Danny Welbeck awazamisha Sporting Lisbon

Danny Welbeck jana alikuwa shujaa wa Arsenal baada ya kuifungia bao pekee na kuifanya Arsenal iifunge timu ya Sporting Lisnon ya Ureno kwa gli 1-0.

Danny Welbeck awazamisha Sporting Lisbon

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery alifanya mabadiliko sita ya wachezaji, huku kiungo Granit Xhaka akianza kama beki wa kushoto kutokana na mabeki wote wa kushoto kuwa majeruhi.

Arsenal waliuanza mchezo huo taratibu hali iliyowapa Sporting Lisbon nafasi ya kutawala mchezo huo lakini kukosa umakini kwa safu yao ya ushabluliaji kilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao kwani hadi timu hizo zinaenda mapumziko, wareno hao walikuwa hawajapiga shuti hata moja kulenga goli la Arsenal.

Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana.

Kama kawaida Arsenal walikianza kipindi cha pili kwa nguvu na mabadiliko ya kumtoa Mohamed Elneny na kuingia Lucas Torreira yalibadilisha sana hali ya mchezo na kuifanya Arsenal itawale kipindi chote cha pili.

Iliwachukua Arsenal hadi dakika ya 77 kupata goli baada ya beki wa Sporting Lisbon,Sebastian Coates, kufanya makosa wakati akiokoa mpira na kumpa nafasi Danny Welbeck aliyepiga mpira wa kiufundi na kuiandikia Arsenal goli pekee na la ushindi.

pamoja na Arsenal kushambulia sana walishindwa kupata goli la pili hivyo hadi mwisho wa mchezo,Arsenal 1-0 Sporting Lisbon.

Ushidi huo unaiweka Arsenal kileleni mwa kundi E, ikiwa na pointi 9 baada ya kushinda michezo yake yote mitatu.

Pia Ushindi huo unaifanya Arsenal iendeleze wimbi la ushindi kwani kwa sasa imefanikiwa kushinda michezo 11 katika michezo 11.

Speak Your Mind

*