Boreham Wood 0-8 Arsenal

orreJana Arsenal ilianza vyema maisha mapya chini ya kocha Unai Emery baada ya kuichapa timu ya Boreham Wood kwa goli 8-0 katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Boreham Wood 0-8 Arsenal

Mashabiki wengi wa Arsenal walionekana kuwa na hamu kubwa ya kuona timu yao ikiwa uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kocha huyo raia wa Hispania aanze kuionoa.

Akichanganya wachezaji makinda na wakongwe, Arsenal walianza mchezo huo vizuri kwani ndani ya dakika 18 za kwanza tayari walikuwa wanaongoza kwa magoli 3-0.

Pierre-Emerick Aubameyang alifunga goli la kwanza baada ya kupiga mpira kiufundi na mlinda mlango wa Boreham Wood hakuweza kufanya lolote kuuzuia kuingia nyavuni.Dakika mbili baadaye alifunga goli la pili baada ya kumalizia krosi safi iliyopigwa na Ainsley Maitland-Niles.

Mshambuliaji huo wa kimataifa wa Gabon alifanikiwa kufunga goli la tatu kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Reiss Nelson kuangushwa ndani ya eneo la hatari.Kinda huyo alifunga goli la nne dakika chache baadaye.

Maitland-Niles na  Emile Smith Rowe walipigiana pasi ambazo ziliwachanganya mabeki wa Boreham Wood, ambapo mpira ulipomfikia Aubamayang, alipiga pasi ndefu ambayo ilimkuta Alexandre Lacazette, ambaye alifunga goli la tano.

Kipindi cha pili Arsenal ilifanya mabadiliko 11 ambapo wachezaji kama Aaron Ramsey,Mkhitaryan.Mabadiliko hayo yaliisaidia Arsenal kwani kinda Eddie Nketiah aliiandikia Arsenal goli la sita.

Jeff Reine-Adelaide ambaye amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa anaichezea timu Angers, alifunga goli la saba.

Mchezaji Mkhitaryan,aliifungia Arsenal goli la nane na la mwisho baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Eddie Nketiah.

Hadi mchezo huo unaisha Boreham Wood 0-8 Arsenal.

Baada ya mchezo huo Arsenal itaendelea na mazoezi katika viunga vya Colney,na wiki ijayo watasafiri kwenda singapole kwa ili kushiriki katika kombe la kimataifa.

Kwa wale ambao hawajaona magoli hayo hapa chini nimekuwekea magoli yote.

Speak Your Mind

*