Arsenal waanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery, kwa mara ya kwanza alisimamia mazoezi ya timu hiyo akijiandaa kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingeleza na michuano mingine.

Katika mazoezi hayo yaliyohudhuriwa na wachezaji wote wa Arsenal ambao hawakushiriki kombe la dunia linaloendelea nchini Urusi, wachezaji wengi wa Arsenal walionekana kuwa katika hali ya uchangamfu na furaha wakati mazoezi hayo yakiendelea.

Katika siku ya kwanza mazoezi mengi yalikuwa ni ya viungo na gym ili kuipasha moto misuri kabla ya kuanza mazoezi magumu na mechi za kirafiki.

Wachezaji kama Aaaron Ramsey,Mustadifi,Kolasinac, Aubamayang,Lacazette,Bellerin,Mkhityrarian,Cech,Damien Martinez, Chambers na makinda kama Eddie Nketiah, Nelson, Josh Da Silva walishiriki katika mazoezi hayo.

Arsenal waanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya

Unai Emeri aliongoza kwa mara ya kwanza mazoezi ya Arsenal kujiandaa na msimu mpya

Kazi kubwa ya Emery msimu huu itakuwa ni kuirudisha Arsenal katika nafasi za ushindani katika ligi kuu ya Uingeleza na kuirudusha kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya katika msimu ujao.Arsenal ilimaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita na kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya Europa League.

Hapa chini nimekuwekea video ya baadhi ya matukio yaliyotokea katika mazoezi ya jana.

Unai Emery atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal

Kocha wa Arsenal Unai Emery jana alikutana alitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal katika tukio lililotokea katika uwanja wa Emirates.

Unai Emery atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Arsenal

Unai Emery

Emery alikutana kwa mara ya kwanza na mashabiki wa Arsenal katika tukio ambalo liliandaliwa na mtendaji mkuu wa Arsenal,Ivan Gazidis.

Baada ya mashabiki wengi wa Arsenal kugawanyika kufuatia kufanya vibaya kwa timu,Gazidis ameanza harakati za kuwaunganisha mashabiki na timu yao na hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwakutanisha mashabiki na kocha mpya.

Katika mkutano huo kuna mambo mengi yalitokea nitajitahidi kuelezea baadhi ambayo mimi naona yana umuhimu zaidi

Unai Emery

Soka la kuvutia kurudi Arsenal

Moja ya vitu alivypoahidi Unai Emery katika mkutano wa jana ilikuwa ni kuunda timu ambayo itacheza soka la kuvutia.

Nataka kuunda timu ambayo itawafanya mashabiki wa Arsenal kufurahia na kuimba kila dakika uwanjani lakini alionya ya kwamba wasahau ushindi wa 1-0 ambao ulikuwa maarufu sana ile miaka ya 90.

Anataka wachezaji kujituma dakika zote 90 uwanjani.

“nataka timu ya watu wanaotaka kushinda , nataka wachezaji wawe na njaa ya ushindi katika kila mchezo,” alisema kocha huyo,  “nataka wajitume dakika zote 90 katika kila mchezo,nataka wafanye hivyo kila siku, hiki ndicho kitu ninachokitaka.Nataka mashabiki waifurahie hii timu.

Aelezea kwa nini anataka timu kushinda 5-4 na sio 1-0

Pia katika mkutano huo Emery aliezea ya kwamba anapendelea timu ishinde kwa goli 5-4 kuliko 1-0, akisema sababu kubwa ni kwamba mashabiki hufurahia zaidi timu yao inapofunga magoli mengi, pia alisisitiza ya kwamba ataunda timu ambayo wakati mwingine itakuwa ikishinda 5-0 na kuwaacha mashabiki wengi waliokuwepo uwanjani hapo wakishangilia.

Aliongeza kiingeleza

Lugha yake ya asili ni kiispania, lakini katika mkutano huo pamoja na kuwa na mkalimani alijitahidi sana kujibu maswali kwa lugha ya kiingeleza, kitu ambacho kilionesha kuwafurahisha mashabiki wengi.

Alikutana na wafanyakazi wengine

Pia katika mkutano huyo Emery alikutana na wafanyakazi wengine ndani ya Arsenal, kuanzia walinzi, wapishi, wafagia ofisi na wengineo ambapo aliwashukuru kwa kufanya kazi kwa juhudi na kuisaidia Arsenal kuwa timu kubwa.

Ivan Gazidis

Usajili

Kuna shabiki mmoja aliulizia mipango ya usajili, na mtendaji mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis alisema ya kwamba tayari wameshaongeza na Unai na wanajua nini anataka hivyo yeye pamoja na wenzake (Raul na Sven) watafanya kila wawezalo kuhakikisha ya kwamba wanawapata wachezaji watakaoboresha kikosi cha sasa, pia alisema ya kwamba kuna wachezaji wa sasa ambao wanaweza kuondoka.

Amzungungumzia David Dein

Kuna shabiki mmoja aliuliza ya kwamba kama Gazidis kama anataka kumuiga David Dein ambaye alikuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Arsenal.Kuhusu hili Gazidis alisema ya kwamba anautambua mchango mkubwa wa David Dein ndani ya Arsenal ila kwa sasa mchezo wa soka umebadilika sana ndiyo maana yeye ameamua kuajili wataalam wa kusaidiana naye kwani hawezi kufanya kazi peke yake.

Arsenal sio timu ya mtu mmoja

Pia Gazidis alisisitiza ya kwamba mfumo wa uendeshwaji wa timu ya Arsenal umebadilika kwa sasa kutoka ule wa mtu mmoja kufanya  karibu kila kitu ambapo kwa sasa mambo yote yatafanywa na watu wengi.

Aizungumzia Totenham

Kuna mshabiki mmoja alimuuliza Gazidi ‘Unafikilia nini kuhusu Totenham? ‘  Gazidis alitabasamu na kusema hilo ni swali gumu sana na siwezi kujibu.

Sven na Raul walitambulishwa pia

Katika mkutano huo pia walitambulishwa msaka vipaji mkuu wa Arsenal, Sven Mislitant na mkurugenzi wa Arsenal, Raul Sahleli.

Kwa kifupi hayo ndiyo mambo yaliyotokea katika mkutano wa jana kati ya uongozi wa Arsenal na mashabiki wa Arsenal katika tukio lililotokea katika uwanja wa Emirates.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

*Lehman aondoka

*Steve Bould abaki

Arsenal imeendelea na wimbi la mabadiliko ambapo leo imetangaza benchi jipya la ufundi litakalomsaidia kocha mkuu Unai Emery.

Mabadiliko-Arsenal yatangaza benchi jipya la ufundi

Benchi jipya la ufundi litakalokua chini ya Unay Emery(pichani) limetangazwa

Katika mabadiliko hayo Unai atakuwa na jopo la ufundi litakaloundwa na kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Juan Carlos Carcedo,kocha mkuu msaidizi wa kikosi cha kwanza Steve Bould; Kocha wa kikosi cha kwanza, Pablo Villanueva,Mkurugenzi wa mtendaji wa kikosi cha kwanza, Darren Burgess,Kocha wa mazoezi ya kujenga mwili na viungo Julen Masach;Kocha wa makipa, Javi Garcia; Kocha wa makipa, Sal Bibbo na mtunza kumbukumbu za video Victor Manas.

Katika orodha ya hapo juu kuna watu watatu ambao walikuwa kwenye timu ya Arsene Wenger ambao ni Steve Bould, Sal Bibbo na Darren Burgess.

Waliobaki wote wamekuja na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Lehman atimka

Wakati huo huo asilimia kubwa la jopo la ufundi lililokuwa chini ya Wenger wameondoka akiwemo mchezaji wa zamani wa Arsenal Jens Lehman.

