Gabriel Martinelli Asaini mkataba mpya Arsenal

Mshambuliaji kinda wa Arsenal, Gabriel Martinelli amesaini mkataba mpya na wa muda mrefu ili kuendelea kuichezea Arsenal.

Gabriel Martinelli Asaini mkataba mpya Arsenal

Martinelli ambaye alijiunga na Arsenal mwaka mmoja uliopita akitokea timu ya Ituano ya kwano Brazil, amefunga magoli 10 na kutoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 4 katika michezo 26, ambapo alianza katika michezo 14 na kuingia kama mchezaji wa akiba katika michezo 12.

Kusaini kwa mchezaji huyo kunakuja masaa 48 tu toka kusaini kwa kinda mwingine wa Arsenal, Bukayo Saka.

Wachezaji wote wawili wamesaini mkataba wa miaka mitano hivyo kuipa nafasi Arsenal ya kuendelea kuwatumia kwa miaka mingi ijayo.

Habari za kusaini mkataba wa Martinelli na Saka ni muendelezo wa wiki nzuri kwa mashabiki wa Arsenal, kwani wiki hii pia timu ilishinda goli 4-0, kocha mkuu alitangaza ya kwamba ana uhakika ya kwamba nahodha Aubamayang atasaini mkataba mpya.

Habari njema zimekuwa adimu sana kwa mashabiki wa Arsenal katika miezi ya hivi karibuni.

Ni matumaini yetu ya kwamba kusaini kwa makinda hao wawili wenye uwezo mkubwa ni mwanzo mwema wa kuijenga upya Arsenal ambayo imeshuka sana kiwango katika miaka ya karibuni.

 

 

Comments

  1. edward joe says

    hiki ni kitu kizuri ila itatupendeza sana pale tutakapo ona nahodha wa timu Aubameyang anasaini mkataba tena

  2. Ni vizuri Aubameyang asaini mkataba upya ili kujenga timu yetu pia kocha asajili beki na viungo wenye uwezo wa kupeleka mpira mbele

Tupia Maoni Yako Hapo Chini