Tetesi-Fernando Calero aonekana London

Beki wa kati wa timu ya Real Valladolid ya Hispania, Fernando Calero ameonekana mjini London na kuibua tetesi za kwamba yupo mbioni kujiunga na Arsenal.

Tetesi-Fernando Calero aonekana London

Fernando Calero (pichani juu) amehusishwa na kuhamia Arsenal

Sio siri ya kwamba Arsenal wapo sokoni wakitafuta beki wa kati baada ya Rob Holding kuumia na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9, Laurent Koscienly bado hajapona vizuri baada ya kuumia kifundo cha mguu mwezi wa tano mwaka huu.

Kutokana na tatizo la majeruhi ambapo mabeki wote ni majeruhi, kocha mkuu Unai Emery amelazimika kumtumia Granit Xhaka ambaye ni kiungo mchezeshaji kama beki wa kati hali inayoifanya timu kukosa mtu wa kuanzisha mashambulizi.

Calero ambaye ana umri wa miaka 23 ana kipengele kinachomruhusu kuhama timu hiyo kwa dau la paundi milioni 10 na inasemekana ya kwamba Arsenal wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa.

Mchezaji huyo aliongozea moto katika tetesi hizo baada ya kuweka picha jumapili usiku baada ya kuweka picha akiwa London Waterloo kwenye mtandao wa Instagram.

calero akiwa london

Je ungependa Fernando Calero atue Arsenal ? tupia maoni yako hapa chini.

Tetesi-Juan Mata kujiunga na Arsenal msimu ujao

Mtandao wa TalkSport umeandika ya kwamba mchezaji Juan Mata atajiunga na Arsenal msimu ujao baada ya kumaliza mkataba wake na Manchester United.

Tetesi-Juan Mata kujiunga na Arsenal msimu ujao

Juan Mata yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na kuna taarifa ya kwamba Man United bado hawajaanza mazungumzo ya kumpatia mkataba mpya.

Mata alicheza chini ya kocha wa wa Arsenal Unai Emery kwa miaka mitatu wakiwa na timu ya Valencia ya Hispania na katika kipindi hicho alifanikiwa kuingia katika timu ya taifa ya Hispania na baadaye kuhamia Chelsea.

Ni rahisi kugundua ya kwamba Mata sio chaguo la Mourinho kwani baada ya kurudi Chelsea kocha huyo alimuuza kiungo huyo kwa Manchester United.

Na sasa inaonekana ya kwamba kocha huyo yupo tayari kumuachia mchezaji huyo baada ya kugoma kumpa mkataba mpya na vyombo vya habari vinaanza kutunga tetesi za kuhamia Arsenal.

Juan Mata ana miaka 30, yupo katika mkataba mkubwa na Manchester United, sidhani kama kwa kiwango chake cha sasa anaweza akawa msaada kwa timu na pia sidhani kama Arsenal watakuwa tayari kumpa mshahara mkubwa mchezaji ambaye atakuwa hayupo katika kikosi cha kwanza.

Pia ikumbukwe ya kwamba Arsenal hawana bahati sana na wachezaji kutoka Man United, mchezaji wa mwisho kuhamia Arsenal kutokea timu hiyo ni Henrik Mkhitryan ambaye kwa mtazamo wangu hajaonesha kiwango kikubwa tangu atue mwezi wa kwanza mwaka huu.

Je wewe unasemaje kuhusu tetesi hizi? toa maoni yako hapa chini.

Tetesi-Arsenal wanampango wa kusajili Eric Bailly

Kuna taarifa za kwamba Arsenal wana mpango wa kumsajili beki wa Manchester United Eric Bailly, hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Guardian.

Tetesi-Arsenal wanampango wa kusajili Eric Bailly

Eric Bailly ambaye alikuwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwa dau la paundi milioni 30, inasemekana ni mmoja ya wachezaji ambao hawaivi na kocha huyo kwa sasa na anaweza akatupiwa vilago vyake katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza.

Katika taarifa nyingine tulizopata ni kwamba Manchester United wanataka kumtumia mchezaji huyo kama chambo cha kumpata nyota wa Arsenal Aaron Ramsey mwezi wa kwanza.

Eric Bailly alinunuliwa kwa paundi 30 mwaka 2916 na kuna tetesi za kwamba Arsenal wapo tayari kumuachia Ramsey mwezi wa kwanza kwa paundi milioni 25, hivyo Manchester United wanaona ya kwamba wanaweza kubadilishana wachezaji hao.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Arsenal na Manchester United kubadilishana wachezaji kwani walifanya hivyo kwa Alexis Sanchez na Henrik Mkhitaryan.

Binafsi sioni sababu ya Arsenal kumsajili Eric Bailly kwani ni beki anayetumia nguvu zaidi kuliko akili, hana uwezo wa kupiga pasi hivyo hataweza kumudu mfumo wa Arsenal ambapo wanapiga pasi kutokea kwa kipa.

Je wewe unasemaje kuhusu tetesi hizi? tupia maoni yako hapa chini.

Tetesi-Hector Herrera kumridhi Aaron Ramsey

Kiungo kutoka Mexico, Hector Herrera, inasemekana ni mmoja wa wachezaji kusajiliwa na Arsenal ili kujaza nafasi ya Aaron Ramsey ambaye anategemewa kuihama Arsenal.

Tetesi-Hector Herrera kumridhi Aaron Ramsey

Mtandao wa ESPN umeandika ya kwamba viongozi wa Arsenal wanampango wa kuongea na mchezaji huyo ili waweze kumsajili bure kwani naye yupo katika mwaka wa mwisho katika mkataba wake na timu yake ya sasa ya Porto ya Ureno.

Herrera mabaye anaweza kucheza kama kiungo wa kati , kiungo mkabaji au beki wa kati amekuwa ni mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa timu ya taifa ya Mexico na Porto kwa muda mrefu sasa.

Taarfia hizo zimekuwa zsiku chache baada ya kuibuka kwa tetesi za kwamba Arsenal tayari imekubaliana na kiungo mshambuliaji wa  Atlanta, Miguel Almiron.

 

Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Miguel Almiron

Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa timu ya Atlanta, Miguel Almiron, hii ni kwa mujibu wa rais wa timu hiyo Darren Eales.

Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Miguel Almiron

Miguel Almiron kutua mwezi wa kwanza

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Paraguay amekuwa akicheza vizuri katika ligi kuu ya Marekani maarufu kama MLS, ambapo kiungo huyo mshambuliaji amefunga magoli 10 na kutoa asisti 12 katika michezo 32 aliyoichezea timu hiyo.

Eales alikiambia kituo cha luninga cha FOX DEPORTES ya kwamba kila kitu kimekamilika na mchezaji huyo ateenda balani ulaya kuichezea timu ya Arsenal ya Uingeleza katika dirisha dogo ya usajili la mwezi wa kwanza.

Taarifa hiyo inaendelea kuhabalisha ya kwamba Arsenal imekubali kulipa ada ya uhamisho ya euro milioni 13 ili kupata huduma za kiungo huyo.

Kwa mujibu ya rais huyo Atlanta tayari wamekubaliana na kiungo wa River Plate ya Argentina,Gonzalo Martinez  ili achukue nafasi ya Almiron.

Kwa mujibu wa gazeti la ABC DEPORTES la nchini Paraguay, Arsenal iliwahi kumtaka mchezaji huyo misimu michache iliyopita lakini walishindwa kufikia makubaliano.

Almiron ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ni nina uhakika wa kwamba kama akitua mwezi wa kwanza atakuwa msaada mkubwa kwa timu.

Muangalia hapo chini kwenye video.

Reiss Nelson ajiunga na Hoffenheim kwa mkopo wa mwaka mmoja

Kinda wa Arsenal, Reiss Nelson amejiunga  na timu ya Hoffenheim ya Ujerumani kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo anahamia katika timu hiyo ya Ujerumani baada ya kusaini mkataba wa muda mrefu kuendelea kuichezea Arsenal.

