David Luiz, Cedric Soares na Pablo Mari wasaini mikataba mipya

Vyombo vingi vya habari vimeripoti wa kuamkia leo ya kwamba wachezaji David Luiz, Cedric Soares na Pablo Mari wamesaini mikataba mipya ya kuendelea kuichezea Arsenal.

David Luiz asaini mwaka mmoja

David Luiz, Cedric Soares na Pablo Mari wasaini mikataba mipya

David Luiz alisajiliwa kutoka Chelsea msimu uliopita, mwanzoni ilidaiwa ya kwamba alisaini mkataba wa miaka miwili lakini baadaye ikagundulika ya kwamba amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Sasa Arsenal wameamua kumuaongezea mwaka mmoja zaidi hadi tarehe 30 ya mwezi wa sita mwakani, uamuzi wa kumpatia mkataba mpya mchezji huyo umepokea na hisia hasi na mashabiki wengi wa Arsenal kwani mchezaji huyo amekuwa akifanya makosa makubwa mengi katika michezo mingi aliyoichezea Arsenal. Mfano wa mwisho ukiwa ni jumatano ya wiki iliyopita baada ya kutoa boko kwa goli la kwanza la Man City na kusababisha penati ya goli la pili na pia kupewa kadi nyekundi.

Alifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Chelsea na pia dhidi ya Liverpool.

Cedric Soares

Huyu ni mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Southampton, inasemekana Arsenal ilitoa paundi milioni tano ili kumpata mchezaji huyo.

Soares ana miaka 28, mwezi wa tisa atakuwa na miaka 29 inasemekana ya kwamba amepewa mkataba wa miaka minne.

Ikumbukwe ya kwamba mchezaji huyo hajaichezea Arsenal katika mchezo wowote,  kwani alisajiliwa akiwa majeruhi na hajafanikiwa kupona mpaka leo, uamuzi wa kumpa mkataba wa miaka minne ni wa kushangaza.

Mchezaji huyu ametua Arsenal bure baada ya mkataba wake kumalizika.

Pablo Mari

Pablo Mari alisajiliwa kwa mkopo kutoka katika timu ya Flamengo ya Brazil, inaonekana ya kwamba Arsenal wameukubali uwezo wake na kuamua kumchukua moja kwa moja.

Inasemekana ya kwamba Arsenal walilipa paundi milioni 4.5 kumpata mchezaji huyo kwa mkopo na sasa wamewapatia Flamengo paundi nyingine milioni 10 na kufanya ada ya kumsajili mchezji huyo kuwa paundi milioni 14.5.

Pablo Mari pia amepewa mkataba wa miaka minne.

Hao ndio wachezaji watatu wa Arsenal waliosaini mikataba mipya. Je wewe unauonaje usajili huyo? unaamini ya kwamba wachezaji hao watakuwa msaada kwa Arsenal? tupia maoni yako hapo chini.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini