Freddie Ljungberg aondoka Arsenal

Arsenal imepata pigo kubwa baada ya kocha wake msaidizi Freddie Ljungberg kujiudhuru wadhifa huo na kutangaza ya kwamba anaondoka.

Fredie ambaye alikuwa ni kiungo muhimu katika jopo la makocha la Arsenal chini ya kocha mkuu Mikel Arteta ameamua kuondoka ili kutimiza kiu yake ya kuwa kocha mkuu.

Ljungberg ambaye ni mchezaji wa zamani wa Arsenal amewahi kushika nafasi mbali mbali katika timu ya Arsenal ikiwemo kocha mkuu wa muda baada ya kutimuliwa kwa Unai Emery.

Freddie Ljungberg aondoka Arsenal

Mkongwe huyo aliutimia ukurasa wake wa twitter kudhibitisha habari hizo ambapo aliushukuru uongozi wa Arsenal kwa kumpa nafasi ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 1998 na sasa ameona ni vyema akae pembeni na kusubiri nafasi yake kama kocha mkuu katika timu nyingine.

Freddie Ljungberg alichezea Arsenal kwa miaka tisa kuanzia mwaka 1998 hadi 2007, alicheza michezo 325 baada ya hapo alizichezea timu za West Ham na Seattle Sounders kabla ya kustaafu na kujiunga na Arsenal kama balozi wa timu mwaka 2013.

Miaka mitatu baadaye alikuwa ni sehemu ya jopo la makocha wa timu ya vijana ambapo alikuwa anafundisha watoto wenye umri wa miaka 15.

Mwaka 2017 alijiunga na timu ya Wolfsburg kama kocha msaidizi kabla ya kurudi Arsenal mwaka 2018 kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 23.

Mwaka 2019 alichaguliwa kujiunga na timu ya wakubwa akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery, baada ya kutimuliwa Emery, Ljungberg aliteuliwa kuwa kaimu kocha mkuu wa Arsenal.

Freddie bado hakapata timu ila ameona bora akae pembeni kabla msimu haujaanza ili ikitokea akapata timu katikati ya msimu asiiache timu njiani.

Kila la heri mkongwe.

Comments

  1. Uwezo Mwasilembo says

    Safari njema

Tupia Maoni Yako Hapo Chini