Wengine waliiondoka ni makocha wa kikosi chakwanza,  Neil Banfield, Tony Colbert, Jens Lehmann, Gerry Peyton na Boro Primorac; Mkuu wa kitengo cha utabibu (daktari mkuu wa Arsenal) , Colin Lewin; Daktari wa saikolojia Andy Rolls na Ben Ashworth; Daktari wa mifupa Dr Philippe Boixel na mratibu wa safari za Arsenal, Paul Johnson .

Tunapenda kuikaribisha timu mpya na kuwatakia mafanikio mema katika zama mpya za Arsenal na pia tunapenda kusema asante kwa kuitumikia Arsenal na kwa heri kwa wale wote walioondoka.

Arsenal yaingia mkataba na Tidal

Arsenal imepata mdhamini mpya baada ya kuingia mkataba na kampuni ya musiki Tidal.

Arsenal walitangaza jumatatu ya kwamba wameingia mtakaba na kampuni hiyo ambao inajihusisha na kusambaza mziki kwenye internet.

Huu ni mkataba wa pili ndani wa wiki chache zilizopita baada ya Arsenal kuingia mkataba na Visit Rwanda’ ambaowaliingiamkatabawenyedhamani ya dolamilioni 30 mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kwenye tovuti rasmi ya Arsenal hawajaelezea ni kiasi gani watapata katika mkataba huo, lakini mtandao wa Goal unadai ya kwamba katika mkataba huo Arsenal watakuwa wanalipwa paundi milioni 1 kwa mwaka.

Mkataba huo hauleti pesa nyingi lakini naamini utachangia katika mapato ya Arsenal, kwani timu kwa sasa inaonesha ya kwamba inafanya vizuri kiuchumi kwa kupata mikataba minono na ya pesa ndefu zaidi.

Arsenal ambayo haitashiriki katika michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya kwa msimu wa pili sasa inahitaji pesa kutoka kwa wadhamini ili iweke kufidia pesa ambazo imezikosa.

Pia sisi kama mashabiki wa Arsenal tunategemea ya kwamba pesa zitakazopatikana katika mikataba kama hii zitatumika katika kuiboresha timu kwa kufanya usajili wa maana.

Kama unataka kusikiliza nyimbo zilizochaguliwa na wachezaji wa Arsenal,Danny Welbeck, Hector Bellerin na  Reiss Nelson. Bofya hapa http://tidal.com/arsenal

 

 

Magoli yote 113 ya Arsenal msimu wa 2017/2018

Msimu ulioisha Arsenal iligunga magoli 113, hapa chini nimekuwekea video yenye magoli hayo yote.

 

Je goli lipi umelipenda zaidi ? tupia maoni yako hapa chini.

Ratiba ya mechi za kirafiki za Arsenal

Baada ya kufanya vibaya katika msimu uliopita Arsenal inajipanga upya ili isirudie makosa yale yale katika msimu ujao, moja ya mabadiliko makubwa ni kuondoka kwa kocha Arsene Wenger aliyekuwa na timu kwa miaka 22.

Pia kuna mabadiliko mengi makubwa yanayoendelea kufanyika nyuma ya pazia. Mpaka sasa Arsenal bado haijakamilisha rasmi usajili wa mchezaji yeyote ingawa taarifa za kuaminika ni kwamba watasajili wachezaji watatu kabla ya kuingia kambini kujiandaa na msimu ujao.

Arsenal ikiwa chini ya mwalimu mpya Unay Emery inatarakiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi tarehe 2 ya mwezi wa saba ambapo wachezaji vijana wataungana na wengine ambao hawatashiriki katika kombe la Dunia na kuanza mazoezi.

Wachezaji kama Alexandre Lacazette, Henrikh Mkhitaryan, Sead Kolasinac, Aaron Ramsey na Pierre Emerick-Aubameyang wanategemewa kuripoti mazoezini siku hiyo ya jumatatu ya tarehe 2 mwezi wa saba.

Mechi ya kwanza Arsenal ikiwa chini ya Emery

Emery ataisimamia Arsenal kwa mara ya kwanza akiwa kama kocha mkuu tarehe 14 ya mwezi wa saba ambapo siku hiyo vijana wake wa Arsenal watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya  Boreham Wood.

Huu ni mchezo wa kirafiki ambao hufanyika kila mwaka kuashiria kuanza kwa msimu mpya na kudumisha urafiki kati ya timu hizo mbili.

Baada ya mchezo huo Arsenal watapanda pia na kuelekea Singapore ambapo watashiriki katika kombe la International Champions Cup.Ambapo watacheza michezo miwili, watacheza na Atletico Madrid tarehe 26 ya mwezi wa saba na siku mbili baadaye wataumana na Paris Saint Germain tarehe 28 ya mwezi wa saba.

Ratiba ya mechi za kirafiki za Arsenal

Arsenal itarudi Ulaya ambapo watapambana wa watoto wa Pep Guardiola mjini Dublin tarehe 1 ya mwezi wa nane (mchezo huu bado haujathibitishwa ).

Mchezo wa mwisho wa kujipima nguvu utakuwa dhidi ya watoto wa darajani Chelsea mchezo huo utafanyika nchini Sweden.

Mwaka huu hakutakuwa na michuano ya kombe la Emirates kutokana na uwanja huo kuwa katika ukarabaki ili kuongeza idadi ya viti uwanjani.

Mradi huo umeshaanza na unategemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi wa nane na uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamani 60,600.

Ligi kuu ya Uingeleza inategemewa kuanza tarehe 11 ya mwezi wa nane mwaka huu.

Ratiba kamili ya mechi za kirafiki za Arsenal

Jul 14 – Boreham Wood v Arsenal, 3 pm Meadow Park, Borehamwood.

Jul 26 – Arsenal v Atletico Madrid, 12:30pm , Singapore National Stadium.

Jul 28 – Arsenal v PSG, 12:30pm ,Singapore National Stadium.

Aug 1 – Arsenal v Man City, Aviva Stadium, Dublin, Ireland.

*Aug 4 – Arsenal v Chelsea,  Friends Arena, Stockholm, Sweden.

Mechi dhidi ya Chelsea imeahirishwa kwa sababu Chelsea watacheza dhidi ya Manchester City tarehe 5 ya mwezi wa nane kugombea ngao ya jamii.

Tumerudi tena

Kwanza kabisa ningependa kuwaomba samahani wadau wote wanaotuunga mkono kwa kushindwa kuwa hewani kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.

Sababu kubwa za kupotea ni mbili.

Moja, kulikuwa na matatizo ya kiufundi ambayo yalisababisha kupoteza database zote( tovuti hii na tofuti nyingine tunazomiliki).

Mbili,kutokana na kulazimika kuanza upya, kazi kubwa ilikuwa inahitajika na kwa kweli tulikosa muda wa kufanya kila kitu (matatizo ya kifamilia, kuhama kutoka katika kituo cha kazi na kuingiliana na muda wa likizo).

Kutokana na sababu zote hizo tulikosa muda na kulazimika kuiacha hii tovuti kwa muda,kwa sasa tumerudi tena na tutaendelea kukuletea taarifa zote muhimu kuuhusu Arsenal.

Kwa sasa tumerudi tena na kuanza kuwaletea taarifa mbali mbali kuhusu timu yetu pendwa ya Arsenal.

Kwa Taarifa za uchambuzi kabla na baada ya mechi, uchambuzi wa mifumo ya uchezaji, wachezaji na mashabiki kwa ujumla, tetesi za usajili na habari nyinginezo kuhusu Arsenal usikose kututembelea kila siku.