Fulham Vs Arsenal-mtazamo wangu

Leo mida ya saa nane mchana Arsenal itakuwa ikipambana na timu ya Fulham katika uwanja wa Craven Cottage katika ligi kuu ya Uingeleza.

Arsenal ambao hawajapoteza mchoze wowote tangu wafungwe na Chelsea mwezi wa nane leo watakuwa na nafasi ya kuendeleza wimbi la ushindi.

Arsenal ambao walisafiri kwenda Azerbaijan na kufanikiwa kuifunga timu ya Qarabaq kwa jumla ya magoli 3-0 inaweza kukabiliwa na tatizo la uchovu wa safari.

Lakini kocha mkuu wa Arsenal juzi alisema ya kwamba hilo halitakuwa tatizo kwani wachezaji wake wapo fiti na wamejiandaa vya kutosha ili kuwafunga Fulham.

Majeruhi

Hakuna majeruhi wapya katika kikosi cha Arsenal, Aubamayang aliyekuwa anaumwa amepona na jana alifanya mazoezi, Mkhitaryan ambaye hakusafiri kuelekea Baku kutokana na matatizo ya kisiasa yupo tayari kucheza, ingawa Aaron Ramsey anaweza kukosa mchezo huo kutokana na mkewe kuwa karibu na kujifungua watoto mapacha.

Mfumo

Kocha wa Arsenal Unai Emery, alitumia mfumo wa 3-4-2-1 katika mchezo dhidi ya Qarabaq, lakini naamini leo atarudi kwenye mfumo anaoutumia kwenye ligi kuu ambao ni 4-2-3-1.

Kikosi

Kutokana na Petr Cech kuwa majeruhi, Bernd Leno ataanza golini.

Binafsi ningependa Sokratis aanze na Rob Holding kama mabeki wa kati ila kuna kitu kinaniambia ya kwamba Emery atampumzisha Holding na nafasi yake kuchukuliwa na Mustafi. Beki wa kulia Bellerin na beki wa kushoto Nacho Monreal.

Viungo wa kati Lucas Torreira na Granit Xhaka kuongoza safu ya kiungo huku Mkhitaryan akicheza kama winga wa kulia, Mesut Ôzil kama kiungo mshambuliaji wa kati, Auba kama Winga wa kushoto huku Lacazette akianza kama mshambuliaji wa kati.

Fulham Vs Arsenal-mtazamo wangu

                                   

Utabiri

Najua Arsenal wana uchovu wa safari na Fulham wana wachezaji wazuri hasa sehemu ya kiungo ila naamini vijana wapo tayari na leo Arsenal anashinda 2-1.

#COYG

Speak Your Mind

*