Dani Ceballos ajiunga tena na Arsenal kwa Mkopo

Timu ya Arsenal imetangaza kurudi tena kwa kiungo Dani Ceballos kutoka Real Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Dani Ceballos

Dani Ceballos mwenye umri wa miaka 24 aliichezea Arsenal msimu uliopita akitokea Real Madrid na baada ya kumalizika msimu alilazimika kurudi katika timu yake.

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Arsenal walikuwa katika mazungumzo na timu ya Real Madrid ili mchezaji huyo aendelee kuichezea Arsenal kwa mwaka mmoja zaidi.

Jana kulikuwa na taarifa za kwamba timu hizo zimefikia makubaliano ambapo Arsenal italipa mshahara wote wa Ceballos hadi mwezi wa sita mwakani na haitalazimika kumnunua mchezaji huyo ama kuipa pesa Madrid ili kufanikisha mkopo huo.

Ceballos alikuwa sehemu muhimu ya kiungo cha Arsenal msimu uliopita baada ya kucheza kwa maelewano makubwa na Granit Xhaka na kuisaidia Arsenal kubeba kombe la FA.

Mchezaji huyo ataendelea kuvaa jezi namba nane kwa msimu ujao.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini