Tetesi za usajili Arsenal-Yann Sommer-Kingsley Coman-Ospina na Akpom

Wakati Arsenal kesho ikitegemewa kusafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki,Vyombo vingi vya habari vimeendelea kuihusisha Arsenal na usajili wa wachezaji mbalimbali.Katika tetesi za usajili wa Arsenal leo tunakuletea taarifa kuhusu Yann Sommer,Kingsley Coman, David Ospina na Chuba Akpom.

Yann Sommer

Yann Sommer

Yann Sommer yupo katika mazungumzo na Arsenal

Gazeti la Marca linaandika ya kwamba Arsenal wapo katika mazungumzo ya kumsajili golikipa kutoka Uswisi,Yann Sommer.

Habari hizo zinakuja huku tayari Arsenal ikiwa imeshamsajili Bernd Leno kwa dau la paundi milioni 19, huku ikiwa na makipa wengine watatu.Martinez,Ospina na Cech.

Sioni Arsenal ikisajili kipa mwingine labda Ospina na Cech wauzwe, pia Barcelona inasemekana inataka kumsajili golikipa huyo wa kimataifa wa Uswisi.

Kingsley Coman

Inasemekana ya kwamba Arsenal ipo sokoni kutafuta winga mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kukokota mpira,na jina la Kingsley Coman, linaendelea kutajwa.Vyombo vingi vya habari vinadai ya kwamba tayari Arsenal imetuma ofa mbili za kumsajili mchezaji huyo lakini zote zilikataliwa na timu yake ya Bayern Munich.

David Ospina

Inavyoonekana ni kwamba siku za David Ospina kuwa golikipa wa Arsenal zimefikia ukingoni,magazeti mengi ya kiingeleza yanahabarisha ya kwamba anakaribia kutua Besiktas, huku pia kukiwa na taarifa ya kwamba timu za Fulham na Tigres ya Mexico zinamuwania golikipa huyo.

Chuba Akpom

Mshambuliaji wa Arsenal, Chuba Akpom yupo karibu na kujiunga na timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la uhamisho linalokadiliwa kufikia paundi milioni 2.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Nigeria ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal, na hayupo katika kikosi cha Arsenal kinachosafiri kesho kuelekea Singapore.

Baada ya kuchezea timu nyingi kwa mkopo inaonekana kwa sasa Arsenal wanampango wa kuachana naye moja kwa moja.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizopata kwa siku ya leo, zingine tukijaaliwa.

Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N’Zonzi na Golovin

Arsenal inaendelea na kujiandaa na msimu ujao wa ligi ambapo jana ilicheza na timu ya Crawley town na kuifunga goli 9-0,na wiki iliyopita kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery, alisema ya kwamba kikosi chake kimekamilika.

Lakini kutokana na kuwa katika kipindi cha usajili bado Arsenal inahisishwa na kusajili wachezaji wapya.Katika tetesi za usajili leo tunakuletea habari zilizoandikwa na magazeti kuhusu wachezaji Kingsley Coman ,N’Zonzi na Golovin ambao wamehusishwa na usajili wa Arsenal.

Kingsley Coman

Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N'Zonzi na Golovin

Kingsley Coman

Arsenal imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa mchezaji Kingsley Coman kutoka Bayern Munich na kulikuwa na tetesi ya kwamba Arsenal walituma ofa ya paundi milioni 50 ambayo ilikataliwa na wakarudi tena na ofa ya paundi milioni 55 ambayo ilikataliwa pia.

Sababu kubwa ya Bayern Munich kuzikataa ofa za Arsenal ni kuwa wanamuona mchezaji huyo kama sehemu kubwa ya safu yake ya ushambuliaji hasa ukichukulia wachezaji kama Frank Ribery umri umeshawatupa mkono na Kingsley Coman atachukua nafasi yake siku si nyingi.

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Kituo cha Sky Sports kimeandika katika tovuti yake ya kwamba Arsenal wanaendelea mazungumzo na Sevilla kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji Steven N’Zonzi. Mchezaji huyo ambaye amewahi kufanya kazi na Unai Emery anaweza kucheza kama kiungo mkabaji na anaweza kuja kuongeza nguvu katika kiungo cha Arsenal.

Aleksandr Golovin

Arsenal ilikuwa inamtaka Aleksandr Golovin, na Arsenal inaelekea kumkosa mchezaji huyo ambaye ameamua kujiunga na Chelsea.

Inasemekana ya kwamba mchezaji huyo alikuwa tayari kujiunga na Arsenal lakini baada ya Arsene Wenger kuondoka Arsenal ameamua kubadili uamuzi wake kwani alikuwa ni shabiki mkubwa wa kocha Wenger.

Hizo ndizo tetesi za usajili za Arsenal tulizozipata kwa siku ya leo,usisahau kushare na mashabiki wengine wa Arsenal.

Tetesi za usajili-Chelsea wanamtaka Petr Cech

Kuna tetesi za kwamba Chelsea wana mpango wa kumsajili mchezaji wao wa zamani na golikipa wa sasa wa Arsenal Petr Cech.

Tetesi za usajili-Chelsea wanamtaka Petr Cech

Watoto hao wa darajani wapo sokoni kutafuta golikipa mpya baada ya kuwa na taarifa ya kwamba golikipa wao wa sasa Thibaut Courtois, yupo njiani kujiunga na wabingwa wa Ulaya Real Madrid.

Katika taarifa zilizoandikwa katika ukurasa rasmi wa kituo cha luninga cha Sky Sports inaelezea ya kwamba kocha mpya wa Chelsea Maurizio Sarri anafikiria uwezekano wa kumrudisha Cech darajani ambapo aliichezea Chelsea kwa miaka 11 kutoka mwaka 2004  hadi mwaka 2015.

Chelsea walikuwa wanamfukuzia golikipa wa Roma Alisson Becker, lakini taarifa za kuaminika ni kwamba Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili mlinda mlango huyo na hivyo kuwaacha Chelsea wakitafuta golikipa mwingine.

Cech ambaye alifanya makosa mengi yaliyosababisha magoli katika msimu uliopita ana wakati mgumu wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal baada ya wakali hao wa London kunyakua Bernd Leno ambaye atakuwa golikipa namba moja.

Na kwa hali inayoonesha Arsenal inaweza kuamua kuachana wa magolikipa wote wawili (Ospina na Cech ) na kuwaacha Damien Martinez na Leno wakichuana kugombea nafasi katika kikosi cha kwanza na mmoja wa makipa wa timu ya chini ya miaka 23 akiwa kama kipa wa tatu.

Je unazionaje tetesi hizi? Arsenal wauze Cech ama abaki kwa sababu ana uzoefu mkubwa kwenye ligi.Tupia maoni yako hapa chini.

Tetesi za usajili Arsenal-Andre Gomes-Dembele na Pavon

Wakati Arsenal ikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya,magazeti mengi yameendelea kuihusisha na usajili wa wachezaji mbali mbali, leo tunakuletea tetesi za usajili zinazowahusu wachezaji Andre Gomes,Dembele na Pavon.

Andre Gomes

Arsenal imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Ureno,Andre Gomez.Katika taarifa zilizoandikwa na vyombo mbali mbali vya habari mchezaji huyo amepania kuachana na timu hiyo ya Hispania kutokana na kukosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mtandao wa Paris United umeandika ya kwamba Arsenal wameshawasiliana na mchezaji huyo na Barcelona wapo tayari kumuachia mchezaji huyo.

Cristian Pavon

Kocha wa Arsenal,Unai Emery ameambiwa kiasi cha pesa ambacho anatakiwa kulipa kama anamtaka mchezaji Cristian Pavon kutoka Boca Juniors.

Gazeti la Daily Mirror linaandika ya kwamba mchezaji huyo amesaini mkataba mpya na Boca na kuna kipengele kinachomruhusu mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 44.

Dembele awapagawisha mashabiki wa Arsenal

Tetesi za usajili Arsenal-Andre Gomes-Dembele na Pavon

Ousmane Dembele

Kwa muda sasa Arsenal imekuwa ikihusishwa na usajili wa Ousmane Dembele kutoka Barcelona,mchezaji huyo ambaye hakucheza vizuri msimu uliopita alikuwa ni sehemu ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyoshinda kombe la Dunia jana.

Kilichotokea ni kwamba mchezaji huyo alikoment katika picha ya beki mpya wa Arsenal Sokratis ambapo alisema ‘big papa’.

Kitendo hicho kimewafanya mashabiki wengi wa Arsenal waamini ya kwamba mchezaji huyo yupo njiani kutua Arsenal.

