Tetesi za usajili-Arsenal wanamfukuzia Lucas Vazquez

Arsenal ina mpango wa kumlipa  Lucas Vazquez mshahara ambao ni mara mbili zaidi na anaolipwa na Real Madrid ili kumshawishi kuhamia kaskazini mwa London.

Tetesi za usajili-Arsenal wanamfukuzia Lucas Vazquez

Katika taarifa itulizozipata kutoka nchini Uhispania ni kwamba na mwandishi wa OkDiario Eduardo Inda, akizungumza na kituo cha kuninga cha El Chiringuito TV, alisema ya kwamba Vazquez ana ofa nzuri kutoka Arsenal na Unai Emery.Pia alielezea ya kwamba Arsenal wanampango wa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa Euro milioni 8 baada ya kodi, inakadiliwa ya kwamba mchezaji huyo analipwa kati ya Euro milioni 3 na 4 kwa mwaka na timu ya Real Madrid.

Taarifa hiyo inaendelea kueleza ya kwamba Emery ameweka wazi nia yake ya kumsajili mchezaji huyo kwani anaamini Vazquez, mwenye umri wa miaka 26 ana uwezo wa kuifanya Arsenal iwe timu ya ushindani katika ligi kuu ya Uingeleza na yupo tayari kumpa kutoa pesa nzuri kwa Real Madrid ili kukamilisha usajili huu.

Pamoja na taarifa hizo kuna taarifa nyingine za kwamba mchezji huyo yupo kwenye orodha ya wachezaji wasiouzwa wa Real Madrid, kwani mchezaji huyo bado ana mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2021 na timu hiyo haipo tayari kumpoteza.

Mchezaji huyo alikuwa na msimu mzuri mwaka uliopita akiwa na timu hiyo kwani alifunga magoli nane na kusaidia kupatikana kwa mengine 16 katika michezo 53 katika msimu wa mwaka 2017/18. Huu ni mchango mkubwa kwani alikuwa mara kwa mara akitokea katika benchi la wachezaji wa akiba.

Inawezekana ya kwamba Emery akamshawishi winga huyo ya kwamba atapata nafasi zaidi ya kucheza akiwa na timu ya Arsenal na pia mshahara mkubwa unaweza kubadili mawazo ya mchezaji huyo na kunfanya alazimishe kuhama.

 

Wachezaji wa Arsenal katika kombe la dunia

Wakati kombe la dunia likiendelea nchini Urusi, leo nimeamua kukuletea ninavyoona mimi kuhusu ushiriki wa wachezaji wa Arsenal katika kombe la dunia.

Wachezaji wa Arsenal katika kombe la dunia

Arsenal ina jumla ya wachezaji 9 wanaoziwakilisha nchi zao katika fainali hizi za kombe la dunia na nikiwa mkweli wengi wao hawajafanya vizuri sana.

Kati ya wachezaji hao tisa, watano tu ndio walioanza katika raundi ya kwanza na wanne wameanza katika raundi ya pili.

Mchezaji wa kwanza wa Arsenal kufanya vizuri katika fainali za mwaka huu alikuwa ni Granit Xhaka, baada ya kufunga bonge la goli la kusawazisha wakati Switzerland ilipocheza dhidi ya Serbia.Baadaye Switzerland walishinda mchezo huo kufuatia goli la pili lililofungwa na Xherdan Shaqiri.

Pia katika mchezo huo Xhaka aliingia katika matatizo na fifa wakati akishangilia hilo goli, amepigwa faini ya dola elfu 10 kwa kosa la kuchanganya siasa na soka.

Katika kikosi hicho pia kuna mchezaji mpya wa Arsenal,Lichsteiner ambaye alicheza vizuri katika mechi zote mbili na alinifurahisha sana katika mechi ya kwanza kwani aliweza kumzuia kwa ufanisi mkubwa mchezaji kutoka Brazil,Neymar.

David Ospina  aliisaidia timu yake ya Colombia kushinda kwa goli 3-0, katika mchezo wa kwanza timu yake ilifungwa huku Ospina akicheza vibaya lakini katika mchezo wa juzi alibadilika baada ya kufanya kazi ya ziada kuzuia ya wachezaji wa Poland.

Pia katika mchezo huo aliumia huku nafasi za kufanya mabadiliko zikiwa zimeisha na bado alifanikiwa kuokoa mpira wa shuti kali uliopingwa na Lewandoski katika dakika za mwisho za mchezo huo.

Mohamed Elneny yeye amecheza michezo yote mitatu akiwa na timu yake ya taifa ya Misri lakini kwa bahati mbaya walifungwa katika michezo yote huku Elneny akishindwa kung’ara.

Nacho Monreal yeye bado hajacheza hata dakika moja moja katika michuano hiyo ya kombe la dunia, hali ambayo pia imemkuta Dany Welbeck ambaye hakugusa mpira wakati Uingeleza wakiifumua Panamá goli 6-1.

Mesut Özil ambaye alianza wakati Ujerumani walipofungwa na Mexico, hakucheza katika mchezo wa pili walipoishinda timu ya Sweden goli 2-1.

Alex Iwobi akiiwakilisha Nigeria aliingia dakika za mwisho wakati tai hao wa kijani walipoifunga timu ya Iceland kwa jumla ya magoli 2-0.Iwobi alianza katika mchezo wa kwanza ambapo walifungwa goli 2-0 dhidi ya Croatia.

Joel Campbell hakucheza wakati timu yake ya taifa ya Costa Rica ilipofungwa katika muda wa nyongeza na Brazil,Joel Campbell aliingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa kwanza ambapo hakuna la maana alilolifanya.

Huo ndio mchango wa wachezaji wa Arsenal mpaka sasa katika kombe la dunia, Je kwako wewe ni mchezaji gani wa Arsenal aliyefanya vizuri mpaka sasa? tupia maoni yako hapa chini.

 

 

Tetesi-Arsenal na Lazio zamgombea Gelson Martins

Arsenal na Lazio zimeingia katika vita kali ya kumuwania mchezaji Gelson Martins,mchezaji huyo ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kuvunja mkataba wake na Sporting FC inasemekana amewekewa mezani mkataba wa miaka mitano na timu zote mbili.

Tetesi-Arsenal na Lazio zamgombea Gelson Martins

Gazeti la kiitaliano la Corriere dello Sport, limeandika ya kwamba Martins amepokea ofa yenye dhamani ya euro milioni 2.5 kwa mwaka baada ya makato ya kodi  kama mshahara kutoka katika timu hizo mbili.

Matarajio ni kwamba winga huyo mwenye kasi atajiunga bure na moja ya timu hizo, baada ya kuomba kuvunja mkataba wake na timu yake ya zamani ya Sporting FC , ingawa timu ambayo itafanikiwa kumsajili italazimika imlipe mchezaji huyo pesa kwa ajili ya kusaini mkataba.

Kabla ya kuvunjwa kwa mkataba huo kulikuwa na tetesi ya kwamba Arsenal walikuwa wanamtaka mchezaji huyo kiasi cha kwamba walituma ombi la kumsajli mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 30, dau ambalo lilikataliwa.

Baada ya viongozi wa Sporting FC kukataa dau hilo la Arsenal, inasemekana ya kwamba Martins alichukizwa na kitendo hicho na hivyo kuanza mchakato wa kuvunja mkataba na timu hiyo ya Ureno.Kisheria mchezaji huyo bado sio huru kwani kesi yake bado ipo mahakamani.

Akitoa mchango wa magoli 26 kamika michezo 52 akicheza kama winga msimu uliopita, Martins utakuwa ni usajili mzuri kwa Arsenal iwapo utakamilika.

Baada ya kuondoka kwa Alexis, Chambo na Walcott, Arsenal inahitaji wienge mwenye uwezo wa kukimbia na kukokota mpira, ni jambo la kusubiri kama wataweza kufanikisha usajili wake katika dirisha hili la usajili.

 

Tetesi za usajili Arsenal-Kostas Manolas-Ever Banega-Mateo Kovačić

Kocha wa Arsenal, Unai Emery ana kazi kubwa ya kukijenga upya kikosi hicho na kila siku Arsenal imekuwa ikihusishwa na wachezaji wapya kila siku.

Leo katika tetesi za usajili zinazoihusu Arsenal, tunakuletea taarifa kuhusu Kostas Manolas,Ever Banega na Mateo Kovačić.

Tetesi za usajilia Arsenal-Kostas Manolas-Ever Banega-Mateo Kovačić

Arsenal na Chelsea wanamtaka Kostas Manolas

Kostas Manolas

Gazete la The Mirror linaandaka ya kwamba Arsenal na Chelsea zimeingia katika vita vya kumuwania beki huyo wa kati ingawa Chelsea ndiyo wenye nafasi kubwa ya kumchukua mchezaji huyo.

