Crystal Palace vs Arsenal-Mtazamo wangu

Baada ya Arsenal kuifunga timu ya Sporting Lisbon katika michuano ya Europa League, leo inachezaitajaribu kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya timu ya Crystal Palace katika muendelezo wa ligi kuu ya Uingeleza.

Crystal Palace vs Arsenal-Mtazamo wangu

Majeruhi

Taarifa pekee nilizopata ni kwamba Petr Cech ameshapona na yupo tayari kuanza, na niliona mahojiano ya kocha Unai Emery na kituo cha Sky Sports ambapo alikuwa anasema ya kwamba inabidi afanye maamuzi magumu ya kuchagua kati ya makipa hao wawili nani aanze kwani wote wamefnya vizuri hadi sasa.

Upande wa kushoto bado kuna tatizo na ni mategemeo yangu kwamba kutakuwa ba beki wa kushoto leo na kama hawatakuwa fiti kucheza naamini ya kwamba Stephan Lichtsteiner ataanza upande huo.

Habari njema kwa mabeki wa Arsenal ni kwamba Christian Benteke hawezi kucheza katika mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi, ingawa bado Crystal Palace wana safu nzuri ya ushambuliaji ikiongozwa na Wilfred Zaha.

Kikosi

Rob Holding amecheza mechi nyingi anaweza akapumzishwa na Granit Xhaka akarudi katika nafasi yake ya kiungo wa kati baada kucheza kama beki wa kushoto katika mchezo uliopita.

Wachezaji wengine natagemea walewale ambao walicheza dhidi ya Leicester City jumatatu iliyopita.

Crystal Palace vs Arsenal-Mtazamo wangu

Utabiri

Huu ni mchezo mgumu lakini Palace kwa sasa hawachezi vizuri sana na pia hawana rekodi nzuri dhidi ya Arsenal, naamini Arsenal itapata ushindi wake wa 12.

Crystal Palace 0-2 Arsenal , Lacazette kufunga goli la kwanza

 

Speak Your Mind

*