Pia wiki iliyopita Aubamayang aliweka picha ya Dembele katika mtandao wa instagram hali ambayo pia iliibua tetesi za kwamba huenda mchezaji huyo akatua Arsenal.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizozipata kwa leo, zingine kesho tukijaaliwa.

Arsenal yakamilisha usajili wa Sam Greenwood.

Timu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji kinda kutoka chuo cha soka cha Sunderland,Sam Greenwood.

Arsenal yakamilisha usajili wa Sam Greenwood.

Sam Greenwood (pichani) akisaini mkataba wa kuichezea Arsenal

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na tovuti ya timu ya Sunderland, ni kwamba mchezaji huyo alikataa mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo na kuomba kujiunga na Arsenal.

Greenwood, mwenye umri wa miaka 16, alizivutia timu nyingi kubwa za Uingeleza zikiwemo Machester United na Liverpool, lakini Arsenal wameshinda vita hivyo na kufanikiwa kumnasa mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa cha kucheza soka.

“Leo naanza ukurasa mpya katika maisha yangu baada ya kusaini kuichezea Arsenal, nina hamu kubwa ya kupambana na kuichezea timu hii,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Mchezaji huyo hategemewi kuwa katika kikosi cha kwanza wala kusafili kwenda Singapole wiki ijayo, atajiunga moja kwa moja na chuo cha soka cha Arsenal, ambapo atakuwa kwenye kikosi cha vijana wenye umri wa miaka 18.

Karibu Arsenal, Sam Greenwood.

Rasmi-Arsenal yakamilisha usajili wa Matteo Guendouzi

Arsenal imeendelea na juhudi zake za kujipanga upya baada ya kumalilisha usajili wake wa tano msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa kinda Matteo Guendouzi.

Rasmi-Arsenal yakamilisha usajili wa Matteo Guendouzi

Matteo Guendouzi ambaye ni kiungo mfaransa mwenye umri wa miaka 19 anajiunga na Arsenal akitokea Lorient inayoshiriki katika ligi daraja la pili ya ufaransa.

Kinda huyo alianza maisha yake ya soka katika timu ya PSG kabla ya kutimka na kujiunga na chuo cha soka cha Lorient mwaka 2014.

Matteo aliichezea timu ya Lorient kwa mara ya kwanza mwaka 2016 akiwa na miaka 17 tu, ambapo baadaye alicheza michezo 30 katika msimu huo.

Mchezaji huyo tayari ameshaiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa kwa vijana wenye umri wa miaka 18,19 na 20.

Baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Tumefurahi sana ya kwamba Matteo anajiunga na Arsenal,Ni mchezaji mwenye umri mdogo lakini mwenye kipaji cha hali ya juu.Anaweza kuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye na tayari ana uzoefu wa kucheza michezo ya kikosi cha kwanza alioupata msimu uliopita akiwa na Lorient.Anataka kujifunza na atakuwa mchezaji wa muhimu katika kikosi cha kwanza”

Matteo atavaa jezi namba 29 akiwa na Arsenal.

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

#TimeForTorreira-Arsenal yakamilisha usajili wa Lucas Torreira

Timu ya Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji kutoka Uruguay Lucas Torreira.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alishiriki katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia ambapo alicheza vizuri kiasi cha kuvutia watu wengi.

 #TimeForTorreira-Arsenal yakamilisha usajili wa Lucas Torreira

Baada ya kukamilika kwa usajili huo Kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Lucas Torreira ni mchezaji kijana mwenye kipaji cha hali ya juu.Ni kiungo mwenye ubora wa hali ya juu, nilimwangalia akiwa akiichezea timu ya Sampdoria katika misimu miwili na pia wote tuliona alivyofanya vizuri akiwa na Uruguay akatika kombe la dunia.Ni mchezaji mwenye umri mdogo lakini akiwa na uzoefu wa kutosha ambaye anataka kuwa bora zaidi.Tunamkaribisha Lucas katika timu, tunaamini atajiunga na kambi ya kujiandaa kwa msimu ujao muda si mrefu.”

Lucas Torreira alianza maisha ya soka akiwa na timu ya I.A 18 Julio na baadaye Montevideo Wanderers zote za nchini kwao Uruguay,Lucas alihamia Italia mwaka 2013 ambapo alijiunga na timu ya Pescara,ambapo aliichezea kwa mara ya kwanza mwaka 2015 mwezi wa tano.

Torreira atavaa jezi namba 11 akiwa katika timu ya Arsenal, Jezi hiyo imeachwa wazi na Mesut Özil ambaye amechukua jezi namba 10 iliyoachwa wazi na Jack Wilshere aliyejiunga na West Hama hapo jana.

Karibu Arsenal  Torreira.

Je mashabiki wa Arsenal mnauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapo chini.

Tetesi za usajili-Arsenal wakubaliana na FC Lorient kuhusu uhamisho wa Matteo Guendouzi

Arsenal imefikia makubaliano na timu ya Ligue 2 FC Lorient kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Matteo Guendouzi.

Matteo Guendouzi

Matteo Guendouzi pichani anategemewa kuwa mchezaji wa Arsenal kesho jumatatu

Arsenal imekubali kuilipa timu hiyo ya Ufaransa ada yenye dhamani ya Euro milioni 8 na bonasi nyingine ambazo zitategemea na mafanikio yake katika timu hiyo ya London.

Kiungo huyo kinda mwenye umri wa miaka 19 anatazamiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ili kuvaa jezi nyekundu na nyeupe zinazotumiwa na Arsenal.

Mchezaji huyo ambaye ana asili ya Morroco, ameishaiwakilisha timu ya taifa ya Ufarasa,Les Bleus, katika umri wa miaka 18,19 na 20 .

Alitokea katika chuo cha soka cha PSG , alihamia Lorient mwaka 2014, kabla ya kusaini mkataba na timu hiyo mwaka 2016,ambapo alivutia wengi na kufanikiwa kuwa mchezaji aliyeshinda asilimia kubwa ya mipira ya juu.

Katika msimu uliopita Guendouzi alicheza michezo 21, alianza katika michezo 19.Akiwa amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa,Lorient wameona bora wamuuze kwani timu nyingi zilianza kumnyemelea.

Loriente wamekua wakijaribu kumsainisha mkataba mpya lakini wameshindwa kwani timu hiyo ilishindwa kufikia mahitaji ya mchezaji huyo kwenye mshahara.

Na sasa Arsenal wameonesha nia ya kumsajili wakiwa tayari kumlipa mshahara anaouhitaji.

Kusajiliwa kwa Matteo Guendouzi hakumaanishi kufa kwa dili la kumsajili Torreira, kwani kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba tayari ameshafanyiwa vipimo, ilikuwa bado kusaini tu, muda huu pengine itakuwa tayari ameshasaini.

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

 

Tetesi za usajili Arsenal-Chuky Lozano na Hector Herrera wanatakiwa na Arsenal

Habari kutoka Mexico zinadai ya kwamba Arsenal ina mpango wa kuwasajili Chuky Lozano na Hector Herrera katika dirisha hili la usajili.

Kituo cha luninga cha ESPN Mexico jana jioni kilitoa taarifa ya kwamba wachezaji hao wawili wanatakiwa na timu ya Arsenal.

Chuky Lozano

Tetesi za usajili Arsenal-Chuky Lozano na  Hector Herrera wanatakiwa na Arsenal

Chuky Lozano

Hirving Lozano ambaye kwa hapa Mexico anajulina kama Chucky Lozano amekuwa akiwindwa na timu kubwa za Ulaya na katika taarifa hizo inasemekana Arsenal ni moja ya timu hizo, taarifa hiyo inaenda mbali zaidi na kusema ya kwamba tayari Arsenal wameshakutana na wawakilishi wa mchezaji huyo na wapo tayari kutoa dau la paundi milioni 35 ili kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea timu ya PSV ya Uholanzi.

Hector Herrera

Hector Herrera

Hector Herrera

Pia taarifa hizo zinaelezea ya kwamba Arsenal inataka kumsajili mchezaji wa kiungo wa Mexico Hector Herrera ambaye Mexico ni maarufu kama HH.

Herrera ambaye ni kiungo mkabaji kwa sasa anaichezea timu ya Porto ya Ureno,kwa mujibu wa taarifa hiyo usajili wa Hector Herrera utategemea sana na kukamilika kwa usajili wa mchezaji Lucas Torreira kutoka Sampdoria, kwani Herrera atasajiliwa tu iwapo kama Arsenal itamkosa Lucas Torreira.