Inasemekana ya kwamba Unay Emery anamtaka beki huyo aje achukue nafasi ya Laurent Koscienly ambaye hawezi kucheza hadi mwisho wa mwaka lakini kikwazo kikubwa ni kwamba Maurizio Sarri ambaye anatazamiwa kuwa kocha wa Chelsea pia anamtaka beki huyo na Kostas Manolas angependa kucheza chini ya Sarri.

 Ever Banega

Inasemekana ya kwamba Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji Ever Banega, gazeti la Daily Star  linaelezea ya kwamba tayari uongozi wa Arsenal umeshakutana na wawakilishi wa mchezaji huyo na kuna uwezekano wa kufikia makubariano.

Benega ameshawahi kufanya kazi na Emery katika timu za Valencia na Sevilla, inawezekana wanataka waungane kwa mara ya tatu.

Mimi binafsi siamini kama usajili huu utakuwa na manufaa kwa Arsenal,kwani Banega ni mchezaji wa kawaida sana.

Mateo Kovačić

Mchezaji wa Real Madrid,Mateo Kovačić, ametangaza nia yake ya kuihama timu hiyo kwa kile anachodai ya kwamba anataka kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Mara baada ya taarifa hizo kutoka kila gazeti limemuhusisha na kuhamia Arsenal,Mateo Kovačić ni mchezaji mzuri na naamini ya kwamba atasaidia kuiimalisha timu ingawa kuna taarifa ya kwamba anapatikana kwa paundi milioni 50 kitu ambacho naamini Arsenal hawataweza kulipa.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizokuletea katika siku ya leo, nyingine kesho Mungu alipenda, usisahau kushare na wengine.

Mesut Özil kuomba jezi namba 10 Arsenal

Kiungo wa Arsenal,Mesut Özil anatazamiwa kuwasilisha ombi rasmi la kuomba jezi namba 10 ili aweze kuitumia katika msimu ujao.

Mesut Özil kuomba jezi namba 10 Arsenal

Jezi namba 10 ilikuwa ikivaliwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal,Jack Wilshere ambaye ametangaza kuhama Arsenal siku chache zilizopita.Wilshere aliichukua namba hiyo baada ya Robin Van Persie kuhamia Machester United.

Özil aliwahi kuwasilisha ombi la kubadilishiwa namba mwaka juzi wakati Jack alipoenda bournemouth, lakini hakuweza kutimiza nia yake hiyo kwani ombi lake lilichelewa.

Sababu kubwa ya Mesut Özil kuitaka namba hiyo ni kwamba katika kampuni yake na matangazo ya kibiashara nembo yake ni M10, kitu ambacho hakiendani na namba anayovaa sasa ambayo ni 11.

Pia ikumbukwe ya kwamba Mesut alichukua namba 10 katika timu ya taifa ya Ujerumani baada ya Lukas Podolski kustaafu, na pia alivaa jezi namba 10 alipokuwa akiichezea Real Madrid ya Hispania.

 

 

Tetesi za usajili Arsenal-Miguel Layun-Soyuncu na Bernard

Wakati mataifa mbalimbali yakiendelea kuwania kombe la Dunia, Vilabu navyo vinaendelea na mikakati ya kujijenga na kujiandaa kwa msimu ujao.

Leo katika tetesi za usajili, Arsenal leo imehusishwa na usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Mexico Miguel Layun, Soyuncu kutoka Freinburg na Bernard kutoka Porto.

Calgar Soyuncu

Tetesi za usajili Arsenal-Miguel Layun-Soyuncu na Bernard

Soyuncu pichani juu yupo tayari kuhamia Arsenal

Gazeti la metro, linaandika ya kwamba Soyuncu amedhibitisha nia yake ya kuhamia Arsenal,gazeti hilo limemnukuu mchezaji huyo akisema ya kwamba Arsenal ni moja ya timu zinazomvutia na yupo tayari kuichezea ila kwa sasa ana mkataba wa miaka mitatu na Freiburg na itabidi kwanza timu hizo zikubaliane ndipo atakapoweza kuhama.

Miguel Layun

Gazeti la Express nalo linaandika ya kwamba Arsenal wana mpango wa kumsajili mchezaji kiraka kutoka Mexico Miguel Layun.Layun mwenye umri wa miaka 29 ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia, beki wa kushoto, kiungo mkabaji na winga zote mbili.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na Porto ya Ureno kwa sasa yupo nchini Urusi akishiriki katika kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Mexico.

