Tetesi-Ivan Gazidis kutimkia AC Milan

Mtendaji mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis yupo mbioni kujiunga na timu ya AC Milan akiwa kama mtendaji mkuu wa timu hiyo.

Tetesi-Ivan Gazidis  kutimkia AC Milan

Taarifa kutoka Italia zinaelezea ya kwamba kampuni ya kimarekani iitwayo Elliott Management, imechukua umiliki wa timu hiyo ya Italia baada ya mmiliki wake wa zamani Li Yonghong kushindwa kulipa deni la paundi milioni 28.

Mwandishi wa habari Gianluca Di Marzio na kituo cha luninga cha Sky Italia wanahabarisha ya kwamba baada ya mkutano jijini London jumatatu hii.Mtendaji mkuu wa Roma Umberto Gandini atajiunga na timu hiyo kama Meneja wa timu.

Mbrazil Leonardo atajiunga na timu hiyo kama mkurugenzi wa Ufundi na Ivan Gazidis, atajiunga kama mtendaji mkuu wa timu hiyo.

Kwa sasa Gazidis yupo nchini Singapole akiwa na kikosi cha Arsenal katika michezo ya kirafiki kujiandaa na msimu ujao.

Gazidis ndiye aliyesimamia mageuzi ya Arsenal baada ya kuondoka kwa kocha mkongwe Arsenal Wenger na baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 10 ndiye kiongozi wa ngazi ya juu aliyekaa muda mrefu katika timu, hivyo kuondoka kwake kunaweza kuifanya Arsenal kuteteleka.

Mimi binafsi siamini kama Gazidis ataondoka kwani yeye ndiye aliyefanikisha mipango ya kumuondoa Arsene Wenger, na kapata madaraka aliyokuwa anayataka, sioni sababu ya kuhamia AC Milan, kwani kwa sasa Arsenal ni timu kubwa na ina pesa zaidi kuliko Milan.

 

 

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Arsenal imetangaza kikosi cha wachezaji 25 ambao watasafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki ili kujiandaa na msimu ujao.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

Wachezaji wengi wa Arsenal walianza mazoezi tangu mwanzoni mwa mwezi huu, na sasa wataungana na wachezaji wengine ambao walitolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia,Mesut Ozil, Mohamed Elneny na Alex Iwobi.

Timu itaondoka London jumapili na itaelekea Singapore ambapo itashiriki katika kombe la International Champions Cup, dhidi ya Atletico Madrid, alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu na dhidi ya Paris Saint Germain, jumamosi tarehe 28 ya mwezi huu.Michezo yote itaanza saa 7:30 kwa saa za Singapore.

Wachezaji wapya Bernd Leno, Sokratis na Matteo Guendouzi wote wanasafiri na kikosi , pia wachezaji waliokuwepo msimu uliopita kama  Pierre-Emerick Aubameyang, Hector Bellerin, Petr Cech, Calum Chambers, Rob Holding, Alexandre Lacazette, Ainsley Maitland-Niles, Henrikh Mkhitaryan, Shkodran Mustafi na Aaron Ramsey nao pia wanasafiri.

Katika kikosi hicho mchezaji Jeff Adelaide ameachwa huku kukiwa na tetesi za kwamba anaenda kwa mkopo,Chuba Akpom pia ameachwa kwani kuna tetesi ya kwamba anakaribia kuhamia timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la paundi milioni 2.

Kikosi kamili ni kama kinavyoonekana kwenye picha.

Arsenal yatangaza kikosi cha wachezaji 25 wanaosafiri kuelekea Singapore

 

 

Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0

Arsenal leo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Crawley town na kufanikiwa kuifunga timu hiyo kwa jumla ya goli 9-0.

Katika mchezo huyo uliofanyika ndani ya viwanja vya mazoezi vya Arsenal,London Colney.Ulifanyika kwa siri na hakuna mashabiki wala waandishi wa habari walioruhusiwa kuuona.

Habari za mchezo huo zilivuja baada ya wachezaji wa Arsenal kuweka picha katika mitandao ya kijamii, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Jeff Adelaide ambaye aliweka picha kwenye ukurasa wake akishangilia moja ya magoli hayo ambaye yeye alifunga.

Mchezaji mwingine ambaye alifunga katika mchezo huo alikuwa ni Henrik Mkhitaryan ambaye pia aliweka picha kwenye mitandao ya kijamii ikionesha  akishangilia goli.

Taarifa tulizopata ni kwamba kikosi kilichocheza ni kile kile kilichoifunga Boreham Wood goli 8-0, Pia katika mchezo huo golikipa mpya wa Arsenal Bernd Leno alidaka kwa mara ya kwanza.

