Carl Jenkinson ajiunga na Nottingham Forest

Wakati dirisha la usajili likielekea ukingoni, Arsenal imeendelea kukifanyia mabadiliko kikosi chake baada ya leo kutanganza kuondoka wa beki wake wa kulia Carl Jenkinson.

Carl Jenkinson ajiunga na  Nottingham Forest

Mchezaji huyo ambaye ni shabiki wa Arsenal, amejiunga na timu ya daraja la kwanza ya Nottingham Forest kwa mkataba wa miaka mitatu ingawa bado haijafahamika Arsenal wamepata kiasi gani kutokana na uhamisho huo.

Carl Jenkinson ambaye alianzia maisha yake ya soka katika timu ya Charlton Athletics kabla ya kujiunga na Arsenal mwezi wa saba mwaka 2011, alizichezea kwa mkopo timu za West Ham na Birmingham.

Beki huyo wa kulia amekosa namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kwani licha ya kuwepo kwenye timu kwa miaka mingi ameichezea Arsenal katika michezo 70.

Pamoja na kutokucheza michezo mingi nitamkumbuka Carl kwa kumweka mfukoni Arjen Robben pale Alianz Arena katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Kila la Heri Carl Jenkinson.

#COYG

Tupia Maoni Yako Hapo Chini