Bernard

Gazeti la Daily Star lenyewe linaandika ya kwamba Arsenal ina mpango wa kumsajili winga nyota kutoka Brazil, Bernard.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa akiichezea Shakhtar Donetsk, amemaliza mkataba wake wa miaka mitano na timu hiyo ya Ukraine na sasa ni mchezaji huru, na sasa kuna tetesi za kwamba Arsenal wanataka kumsainisha kabla hajachukuliwa na timu zingine kubwa.

Pia kulikuwa na tetesi ya kwamba mchezaji huyo alikubaliana kila kitu na Arsenal Arsenal miaka mitano iliyopita, lakini mchezaji mwingine wa wa Brazil Hulk alimshauri aitose Arsenal na mpango huo ukafa.

Arsenal Bernard Shakhtar

Bernard anaweza kusajiliwa na Arsenal

Kwa leo hizo ndizo tetesi tulizopata na tukipata zingine tutaziweza hapa, usisahau kushare na wengine pia.

JACK WILSHERE –Kipaji cha hali ya juu kilichoshindwa kufikia kilele cha mafanikio

‘Hatacheza katika timu ya wachezaji kwa muda mrefu’. Hayo yalikuwa ni maneno ya Arsene Wenger,alipokuwa akimuongelea Jack Wilshere, bado akiwa ni mwanafunzi katika shule ya  soka ya Arsenal, baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo dhidi ya West Ham zaidi ya miaka 10 iliyopita.

JACK WILSHERE –Kipaji cha hali ya juu kilichoshindwa kufikia kilele cha mafanikio

Goli kali alilofunga Wilshere litabaki kuwa moja ya magoli bora yaliyowahi kufungwa na mchezaji wa timu za vijana za Arsenal, na kwa wakati huo ilikuwa ni wazi ya kwamba angekuja kuwa nyota mkubwa kwa miaka mingi ambaye ingefuatia.

Kijana huyo mdogo alikuwa ameiweka dunia mguuni pake na hakuna ambaye alikuwa na shaka ya kwamba kijana huyo kutoka Hale End angekuja kuwa mchezaji wa kiwango cha dunia.Bahati mbaya majeraha ya mara kwa mara yalisababisha kudumaa kwa kipaji cha Wilshere,ambaye juzi baada ya kuichezea Arsenal michezo 197,ametangaza ataondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu.

Kila shabiki wa soka anajua kwa nini Wilshere hakufikia katika kilele cha mafanikio kama wengi tulivyokuwa na matumaini, lakini hilo halituzuii kukumbuka ya kwamba alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu ambaye jina lake lilikuwa likiimbwa na mashabiki wengi wa Arsenal kila alipokuwa akigusa mpira.

Jack alianza maisha ya soka katika shule ya soka ya Luton Town,baadaye mwaka 2001 alijiunga na Arsenal ambapo alicheza katika timu za watoto.

Katika mwisho wa msimu wa mwaka 2006/07 Wilshere alipata nafasi ya kucheza katika timu ya watoto wenye chini ya umri wa miaka 18, na msimu uliofuatia alifanikiwa kuwa nyota wa timu hiyo ya watoto.Akiwa na uwezo wa kupiga pasi za haraka na uwezo mkubwa wa kukimbia huku akiwa na mpira,alikuwa akionekana ni bora hata kuliko wachezaji waliokuwa na umri mkubwa kumzidi.

Baada ya kung’ara katika timu hiyo ya watoto Wilshere alipandishwa katika kikosi cha wachezaji wa akiba na mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Reading ambapo alifunga katika mchezo huo na baadaye kucheza kwa kiwango cha hali ya juu katika mchezo uliofuata dhidi ya West Ham.

Mchezo mwingine ambao Jack Wilshere alicheza kwa kiwango cha hali ya juu ulikuwa dhidi ya Derby Country baada ya kupiga pasi ya maana na kumtengenezea goli mchezaji mwenzake  Rhys Murphy.

Aliendelea kucheza vizuri katika timu za vijana na akiba, Wilshere alikuwa ni mmoja ya wachezaji walioshinda kombe la FA kwa timu za vijana mwaka 2009( akiwa na Frimpong na Francis Coquelin), kipindi hicho tayari alikuwa ameshaanza kuichezea timu ya wakubwa.