Mimi binafsi ningependa Chuky Lozano achezee Arsenal kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mmoja ya wachezaji ambao ndani ya miaka 2 au 3 wanaweza kuwa bora kabisa duniani.

Torreira safarini kuelekea London

Mchezaji Lucas Torreira yupo safarini kuelekea London Uingeleza,Katika taarifa iliyoandikwa na mtandao  wa carasycaretas.com.uy wa nchini Uruguay  mchezaji huyo anatazamiwa kufanya vipimo Arsenal leo na baadaye kusaini mkataba wa  miaka mitano.

Torreira safarini kuelekea London

Lucas Torreira anaweza kusaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Arsenal

Taarifa zaidi tulizopata ni kwamba mchezaji huyo wa miaka 22 atafanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitano ndani ya London Colney leo ambapo akishamaliza atapanda ndege kuelekea nchini kwao Uruguay ambapo ataenda likizo kabla hajaanza rasmi kuitumikia Arsenal.

Hii taarifa inakuja baada ya jioni ya jana Torreira kuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Uruguay ambao hawakuwemo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaondoka Urusi asubuhi ya jumapili hii kurudi nchini kwao.

Lucas alicheza vizuri katika michuano ya kombe la dunia ambapo timu yake ilifungwa kwa jumla ya magoli 2-0 na kutolewa na ufaransa katika robo fainali ya michuano hiyo.

Tetesi za usajili Arsenal-Ousmane Dembele-Goncalo Guedes-Cristian Pavon na Mustafi

Wakati Arsenal wakiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya, kuna baadhi ya wachezaji wamehusishwa na kuhama ama kuhamia Arsenal.

Katika tetesi za usajili wa leo tunakuletea habari zinazowahusu wachezaji Ousmane Dembele,Goncalo Guedes,Cristian Pavon na Mustafi.

Ousmane Dembele

Tetesi za usajili Arsenal-Ousmane Dembele-Goncalo Guedes-Cristian Pavon na Mustafi

Gazeti za the Express limemuhusishwa mchezaji Barcelona Ousmane Dembele, na kuhamia Arsenal, katika taarifa hiyo inasemekana ya kwamba mchezaji huyo ana wasiwasi wa kwamba atakosa nafasi ya kucheza michezo mingi katika timu hiyo ya Hispania kutokana na kuwepo na ushindani mkubwa wa namba katika kikosi hicho.

Wakati huo huo gazeti la Manchester Evening limeandika ya kwamba Barcelona hawatakubali kumuuza mchezaji huyo kwani yupo katika mipango yao ya baadaye.

Goncalo Guedes

Goncalo Guedes anatakiwa na Arsenal

Goncalo Guedes anatakiwa na Arsenal

Gazeti la Experess pia linaandika ya kwama kocha mkuu wa Arsenal anamtaka mshambuliaji wa PSG Goncalo Guedes ambaye inasemekana ana dhamani ya paundi milioni 44.

Taarifa zilizoandikwa na vyombo vingine vya habari zinadai ya kwamba tayari Arsenal imewasilisha ombi rasmi la kumsajili mchezaji huyo lakini bado hawajapewa jibu.

Cristian Pavon

Kocha wa Arsenal, Unai Emery ana mpango wa kumfanya Cristian Pavon kuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Arsenal msimu huu.

Pavon ambaye alikuwa anatafutwa na Arsenal mwezi wa kwanza kuchukua nafasi ya Alexis wakati akihamia Manchester United, yupo kwenye mipango ya kocha Emery katika msimu huu.

Lakini timu anayoichezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22,Boca Juniors ya Argentina inasemekana hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo ingawa dau kubwa linaweza kusaidia kubadilisha msimamo wao.

Shkodran Mustafi

Shkodran Mustafi

Gazeti la Corriere dello Sport  linaandika ya kwamba Juventus inamtaka beki wa kati wa Arsenal Shkodran Mustafi.

Beki huyo ambaye hakucheza vizuri katika msimu uliopita na kufanya makosa mengi hali iliyomfanya kutemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani.

Kuwasili kwa Sokratis Papastathopoulos kunaweza kuwa mwisho wa mchezaji huyo kuvaa jezi za Arsenal kwani kuna taarifa za kwamba Arsenal walikuwa tayari kumuuza msimu ujao na watafanya hivyo msimu huu iwapo itapatikana timu iliyo tayari kumsajili.

Hizo ndizo tetesi tulizokuletea kwa leo.