Kwa sasa hatuna taarifa kamili ya wafungaji wala video ya mchezo huo, ila tumefanikiwa kupata baadhi ya picha za mchezo huo  ambazo tukakuwekea hapa chini.

Wafungaji
Timu ya kwanza (walicheza dakika 60)
Reine adelaide: 1
Perez: 2
Lacazette: 2
Mkhitaryan: 1
 
Timu ya pili (walicheza dakika 30)
Aubameyang:1
Nketiah:1
Nelson:1

 

Leno akidaka katika mchezo dhidi ya Crawley town

Leno akidaka katika mchezo dhidi ya Crawley town

 

Jeff akishangilia goli katika mchezo dhidi ya Crawley town

Jeff akishangilia goli katika mchezo dhidi ya Crawley town

Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0 Arsenal yaichapa Crawley town kwa magoli 9-0

Mesut Özil kusafiri na Arsenal kuelekea Singapore

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery amedhibitisha ya kwamba kiungo mchezeshaji wa Arsenal, Mesut Özil atakuwa ni mmoja ya wachezaji watakaosafiri na Arsenal kuelekea nchini Singapore  katika ziara ya michezo na mazoezi ya  kujiandaa na msimu mpya wa ligi na michuano mingine.

Mesut Özil kusafiri na Arsenal kuelekea Singapore

Arsenal watasafiri kuelekea katika bara la Asia mwishoni mwa wiki hii na Emery amedhibitisha ya kwamba Özil, Mohamed Elneny na  Alex Iwobi watajiunga na wachezaji wengine katika safari hiyo.

“Wachezaji wote ni sawa,” Emery aliuambia mtandao rasmi wa Arsenal.”Walikuwa na wiki kadhaa za mapumziko, najua ya kwamba wobi, Elneny na Mesut Ozil wanajiunga na timu katika safari ya Singapore”.

Arsenal watacheza na Atletico Madrid katika uwanja wa taifa wa Singapore katika kombe la International Champions Cup, alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu.

 

Boreham Wood 0-8 Arsenal

orreJana Arsenal ilianza vyema maisha mapya chini ya kocha Unai Emery baada ya kuichapa timu ya Boreham Wood kwa goli 8-0 katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Boreham Wood 0-8 Arsenal

Mashabiki wengi wa Arsenal walionekana kuwa na hamu kubwa ya kuona timu yao ikiwa uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kocha huyo raia wa Hispania aanze kuionoa.

Akichanganya wachezaji makinda na wakongwe, Arsenal walianza mchezo huo vizuri kwani ndani ya dakika 18 za kwanza tayari walikuwa wanaongoza kwa magoli 3-0.

Pierre-Emerick Aubameyang alifunga goli la kwanza baada ya kupiga mpira kiufundi na mlinda mlango wa Boreham Wood hakuweza kufanya lolote kuuzuia kuingia nyavuni.Dakika mbili baadaye alifunga goli la pili baada ya kumalizia krosi safi iliyopigwa na Ainsley Maitland-Niles.

Mshambuliaji huo wa kimataifa wa Gabon alifanikiwa kufunga goli la tatu kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Reiss Nelson kuangushwa ndani ya eneo la hatari.Kinda huyo alifunga goli la nne dakika chache baadaye.

Maitland-Niles na  Emile Smith Rowe walipigiana pasi ambazo ziliwachanganya mabeki wa Boreham Wood, ambapo mpira ulipomfikia Aubamayang, alipiga pasi ndefu ambayo ilimkuta Alexandre Lacazette, ambaye alifunga goli la tano.

Kipindi cha pili Arsenal ilifanya mabadiliko 11 ambapo wachezaji kama Aaron Ramsey,Mkhitaryan.Mabadiliko hayo yaliisaidia Arsenal kwani kinda Eddie Nketiah aliiandikia Arsenal goli la sita.

Jeff Reine-Adelaide ambaye amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa anaichezea timu Angers, alifunga goli la saba.

Mchezaji Mkhitaryan,aliifungia Arsenal goli la nane na la mwisho baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Eddie Nketiah.

Hadi mchezo huo unaisha Boreham Wood 0-8 Arsenal.

Baada ya mchezo huo Arsenal itaendelea na mazoezi katika viunga vya Colney,na wiki ijayo watasafiri kwenda singapole kwa ili kushiriki katika kombe la kimataifa.

Kwa wale ambao hawajaona magoli hayo hapa chini nimekuwekea magoli yote.

Arsenal waanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery, kwa mara ya kwanza alisimamia mazoezi ya timu hiyo akijiandaa kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingeleza na michuano mingine.

