Denis Suarez akaribia kutua Arsenal

Kiungo wa Barcelona, Denis Suarez anakaribia kutua Arsenal, hii ni kwa mujibu wa kituo cha luninga cha SkySport Italia.

Denis Suarez played under Unai Emery at Sevilla

Mchezaji huo ambaye ni raia wa Hispania, amewahi kufundishwa na kocha wa sasa wa Arsenal, Unai Emery na inasemekana ya kwamba yupo tayari kufanya kazi na bosi wake wa zamani, mchezaji huyo pia anatakiwa na timu za AC Milan na Roma.

Suarez alisajiliwa na Manchester City  mwezi wa tano mwaka 2011, lakini alikosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na kuamua kutimkia Barcelona ya kwao Hispania mwaka 2013.

Baadaye alienda kuichezea timu ya Sevilla kwa mkopo akitokea Barcelona na hapo ndipo alipokutana na Unai Emery.

Mwaka 2015 alisajiliwa na timu ya Villarreal ambapo alicheza kwa muda usiozidi mwaka mmoja kabla ya kurudi tena Barcelona kwa dau la Euro milioni 3.5, sasa anatafuta kuhama tena baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika timu hiyo ya katarunya.

Speak Your Mind

*