Gabrielli Martinelli aumia, kuwa nje miezi kadhaa

Mshambuliaji kinda wa Arsenal, Gabrielli Martinelli ameumia mazoezini baada ya kugongana na mchezi mwingine mazoezini na kuwa nje kwa miezi kadhaa.

Gabrielli Martinelli aumia, kuwa nje miezi kadhaa

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo dhidi ya Southampton, kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta alisema ya kwamba mchezaji huyo aliumia jana mazoezini baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi.

Ndio Martinelli aliumia mazoezini, na leo amefanyiwa vipimo na madaktari, habari mbaya ni kwamba mchezaji huyo atakuwa nje kwa muda wa miezi kadhaa, alisema kocha huyo.

Kuumia kwa mchezaji huyo ni muendelezo wa balaa la majeruhi lililoikumba Arsenal baada ya kuanza upya kwa ligi kuu ya Uingeleza.

Pablo Mari na Granit Xhaka waliumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester City wakati David Luiz alipata kadi nyekundu.

katika mchezo wa pili dhidi Brighton, golikipa tegemeo bernd Leno aliumia na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6.

Hapo bado haujawaongezea Cedric Soures, Lucas Torreira, na Calum Chambers.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini