasemekana ana mpango wa kuondoka katika timu hiyo na pia kuna tetesi nyingine za kwamba Arsenal watatuma ombi jingine la kumsajili mchezaji huyo na kuboresha kiasi cha pesa ambacho watatoa.

David Ospina

Tetesi-Tigres na Fenerbahçe wamuwania David Ospina

Arsenal wanaweza kumuuza David Ospina ili kupata pesa ya kumsajili golikipa kutoka  Bayer Leverkusen, Bernd Leno.

Leno yupo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Arsenal na inasemekana ya kwamba Arsenal wanaweza kumpata kwa dau la paundi milioni 22.

Ili kupata pesa ya kumnunua kipa huyo, Arsenal wana mpango wa kumuuza Ospina na gazeti la

And in order to pay for the Germany shot-stopper, reserve goalkeeper Ospina could be heading out of the exit door.

The Daily Mail  linahabarisha ya kwamba mchezaji huyo kutoka Colombia anaweza kuuzwa kwenda timu ya Tigres ya Mexico.

Hizo ni tetesi za usajili wa Arsenal kwa siku ya leo, zingine kesho Mungu akipenda,Usisahau kushara na wengine pia ili waweze kusoma hizi tetesi.

 

Arsenal yaingia mkataba na Tidal

Arsenal imepata mdhamini mpya baada ya kuingia mkataba na kampuni ya musiki Tidal.

Arsenal walitangaza jumatatu ya kwamba wameingia mtakaba na kampuni hiyo ambao inajihusisha na kusambaza mziki kwenye internet.

Huu ni mkataba wa pili ndani wa wiki chache zilizopita baada ya Arsenal kuingia mkataba na Visit Rwanda’ ambaowaliingiamkatabawenyedhamani ya dolamilioni 30 mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kwenye tovuti rasmi ya Arsenal hawajaelezea ni kiasi gani watapata katika mkataba huo, lakini mtandao wa Goal unadai ya kwamba katika mkataba huo Arsenal watakuwa wanalipwa paundi milioni 1 kwa mwaka.

Mkataba huo hauleti pesa nyingi lakini naamini utachangia katika mapato ya Arsenal, kwani timu kwa sasa inaonesha ya kwamba inafanya vizuri kiuchumi kwa kupata mikataba minono na ya pesa ndefu zaidi.

Arsenal ambayo haitashiriki katika michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya kwa msimu wa pili sasa inahitaji pesa kutoka kwa wadhamini ili iweke kufidia pesa ambazo imezikosa.

Pia sisi kama mashabiki wa Arsenal tunategemea ya kwamba pesa zitakazopatikana katika mikataba kama hii zitatumika katika kuiboresha timu kwa kufanya usajili wa maana.

Kama unataka kusikiliza nyimbo zilizochaguliwa na wachezaji wa Arsenal,Danny Welbeck, Hector Bellerin na  Reiss Nelson. Bofya hapa http://tidal.com/arsenal

 

 

Tetesi-Tigres na Fenerbahçe wamuwania David Ospina

Timu ya Tigres itajaribu kumsajili golikipa wa Arsenal David Ospina ikiwa golikipa wao  Nahuel Guzman ataihama timu hiyo na kutimkia   Boca Juniors  ya Argentina.

Tetesi-Tigres na Fenerbahçe wamuwania David Ospina

Tigres ambayo inashiliki ligi kuu ya Mexico, wamehusishwa na uhamisho wa Ospina baada ya Nahuel Guzman kufanya kosa la kizembe na kusababisha timu hiyo kufungwa na mahasimu wao Santos katika robo fainali ya Liguilla (nane bora ya ligi kuu ya Mexico) msimu huu.Tigres wapo tayari kumwachia kipa huyo kwa dau la dola milioni 10.

Na kutokana na vyanzo vyingi vya habari hapa Mexico wakiwemi Univision. Kocha mkuu wa Tigres Tuca anataka David Ospina  kiziba pengo hilo.

Ospina alihamia Arsenal mwanzoni mwa msimu wa 2014. Wenger alimfanya kuwa kipa chaguo la kwanza, lakini baadaye alipoteza nafasi hiyo baada ya kusajiliwa kwa Petr Cech kutoka Chelsea.

Ospina ameanza katika michezo 11 tu ya ligi kuu ya Uingeleza katika misimu mitatu iliyopita ingawa alicheza katika michezo 10 kwenye Europa League msimu iliopita.

Wakati Tigres wakijiandaa kuongea na wawakilishi wa Ospina, mtandao mwingine Multimedios unahabarisha ya kwamba tiku kutoka Uturuki Fenerbahçe nao wapo tayari kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Kwa sasa Ospina yupo nchini Russia akishiriki michuano ya kombe la Dunia akiiwakilisha nchi yake ya Colombia.

 

Ainsley Maitland-Niles asaini mkataba mpya, Apewa jezi namba 15

Ainsley Maitland-Niles amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na Arsenal,katika taarifa ramsi iliyotolewa na tofuti rasmi ya Arsenal, mchezaji huyo amekubali kuendelea kuitumikia timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Ainsley Maitland-Niles asaini mkataba mpya, Apewa jezi namba 15

Akiwa amejiunga na chuo cha soka cha Arsenal tangu akiwa na miaka 9, mchezaji huyo alikuwa na msimu wa mafanikio makubwa msimu uliopita ambapo alifanikuwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.Alifinikiwa kucheza katika michezo 28 katika msimu wa  2017/18 akicheza kama beki mshambuliaji, beki wa kulia na kiungo.