Baadaye Wilshere alifanikiwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na alicheza kwa mafanikio makubwa, tukio la kukumbukwa ni pale alipoweza kuwafunika Xavi na Iniesta mwaka akiwa na miaka 19 tu.Pia aliweza kufunga moja ya magoli bora kabisa niliyowahi kushuudia baada ya kumalizia gonga 22 za wachezaji wa Arsenal na kisha kuwafunga Norwich.

Anaondoka Arsenal akiwa ameshinda makombe mawili ya FA na timu ya wakubwa.

Ni jambo la kusikitisha ya kwama Jack Wilshere hataweza kucheza hadi anastaafu akiwa katika timu ya Arsenal, lakini naamini bado ana uwezo wa kwenda sehemu nyingine na kwenda kufufua makali yake.

Bila kujali kama anaichezea timu ya watoto , ya wachezaji wa akiba ama kikosi cha kwanza,Wilshere mara zote alikuwa akiichezea Arsenal kwa mapenzi makubwa, hali hiyo ilimfanya kupendwa na mashabiki wengi wa Arsenal.

Mimi binafsi naona kuondoka kwake ni kitu sahihi kufanya ili kujaribu kuokoa kipaji chake kwani kwa sasa anahitaji kucheza mara kwa mara kitu ambacho asingeweza kufanya akiwa na Arsenal.

Ni matumaini yangu ya kwamba muda si mrefu atarudi kwenye kiwango chake na tutamuona tena akiwa na timu ya taifa ya Uingeleza.

Asante na kwa heri Jack Wilshere.

Hapa chini nimekuwekea goli la Wilshere alilowafunga West Ham.

 

Jack Wilshere atangaza kuondoka Arsenal

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, ametangaza rasmi kuondoka kwenye timu hiyo mara tu mkataba wake utakapofikia ukingoni mwishoni mwa mwezi huu.

Jack Wilshere atangaza kuondoka Arsenal

Jack Wilshere atangaza kuondoka Arsenal

Mchezaji juyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na kikosi cha Arsenal kwa miaka 17 na kuna kipindi alichukulia kuwa ni mmoja ya wachezaji wenye vipaji bora kabisa duniani, lakini majeraha ya mara kwa mara yamemfanya ashindwe kufikia matarajio ya wengi.

Katika walaka wake aliouandika kwenye mtandao wa instagram, mchezaji huyo alitangaza uamuzi huo huku akiweka wazi ya kwamba ameamua kufanya hivyo baada ya kukutana na kocha mkuu wa Arsenal , Unay Emery ambaye alishindwa kumhakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Jack Wilshere aliendelea kuandika ya kwamba alikubali kusaini mkataba wa malipo kidogo kuliko aliyoyokuwa anapata awali lakini kitendo cha kushindwa kuhakikishiwa namba kilimfanya afikirie upya na kuamua kwenda sehemu ambayo atapewa nafasi ya kucheza soka.

Pia alichukua nafasi hiyo kuwashukuru wachezaji, kocha Arsene Wenger na mashabiki waliomuunga mkono na kumpa nafasi katika kipindi chote hicho alichokuwa na timu ya Arsenal.

Taarifa hizo zimepokelewa na mitazamo tofauti na mashabiki wengi wa Arsenal, kuna baadhi wanaunga mkono uamuzi wa kocha kutokumhakikishia namba huku wengine wakisema ya kwamba kocha alitakiwa ampe nafasi.

Kuondoka kwa Wilshere kutaiacha jezi namba 10 wazi hali itakayompa nafasi Mesut Özil kuichukua, kwani kwa kipindi kirefu amekuwa akidai ya kwamba anaitaka.

Hapa chini nimekuwekea walaka huo unaweza kuusoma.

Jack Wilshere

zaidi unaweza kuusoma katika ukurasa wake wa instagram. https://www.instagram.com/p/BkOCXr9B43r/?taken-by=jackwilshere

kila la heri Jack Wilshere

Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa wa kijerumani  Bernd Leno amekubali kujiunga na Arsenal akitokea timu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa mpya wa Arsenal Bernd Leno

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea Bayer Leverkusen michezo zaidi ya 230 katika misimu saba aliyokuwa na timu hiyo ya kijerumani.

Alianza soka akiwa na timu ya  Stuttgart, Leno alijiunga na Leverkusen mwaka 2011 na mwaka huo huo mwezi wa tisa alikuwa aliweka rekodi ya kuwa golikipa mwenye umri mdogo zaidi kucheza katika ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa na umri wa miaka 19 na siku 193, wakati timu yake ya Leverkusen ilipocheza na Chelsea katika hatua ya makundi.

Katika mechi za kimataifa,Bernd aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na ameishaichezea timu hiyo katika michezo 6, mwaka jana alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la mabara.

Baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Tumefurahi ya kwamba Bernd Leno amejiunga nasi, amekuwa akicheza kwa kiwango kwa juu na kuwa kipa wa kwanza wa Leverkusen kwa muda mrefu katika ligi kuu ya Ujerumani katika miaka 7 iliyopita.Wote tuna furaha kubwa ya kwamba Bernd amechagua kujiunga na timu ya Arsenal, na tunategemea kuanza kufanya naye kazi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya ”.

Kipa huyo mpya bado hajapewa namba,ambayo itatangazwa muda mfupi ujao.

Karibu Arsenal Bernd Leno

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Lehman aondoka

*Steve Bould abaki

Arsenal imeendelea na wimbi la mabadiliko ambapo leo imetangaza benchi jipya la ufundi litakalomsaidia kocha mkuu Unai Emery.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

Benchi jipya la ufundi litakalokua chini ya Unay Emery(pichani) limetangazwa

Katika mabadiliko hayo Unai atakuwa na jopo la ufundi litakaloundwa na kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Juan Carlos Carcedo,kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Steve Bould; Kocha wa kikosi cha kwanza, Pablo Villanueva,Mkurugenzi wa mtendaji wa kikosi cha kwanza, Darren Burgess,Kocha wa mazoezi ya kujenga mwili na viungo Julen Masach;Kocha wa makipa, Javi Garcia; Kocha wa makipa, Sal Bibbo na mtunza kumbukumbu za video Victor Manas.

Katika orodha ya hapo juu kuna watu watatu ambao walikuwa kwenye timu ya Arsene Wenger ambao ni Steve Bould, Sal Bibbo na Darren Burgess.

Waliobaki wote wamekuja na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Lehman atimka

Wakati huo huo asilimia kubwa la jopo la ufundi lililokuwa chini ya Wenger wameondoka akiwemo mchezaji wa zamani wa Arsenal Jens Lehman.

Wengine waliiondoka ni makocha wa kikosi chakwanza,  Neil Banfield, Tony Colbert, Jens Lehmann, Gerry Peyton na Boro Primorac; Mkuu wa kitengo cha utabibu (daktari mkuu wa Arsenal) , Colin Lewin; Daktari wa saikolojia Andy Rolls na Ben Ashworth; Daktari wa mifupa Dr Philippe Boixel na mratibu wa safari za Arsenal, Paul Johnson .

Tunapenda kuikaribisha timu mpya na kuwatakia mafanikio mema katika zama mpya za Arsenal na pia tunapenda kusema asante kwa kuitumikia Arsenal na kwa heri kwa wale wote walioondoka.

Tetesi Arsenal kutangaza usajili wa Bernd Leno kesho

Kwa zaidi ya wiki sasa kumekuwa na tetesi za kwamba Arsenal inatafuta golikipa mpya na pia kuna tetesi ya kwamba tayari wameshakubaliana na Bernd Leno ili kuja kuichezea timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Tetesi Arsenal kutangaza usajili wa Bernd Leno kesho

Wiki iliyopita jarida la Bild liliandika ya kwamba Arsenal na Bayer Leverkusen walikuwa wameshafikia makubaliano juu ya uhamisho wa mchezaji huyo ambapo walikuwa wakihitaji kati ya paundi milioni 20 na 25 na Arsenal walikuwa tayari kulipa kiasi hicho cha pesa.

Baada ya kufanikiwa kumsajili Lukas Hradecky, timu hiyo inayoshiriki katika ligi kuu ya Ujerumani walisema ya kwamba kipa wao mpya ndiye atakayekuwa anaanza hali iliyosababisha Leno aanze kutafuta timu mpya.

Timu nyingi zilikuwa zilikuwa zinatafuta nafasi ya kumsajili mchezaji huyo zikiwemo Napoli na Atletico Madrid , lakini kwa sasa inaonekana ya kwamba Arsenal imeshinda vita hivyo.

Jioni hii mwandishi wa bild Christian Falk, anadai ya kwamba kila kitu kimekamilika na usajili huo utatangazwa kesho.