Reiss Nelson ajiunga na Hoffenheim kwa mkopo wa mwaka mmoja

Nelson mwenye umri wa miaka 18 pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uingeleza kwa vijana wenye umri wa miaka 21 ameshaichezea timu ya wakubwa ya Arsenal katika michezo 16 tangu msimu uliopita.

Akiwa katika timu hiyo ya Hoffenheim, Nelson atavaa jezi namba tisa na atakuwa akijifunza kutoka kwa moja ya makocha bora kabisa kwa sasa Julian Nagelsmann.

Mara baada ya kukamilika kwa uhamisho huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema  “Reiss ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu.Uhamisho wake kwenda Hoffenheim utampa nafasi ya kuchezaa mara kwa mara katika timu yenye ushindani mkubwa.”

 

Tetesi za usajili-Reiss Nelson mbioni kujiunga na Hoffenheim

Kiungo kinda wa Arsenal, Reiss Nelson yupo mbioni kujiunga na timu ya Hoffenheim inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani.

Tetesi za usajili-Reiss Nelson mbioni kujiunga na Hoffenheim

Wakati dirisha la usajili limeshafungwa nchini Uingeleza,Timu za ujerumani bado zina uweza wa kuuza na kununua wachezaji na hivyo timu hiyo imeona ni bora ikiongeze nguvu kikosi chake kwa kumsajili kinda huyo wa Arsenal.

Reiss Nelson anaingia katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake wa awali na inasemekana yupo tayari kuondoka ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo mwaka jana alipata nafasi kubwa ya kucheza katika kombe la Europa League na kombe la Carabao na pia mwishoni alipata nafasi ya kucheza katika ligi kuu lakini kwa msimu huu bado hajapata nafasi yeyote.

Na pia ikichukuliwa ya kwamba rafiki wake wa karibu Sancho ambaye aliikacha Manchester City na kujiuna na Dortmund na sasa anacheza mara kwa mara, na yeye ataona ni bora aende Ujerumani akajaribu bahati yake.

Ni jambo la kusubiri kuona ya kwamba kama Arsenal watajaribu kumshawishi abaki au watamuachia.

#COYG

 

Joel Campbell ajiunga na Frosinone

Hatimaye mchezaji Joel Campbell ameondoka Arsenal na kujiunga na timu ya seria A ya Frosinone, Arsenal walitangaza mapema leo.

Joel Campbell ajiunga na Frosinone

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani alijiunga na Arsenal akitokea Deportivo Saprissa ya nchini kwao Costa Rica, mwezi wa nane mwaka 2011 na ameichezea katika mechi 40 katika kipindi hicho.

Joel Campbell alizichezea timu nyingi kwa mkopo kama Lorient, Olympiacos, Vilarreal, Sporting Lisbon na aliichezea timu ya Real Betis, kwa mara mbili, mara ya mwisho ilikuwa katika msimu wa 2017/18 .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Costa Rica, ana miaka 26 na tayari ameishaichezea timu yake ya taifa katika michezo 79 na kufanikiwa kuifungia magoli 15. Katika kombe la dunia la mwaka huu lililofanyika nchini Russia aliichezea mara mbili.
Kila la heri Joel Campbell.

Krystian Bielik ajiunga na Charlton kwa mkopo

Mchezaji wa Arsenal, Krystian Bielik  amejiunga na  Charlton Athletic inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Uingelekza kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Krystian Bielik ajiunga na Charlton kwa mkopo

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alijunga na Arsenal akitokea timu ya Legia Warsaw mwezi wa kwanza mwaka 2015 na aliichezea timu ya wakubwa ya Arsenal mwaka huo huo.

Mchezaji huyo pia alienda kwa mkopo katika timu ya Birmingham City msimu uliopita ambapo alicheza michezo 10.

Baadaye alijiunga na Walsall kwa mkopo katika dirisha la usajili kwa ajili ya msimu wa pili wa lakini alipata majeraha na hivyo kulazimika kurudi Arsenal kwa matibabu zaidi.

Krystian ni mchezaji wa kimataifa wa  Poland ambapo ameiwakirisha nchi yake katika michuano mbali mbali inayovahuse vijana wenye chini ya umri wa miaka 19.

Katika taarifa iliyotolewa na tovuti rasmi ya Arsenal ilimtakia kila la heri mchezaji huyo.

Wachezaji waliobaki Arsenal baada ya Dirisha la usajili kufungwa

Jana dirisha la usajili kwa timu za kiingeleza lilifungwa rasmi,na kama kawaida Arsenal ilikuwa inahangaika kusajili baadhi ya wachezaji na pia kuuza baadhi ya wachezaji.

Wachezaji waliobaki Arsenal baada ya Dirisha la usajili kufungwa

Kwa jana mchezaji pekee wa Arsenal aliyefanikiwa kuhama ni Lucas Pérez, ambaye alihamia West ham,Kuondoka kwa mchezaji huyo kulifanya idadi ya wachezaji wasio wazawa kufikia 17, kiasi ambacho kisheria ndicho kinachotakiwa.

Mchezaji mzawa ni yule mchezaji ambaye amecheza katika timu iliyochini ya chama cha soka cha Uingeleza au Wales kwa miezi 36 kabla ya kufikisha umri wa miaka 21.

Timu zinaruhusiwa kutumia idadi yeyote ya wachezaji wasiozidi miaka 21 na wachezaji wasio wazawa wenye umri wa zaidi ya miaka 21 wanatakiwa wasizidi 17.

Baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili  ifuatayo ni orodha ya wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 21  waliobaki Arsenal.

Jina Nafasi Mzawa       Zaidi ya miaka 21
1 Aaron Ramsey Kiungo Ndiyo Ndiyo
2 Alex Iwobi Kiungo Mshambuliaji Ndiyo Ndiyo
3 *Carl Jenkinson Beki wa Kulia Ndiyo Ndiyo
4 Cohen Bramall Beki wa kushoto Ndiyo Ndiyo
5 Danny Welbeck Mshambuliaji Ndiyo Ndiyo
6 Deyan Iliev Golikipa Ndiyo Ndiyo
7 Emiliano Martinez Golikipa Ndiyo Ndiyo
8 Hector Bellerin Beki wa kushoto Ndiyo Ndiyo
9 Rob Holding Beki wa kati Ndiyo Ndiyo
1 Andre Lacazette Mshambuliaji Hapana Ndiyo
2 Bernd Leno Golikipa Hapana Ndiyo
3 *David Ospina Golikipa Hapana Ndiyo
4 Granit Xhaka Kiungo wa kati Hapana Ndiyo
5 Henrikh Mkhitarian Kiungo mshambuliaji Hapana Ndiyo
6 *Joel Campbell Mshambuliaji Hapana Ndiyo
7 Laurent Koscielny Beki wa kati Hapana Ndiyo
8 Lucas Torreira Kiungo mkabaji Hapana Ndiyo
9 Mesut Özil Kiungo Mshambuliaji Hapana Ndiyo
10 Mohamed Elneny Kiungo wa kati Hapana Ndiyo
11 Nacho Monreal Beki wa kushoto Hapana Ndiyo
12 Petr Cech Golikipa Hapana Ndiyo
13 Pierre-Emerick Aubameyang Mshambuliaji Hapana Ndiyo
14 Sead Kolasinac Beki wa Kushoto Hapana Ndiyo
15 Shkodran Mustafi Beki wa kati Hapana Ndiyo
16 Sokratis Papastathopoulos Beki wa kati Hapana Ndiyo
17 Stephan Lichtsteiner Beki wa kulia Hapana Ndiyo

Ukiangalia vizuri kuna wachezaji 17 wenye umri wa zaidi ya miaka 21, kocha mkuu wa Arsenal alisema ya kwamba wachezaji Carl Jenkinson, David Ospina na Joel Campbell wanaweza kuondoka kabla ya dirisha la usajili la Ulaya halijafungwa.(dirisha la usajili la ulaya linafungwa tarehe 31 ya mwezi huu) Hapo utaona ya kwamba bado kuna nafasi ya kusajili wachezaji wasio wazawa na wenye umri wa miaka 21.

