Golikipa wa Arsenal, Bernd Leno ameitwa na timu ya taifa ya Ujerumani ili kuichezea katika kombe la UEFA Nations League.
Timu ya Taifa ya Ujerumani itacheza na timu za taifa za Ufaransa na Uholanzi katika michuano hiyo.
Leno ameitwa kuchukua nafasi ya Kevin Trapp, ambaye atakosa michezo yote miwili kutokana na kuwa na maumivi ya misuli.
Leno ameishaichezea Arsenal katika michezo mitano tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Bayer Leverkusen katika dirisha lililopita la usajili.
Kwa sasa mchezaji huyo anacheza mechi zote za Arsenal baada ya kuumia kwa kipa namba moja wa Arsenal Petr Cech ambaye anatazamiwa kurudi ndani ya wiki mbili zijazo.
Kuitwa kwa Bernd Leno ni jambo zuri kwani kutasaidia kuongeza uwezo kwa kujiamini kwa mchezaji huyo.
#COYG
Speak Your Mind