Katika mazoezi hayo yaliyohudhuriwa na wachezaji wote wa Arsenal ambao hawakushiriki kombe la dunia linaloendelea nchini Urusi, wachezaji wengi wa Arsenal walionekana kuwa katika hali ya uchangamfu na furaha wakati mazoezi hayo yakiendelea.

Katika siku ya kwanza mazoezi mengi yalikuwa ni ya viungo na gym ili kuipasha moto misuri kabla ya kuanza mazoezi magumu na mechi za kirafiki.

Wachezaji kama Aaaron Ramsey,Mustadifi,Kolasinac, Aubamayang,Lacazette,Bellerin,Mkhityrarian,Cech,Damien Martinez, Chambers na makinda kama Eddie Nketiah, Nelson, Josh Da Silva walishiriki katika mazoezi hayo.

Arsenal waanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya

Unai Emeri aliongoza kwa mara ya kwanza mazoezi ya Arsenal kujiandaa na msimu mpya

Kazi kubwa ya Emery msimu huu itakuwa ni kuirudisha Arsenal katika nafasi za ushindani katika ligi kuu ya Uingeleza na kuirudusha kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya katika msimu ujao.Arsenal ilimaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita na kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya Europa League.

Hapa chini nimekuwekea video ya baadhi ya matukio yaliyotokea katika mazoezi ya jana.

Unai Emery atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal

Kocha wa Arsenal Unai Emery jana alikutana alitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal katika tukio lililotokea katika uwanja wa Emirates.

Unai Emery atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal

Unai Emery

Emery alikutana kwa mara ya kwanza na mashabiki wa Arsenal katika tukio ambalo liliandaliwa na mtendaji mkuu wa Arsenal,Ivan Gazidis.

Baada ya mashabiki wengi wa Arsenal kugawanyika kufuatia kufanya vibaya kwa timu,Gazidis ameanza harakati za kuwaunganisha mashabiki na timu yao na hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwakutanisha mashabiki na kocha mpya.

Katika mkutano huo kuna mambo mengi yalitokea nitajitahidi kuelezea baadhi ambayo mimi naona yana umuhimu zaidi

Unai Emery

Soka la kuvutia kurudi Arsenal

Moja ya vitu alivypoahidi Unai Emery katika mkutano wa jana ilikuwa ni kuunda timu ambayo itacheza soka la kuvutia.

Nataka kuunda timu ambayo itawafanya mashabiki wa Arsenal kufurahia na kuimba kila dakika uwanjani lakini alionya ya kwamba wasahau ushindi wa 1-0 ambao ulikuwa maarufu sana ile miaka ya 90.

Anataka wachezaji kujituma dakika zote 90 uwanjani.

“nataka timu ya watu wanaotaka kushinda , nataka wachezaji wawe na njaa ya ushindi katika kila mchezo,” alisema kocha huyo,  “nataka wajitume dakika zote 90 katika kila mchezo,nataka wafanye hivyo kila siku, hiki ndicho kitu ninachokitaka.Nataka mashabiki waifurahie hii timu.

Aelezea kwa nini anataka timu kushinda 5-4 na sio 1-0

Pia katika mkutano huo Emery aliezea ya kwamba anapendelea timu ishinde kwa goli 5-4 kuliko 1-0, akisema sababu kubwa ni kwamba mashabiki hufurahia zaidi timu yao inapofunga magoli mengi, pia alisisitiza ya kwamba ataunda timu ambayo wakati mwingine itakuwa ikishinda 5-0 na kuwaacha mashabiki wengi waliokuwepo uwanjani hapo wakishangilia.

Aliongeza kiingeleza

Lugha yake ya asili ni kiispania, lakini katika mkutano huo pamoja na kuwa na mkalimani alijitahidi sana kujibu maswali kwa lugha ya kiingeleza, kitu ambacho kilionesha kuwafurahisha mashabiki wengi.

Alikutana na wafanyakazi wengine

Pia katika mkutano huyo Emery alikutana na wafanyakazi wengine ndani ya Arsenal, kuanzia walinzi, wapishi, wafagia ofisi na wengineo ambapo aliwashukuru kwa kufanya kazi kwa juhudi na kuisaidia Arsenal kuwa timu kubwa.

Ivan Gazidis

Usajili

Kuna shabiki mmoja aliulizia mipango ya usajili, na mtendaji mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis alisema ya kwamba tayari wameshaongeza na Unai na wanajua nini anataka hivyo yeye pamoja na wenzake (Raul na Sven) watafanya kila wawezalo kuhakikisha ya kwamba wanawapata wachezaji watakaoboresha kikosi cha sasa, pia alisema ya kwamba kuna wachezaji wa sasa ambao wanaweza kuondoka.

Amzungungumzia David Dein

Kuna shabiki mmoja aliuliza ya kwamba kama Gazidis kama anataka kumuiga David Dein ambaye alikuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Arsenal.Kuhusu hili Gazidis alisema ya kwamba anautambua mchango mkubwa wa David Dein ndani ya Arsenal ila kwa sasa mchezo wa soka umebadilika sana ndiyo maana yeye ameamua kuajili wataalam wa kusaidiana naye kwani hawezi kufanya kazi peke yake.

Arsenal sio timu ya mtu mmoja

Pia Gazidis alisisitiza ya kwamba mfumo wa uendeshwaji wa timu ya Arsenal umebadilika kwa sasa kutoka ule wa mtu mmoja kufanya  karibu kila kitu ambapo kwa sasa mambo yote yatafanywa na watu wengi.

Aizungumzia Totenham

Kuna mshabiki mmoja alimuuliza Gazidi ‘Unafikilia nini kuhusu Totenham? ‘  Gazidis alitabasamu na kusema hilo ni swali gumu sana na siwezi kujibu.

Sven na Raul walitambulishwa pia

Katika mkutano huo pia walitambulishwa msaka vipaji mkuu wa Arsenal, Sven Mislitant na mkurugenzi wa Arsenal, Raul Sahleli.

Kwa kifupi hayo ndiyo mambo yaliyotokea katika mkutano wa jana kati ya uongozi wa Arsenal na mashabiki wa Arsenal katika tukio lililotokea katika uwanja wa Emirates.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Lehman aondoka

*Steve Bould abaki

Arsenal imeendelea na wimbi la mabadiliko ambapo leo imetangaza benchi jipya la ufundi litakalomsaidia kocha mkuu Unai Emery.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

Benchi jipya la ufundi litakalokua chini ya Unay Emery(pichani) limetangazwa

Katika mabadiliko hayo Unai atakuwa na jopo la ufundi litakaloundwa na kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Juan Carlos Carcedo,kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Steve Bould; Kocha wa kikosi cha kwanza, Pablo Villanueva,Mkurugenzi wa mtendaji wa kikosi cha kwanza, Darren Burgess,Kocha wa mazoezi ya kujenga mwili na viungo Julen Masach;Kocha wa makipa, Javi Garcia; Kocha wa makipa, Sal Bibbo na mtunza kumbukumbu za video Victor Manas.

Katika orodha ya hapo juu kuna watu watatu ambao walikuwa kwenye timu ya Arsene Wenger ambao ni Steve Bould, Sal Bibbo na Darren Burgess.

Waliobaki wote wamekuja na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Lehman atimka

Wakati huo huo asilimia kubwa la jopo la ufundi lililokuwa chini ya Wenger wameondoka akiwemo mchezaji wa zamani wa Arsenal Jens Lehman.

Wengine waliiondoka ni makocha wa kikosi chakwanza,  Neil Banfield, Tony Colbert, Jens Lehmann, Gerry Peyton na Boro Primorac; Mkuu wa kitengo cha utabibu (daktari mkuu wa Arsenal) , Colin Lewin; Daktari wa saikolojia Andy Rolls na Ben Ashworth; Daktari wa mifupa Dr Philippe Boixel na mratibu wa safari za Arsenal, Paul Johnson .

Tunapenda kuikaribisha timu mpya na kuwatakia mafanikio mema katika zama mpya za Arsenal na pia tunapenda kusema asante kwa kuitumikia Arsenal na kwa heri kwa wale wote walioondoka.

Arsenal yaingia mkataba na Tidal

Arsenal imepata mdhamini mpya baada ya kuingia mkataba na kampuni ya musiki Tidal.

Arsenal walitangaza jumatatu ya kwamba wameingia mtakaba na kampuni hiyo ambao inajihusisha na kusambaza mziki kwenye internet.

Huu ni mkataba wa pili ndani wa wiki chache zilizopita baada ya Arsenal kuingia mkataba na Visit Rwanda’ ambaowaliingiamkatabawenyedhamani ya dolamilioni 30 mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kwenye tovuti rasmi ya Arsenal hawajaelezea ni kiasi gani watapata katika mkataba huo, lakini mtandao wa Goal unadai ya kwamba katika mkataba huo Arsenal watakuwa wanalipwa paundi milioni 1 kwa mwaka.

Mkataba huo hauleti pesa nyingi lakini naamini utachangia katika mapato ya Arsenal, kwani timu kwa sasa inaonesha ya kwamba inafanya vizuri kiuchumi kwa kupata mikataba minono na ya pesa ndefu zaidi.

Arsenal ambayo haitashiriki katika michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya kwa msimu wa pili sasa inahitaji pesa kutoka kwa wadhamini ili iweke kufidia pesa ambazo imezikosa.

Pia sisi kama mashabiki wa Arsenal tunategemea ya kwamba pesa zitakazopatikana katika mikataba kama hii zitatumika katika kuiboresha timu kwa kufanya usajili wa maana.

Kama unataka kusikiliza nyimbo zilizochaguliwa na wachezaji wa Arsenal,Danny Welbeck, Hector Bellerin na  Reiss Nelson. Bofya hapa http://tidal.com/arsenal

 

 

Magoli yote 113 ya Arsenal msimu wa 2017/2018

Msimu ulioisha Arsenal iligunga magoli 113, hapa chini nimekuwekea video yenye magoli hayo yote.

 

Je goli lipi umelipenda zaidi ? tupia maoni yako hapa chini.

Ratiba ya mechi za kirafiki za Arsenal

Baada ya kufanya vibaya katika msimu uliopita Arsenal inajipanga upya ili isirudie makosa yale yale katika msimu ujao, moja ya mabadiliko makubwa ni kuondoka kwa kocha Arsene Wenger aliyekuwa na timu kwa miaka 22.

Pia kuna mabadiliko mengi makubwa yanayoendelea kufanyika nyuma ya pazia. Mpaka sasa Arsenal bado haijakamilisha rasmi usajili wa mchezaji yeyote ingawa taarifa za kuaminika ni kwamba watasajili wachezaji watatu kabla ya kuingia kambini kujiandaa na msimu ujao.

Arsenal ikiwa chini ya mwalimu mpya Unay Emery inatarakiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi tarehe 2 ya mwezi wa saba ambapo wachezaji vijana wataungana na wengine ambao hawatashiriki katika kombe la Dunia na kuanza mazoezi.

Wachezaji kama Alexandre Lacazette, Henrikh Mkhitaryan, Sead Kolasinac, Aaron Ramsey na Pierre Emerick-Aubameyang wanategemewa kuripoti mazoezini siku hiyo ya jumatatu ya tarehe 2 mwezi wa saba.

Mechi ya kwanza Arsenal ikiwa chini ya Emery

Emery ataisimamia Arsenal kwa mara ya kwanza akiwa kama kocha mkuu tarehe 14 ya mwezi wa saba ambapo siku hiyo vijana wake wa Arsenal watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya  Boreham Wood.

Huu ni mchezo wa kirafiki ambao hufanyika kila mwaka kuashiria kuanza kwa msimu mpya na kudumisha urafiki kati ya timu hizo mbili.

Baada ya mchezo huo Arsenal watapanda pia na kuelekea Singapore ambapo watashiriki katika kombe la International Champions Cup.Ambapo watacheza michezo miwili, watacheza na Atletico Madrid tarehe 26 ya mwezi wa saba na siku mbili baadaye wataumana na Paris Saint Germain tarehe 28 ya mwezi wa saba.

Ratiba ya mechi za kirafiki za Arsenal

Arsenal itarudi Ulaya ambapo watapambana wa watoto wa Pep Guardiola mjini Dublin tarehe 1 ya mwezi wa nane (mchezo huu bado haujathibitishwa ).

Mchezo wa mwisho wa kujipima nguvu utakuwa dhidi ya watoto wa darajani Chelsea mchezo huo utafanyika nchini Sweden.

Mwaka huu hakutakuwa na michuano ya kombe la Emirates kutokana na uwanja huo kuwa katika ukarabaki ili kuongeza idadi ya viti uwanjani.

Mradi huo umeshaanza na unategemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi wa nane na uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamani 60,600.

Ligi kuu ya Uingeleza inategemewa kuanza tarehe 11 ya mwezi wa nane mwaka huu.

Ratiba kamili ya mechi za kirafiki za Arsenal

Jul 14 – Boreham Wood v Arsenal, 3 pm Meadow Park, Borehamwood.

Jul 26 – Arsenal v Atletico Madrid, 12:30pm , Singapore National Stadium.

Jul 28 – Arsenal v PSG, 12:30pm ,Singapore National Stadium.

Aug 1 – Arsenal v Man City, Aviva Stadium, Dublin, Ireland.

*Aug 4 – Arsenal v Chelsea,  Friends Arena, Stockholm, Sweden.

Mechi dhidi ya Chelsea imeahirishwa kwa sababu Chelsea watacheza dhidi ya Manchester City tarehe 5 ya mwezi wa nane kugombea ngao ya jamii.