Mwezi wa 12 mwaka 2014, akiwa na miaka 17 na siku 102,Ainsley Maitland-Niles alifanikiwa kuwa mchezaji mdogo wa pili kuichezea Arsenal katika ligi ya mabingwa wa Ulaya, Baada ya kufanikiwa kuichezea Arsenal kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Aliichezea Arsenal katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingeleza dhidi ya Newcastle siku nne baadaye.

Ikiwa ni sehemu ya maendeleo yake mchezaji huyo alicheza kwa mkopo katika timu ya Ipswich Town katika msimu wa 2015/16, ambapo alicheza michezo 30, akifunga magoli mawili na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi katika mwezi wake wa kwanza katika timu hiyo.

Akiwa na timu ya watoto ya Uingelea Ainsley, alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ambapo alikuwa ni mmoja ya wachezaji muhimu wakati madogo hao walipochukua kombe la dunia mwezi wa 6 mwaka jana.

wakati huo huo mchezaji huyo amebadilisha namba ya jezi ambapo kwa sasa atakuwa anavaa jezi namba 15.

Ainsley Maitland-Niles asaini mkataba mpya, Apewa jezi namba 15

 

Arsenal yaachana na wachezaji 9

Timu ya Arsenal imetangaza kuachana na wachezaji 9 ambao hawatakuwa katika kikosi cha msimu ujao, Ijumaa iliyopita Arsenal ilipeleka orodha ya wachezaji ambao ina mpango wa kubaki nao na pia ambao inawaacha.

Pia kuna wachezaji ambao wamepewa mikataba ambapo bado hawajasaini, kwa mfano Jack Wilshere ambaye mkataba wake umefika ukingoni na tayari ameshapewa mkataba mpya lakini bado hajausaini kwani anataka kuhakikishiwa namba kabla ya kukubali.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji ambao wataachwa na Arsenal kwa ajili ya msimu ujao:

  • Marc Bola
  • Santi Cazorla
  • Alexander Crean
  • Aaron Eyoma
  • Ryan Huddart
  • Chiori Johnson
  • Hugo Keto
  • Per Mertesacker
  • Tafari Moore

Per Mertesacker,ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal anachukua nafasi ya ukocha katika chuo cha soka cha Arsenal, na hataendelea kucheza lakini bado atabakiwa kwenye timu.

Santi Cazorla yeye ameamua kurudi Hispania ambapo tayari ameshaanza kufanya mazoezi na timu ya Villarreal katika maandalizi ya msumu ujao.

Katika orodha hiyo majina mawili ambayo hayakutegemewa ni Marc Bola na Tafari Moore.Wachezaji hao wawili walifanya vizuri katika timu zao walipoenda kwa mkopo, lakini inaonesha ya kwamba jopo la ufundi la Arsenal limeona ya kwamba ni bora liwaachie wakatafute nafasi kwingine.

Wote wawili wana miaka 20 na ingekuwa ni vigumu kwao kupata nafasi katika kikosi cha kwanza na kwa umri huu ni bora wakapate kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.

 

Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Joel Lopez kutoka Barcelona

Mwandishi wa kiispania ,Gerard Romero amehabarisha ya kwamba Arsenal imekamilisha usajili wa kinda kutoka Barcelona Joel Lopez.

Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Joel Lopez kutoka Barcelona

Joel Lopez , mwenye umri wa miaka 16 ni beki wa kushoto na amekuwa akiichezea Barcelona tangu akiwa na miaka 7 na kwa siku za hivi karibuni amekuwa akisemwa ya kwamba ni mmoja ya vipaji bora kabisha vilivyopo katika chuo cha soka cha wakali hao kutoka Hispania, La Masia.

Pamoja ya kwamba viongozi wengi wa Barcelona wanamuona ni mmoja ya wachezaji wenye kipaji kikubwa kutoka La Masia, timu hiyo imeshindwa kumshawishi mchezaji huyo kusaini mkataba mpya.

Anaelekea Arsenal

Kutoka katika taarifa iliyotolewa na mwandishi Gerard Romero, inaonekana kitendo cha kushindwa kumshawishi kinda huyo kusaini mkataba mpya kinaweza kusababisha kumpoteza mchezaji huyo,kwani kuna taarifa kutoka mcheza wa leo ya kwamba leo asubuhi mchezaji huyo ameshawataarifu viongozi wa Barcelona ya kwamba ameshakubariana na Arsenal na atajiunga na timu hiyo katika majira haya ya Usajili.

Arsenal wamekuwa wakimfuatilia kinda huyo kwa muda mrefu na pia Liverpool walionesha nia ya kumtaka kinda huyo ila uwepo wa Raul Sanllehi katika timu ya Arsenal inasemekana ndiyo sababu ya dogo huyo kuichagua timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Iwapo Lopez atajiunga na Arsenal atakuwa amefuata nyota za wakali wengine kutoka La Masia waliofanya hivyo kama Cesc Fabregas, Hector Bellerin na Fran Merida.