Kuongeza kwa orodha hiyo, kuna wachezaji ambao wana umri wa chini ya miaka 21

Jina Nafasi Atakuwa mchezaji mzawa akifikisha miaka zaidi ya 21
1 Ainsley Maitland-Niles Kiungo/Beki wa kushoto Ndiyo
2 Edward Nketiah Mshambuliaji Ndiyo
3 Emile Smith-Rowe Kiungo mshambuliaji Ndiyo
4 Joe Willock Kiungo wa kati Ndiyo
5 Joshua DaSilva Mshambuliaji Ndiyo
6 Reiss Nelson Kiungo mshambuliaji Ndiyo
7 Konstantinos Mavopranos Beki wa kati Hapana
8 Matteo Guendouzi Kiungo mkabaji Hapana

Hiyo ni orodha ya wachezaji ambao watakua katika kikosi cha kwanza, lakini ikumbukwe ya kwamba wachezaji wote chini ya umri wa miaka 21 wanaruhusiwa kucheza katika timu ya wakubwa bila hata kuwa katika orodha ya awali.

Ifuatayo ni Orodha ya Wachezaji wapya

Waliojiunga na Arsenal: Jumla 5

 • Lucas Torreira Sampdoria, £26.5m
 • Bernd Leno Leverkusen, £19.2m
 • Sokratis Papastathopoulos Dortmund, £17.7m
 • Matteo Guendouzi Lorient, £8m
 • Stephan Lichtsteiner Juventus,bure.

Walioondoka: Jumla  10

 • Lucas Pérez West Ham, £4m
 • Jeff Reiné-Adelaïde Angers, £2.7m
 • Chuba Akpom PAOK, £900,000
 • João Virginia Everton, Haijuikani
 • Jack WilshereWest Ham, Bure
 • Santi Cazorla Villarreal, Bure
 • Hugo Keto Brighton,Bure
 • Calum Chambers Fulham, Mkopo
 • Takuma Asano Hannover, Mkopo.
 • Per Metersacker , Amestaafu

Tofauti kati ya pesa ya kunununa na kuuza wachezaji: £63.8m

Hicho ni kikosi kamili cha Arsenal baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, maoni yako kuhusu nafasi ya kikosi hiki katika msimu mpya wa ligi?

Tetesi-Barcelona wanataka kubadilishana Dembele na Aaron Ramsey

Barcelona wapo tayari kumuachia Ousmane Dembele ajiunge na Arsenal kwa sharti moja tu, Arsenal iwape Aaron Ramsey.

Tetesi-Barcelona wanataka kubadilishana Dembele na Aaron Ramsey

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amehusishwa na kuhamia Arsenal mara nyingi katika dirisha hili la usajili na kuna tetesi za kwamba Barcelona hawamtaki hasa baada ya kumsajili Malcom siku chache zilizopita.

Gazeti la The Sun  linadai ya kwamba Arsenal wanaweza kulazimishwa kumuachia Ramsey kama wanataka kumpata kinda huyo kutoka Barcelona.

Mpaka sasa Arsenal imeshasajili wachezaji watano na kuna habari za kwamba wana mpango wa kusajili mchezaji mmoja ama wawili ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji hasa upande wa mawinga.

Arsenal itabidi ifanye kazi ya ziada ili kumsajili Dembele ambaye kwa sasa ni mchezaji wa tatu kwa kununuliwa kwa bei kubwa duniani, kwani Barcelona walilipa pesa nyingi ili kumsajili mwaka mmoja uliopita na watataka kurudisha sehemu kubwa ya pesa hizo.

Dembele,ambaye alisajiliwa kwenda kwa wakali hao wanaotumia uwanja wa  Nou Camp  kwa dau la paundi milioni 134 ameshindwa kuwika akiwa na timu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifanikiwa kufunga magoli matatu tu katika ligi kuu ya Hispania msimu ulioisha.

Na Barcelona wapo tayari kumuuza, lakini wanamtaka Aaron Ramsey kama sehemu ya usajili huo,Ramsey anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na iwapo asiposaini sasa anaweza kuondoka bure mwakani.

Je mashabiki wa Arsenal, mnaonaje tetesi hizi? wabadilishane au kila mtu abakie na wake?