Emirates FA Cup-Arsenal kucheza na mshindi kati ya Solihull au Blackpool

Ratiba ya michuano ya Emirates FA Cup imetoka na Arsenal imepangiwa kucheza ugenini na mshindi kati ya Solihull au Blackpool.

Emirates FA Cup-Arsenal kucheza na mshindi kati ya Solihull au Blackpool

Mshindi wa mchezo kati ya Solihull au Blackpool atapakitana tarehe 11 ya mwezi huu wakati Solihull watakaposafiri kwenda  Bloomfield Road kwa ajili ya mchezo wa marudio baada ya timu hizo kutoka 0-0 mwishoni mwa wiki.

Arsenal haijawahi kucheza na Solihull ambayo inacheza ligi daraja la tatu la Uingeleza, Blackpool na Arsenal zilicheza katika raundi ya nne ya kombe la Carabao ambapo Arsenal ilishinda kwa jumla ya goli 2-1.

Raundi ya tatu ya michuano hiyo itafanyika mwisho wa juma wa wiki inayoanza tarehe 5 ya mwezi wa kwanza mwaka 2019.

Binafsi ningependa Arsenal icheze na Solihull kwa sababu ni timu ambayo hatujawahi kucheza nayo lakini kati ya hao wawili yeyote tunaweza kumfunga na kikosi chetu cha pili.

 

Speak Your Mind

*