Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Joel Lopez kutoka Barcelona

Mwandishi wa kiispania ,Gerard Romero amehabarisha ya kwamba Arsenal imekamilisha usajili wa kinda kutoka Barcelona Joel Lopez.

Tetesi-Arsenal yakamilisha usajili wa Joel Lopez kutoka Barcelona

Joel Lopez , mwenye umri wa miaka 16 ni beki wa kushoto na amekuwa akiichezea Barcelona tangu akiwa na miaka 7 na kwa siku za hivi karibuni amekuwa akisemwa ya kwamba ni mmoja ya vipaji bora kabisha vilivyopo katika chuo cha soka cha wakali hao kutoka Hispania, La Masia.

Pamoja ya kwamba viongozi wengi wa Barcelona wanamuona ni mmoja ya wachezaji wenye kipaji kikubwa kutoka La Masia, timu hiyo imeshindwa kumshawishi mchezaji huyo kusaini mkataba mpya.

Anaelekea Arsenal

Kutoka katika taarifa iliyotolewa na mwandishi Gerard Romero, inaonekana kitendo cha kushindwa kumshawishi kinda huyo kusaini mkataba mpya kinaweza kusababisha kumpoteza mchezaji huyo,kwani kuna taarifa kutoka mcheza wa leo ya kwamba leo asubuhi mchezaji huyo ameshawataarifu viongozi wa Barcelona ya kwamba ameshakubariana na Arsenal na atajiunga na timu hiyo katika majira haya ya Usajili.

Arsenal wamekuwa wakimfuatilia kinda huyo kwa muda mrefu na pia Liverpool walionesha nia ya kumtaka kinda huyo ila uwepo wa Raul Sanllehi katika timu ya Arsenal inasemekana ndiyo sababu ya dogo huyo kuichagua timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Iwapo Lopez atajiunga na Arsenal atakuwa amefuata nyota za wakali wengine kutoka La Masia waliofanya hivyo kama Cesc Fabregas, Hector Bellerin na Fran Merida.

Tetesi-Arsenal wakubaliana na Sampdoria kuhusu uhamisho wa Lucas Torreira

Arsneal wamekubali kulipa dau la paundi milioni 25 ili kumnasa kiungo wa Sampdoria Lucas Torreira,hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo kutoka Italia Gianluca Di Marzio.

Tetesi-Arsenal wakubaliana na Sampdoria kuhusu uhamisho wa Lucas Torreira

Di Marzio ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa habari ya kwamba kulikuwa na mazungumzo kati ya Arsenal na Sampdoria juu ya uwezeakano wa kumsajili kiungo huyo, lakini alieleza ya kwamba kulikuwa hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa.

Hii ilitokana na wakala wa mchezaji huyo kuweza vikwazo na hivyo kuomba muda zaidi wa kufikiria ambapo ilitarajiwa ya kwamba tarehe 15 ya mwezi huu ndipo angetoa jibu.

Baada ya habari hiyo kuvuja mtandao wa , SampNews24 umeandika ya kwamba Samppdoria tayari wameshakubali kumuachia mchezaji huyo na pia Arsenal wapo tayari kutoa dau la kuvunja mkataba wake, pia wanaelezea tatizo bado lipo kwa wakala ambaye bado hajaridhika.

Arsenal wana harakisha mpango huo ili mchezaji huyo Asaini kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.Torreira anaenda kwenye michuano hiyo akiwa na timu yake ya taifa ya Uruguay na tunajua ya kwamba iwapo atafanya vizuri katika michuano hiyo itaongeza ugumu wa kumpata mchezaji huyo kwani timu nyingi kubwa zitaanza kumtaka.

Inavyoonekana ni kwamba wakala wake anaweza kufanya uamuzi kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Torreira alikuwa na msimu mzuri katika timu yake ya Sampdoria.Alifunga magoli matano katika michezo 38 na amewavutia mno wakubwa pale Arsenal.

Mchezaji huyo ambaye ni kiungo mkabaji, ana uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi ya timu pinzani na pia huwa hana tatizo la kwenda uvunguni inapohitajika.

Anapenda kupiga mashuti ya mbali kama Granit Xhaka na pia huwa anafunga kutoka mbali.

Iwapo Arsenal watafanikiwa kukamilisha usajili wa Lucas Torreira,Socratis na kipa naamini msimu ujao timu inaweza kufanya vizuri sana.

L’Equipe: Arsenal imekamilisha usajili wa Sokratis Papastathopoulos

Jarida la michezo la kifaransa  L’Equipe, linadai ya kwamba Arsenal imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos.

L’Equipe: Arsenal imekamilisha usajili wa Sokratis Papastathopoulos

Sokratis, beki mzoefi aliyeichezea timu ya taifa ya Ugiriki michezo 79, amekuwa akiichezea Dortmund tangu asajiliwe na timu hiyo mwaka 2o13 akitokea kwa wakali wengine kutoka Bundesliga, Werder Bremen.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka 5 aliyokaa katika timu hiyo inayotumia uwanja wa Westfalenstadion,beki huyo kisiki alikuwa mhimili mkubwa wa timu hiyo na kumfanya kuwa mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho.Kuondoka kwa Mats Hummels katika majira ya kiangazi ya mwaka 2016 kulimfanua Socratis kuwa kiongozi wa uwanjani wa timu hiyo

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alicheza michezo 43 katika mashindano yote msimu uliopita, akifunga magoli matatu katika kipindi hicho.

Kutokana na Dortmund kuyumba sana ndani ya miezi 6 iliyopita, kiwango cha mchezaji huyo nacho kiliyumba pia hali iliyosababisha kutaka kuhama ili kubadilisha hali ya hewa.

Kama matokeo ya kuteteleka kwa kiwango chake uwanjani kulikuwa na tetesi ya kwamba mchezaji huyo ameamua kuihama timu hiyo huku Arsenal Manchester United wakitajwa kuongoza mbio za kuiwania saini yake.

Usajili wakamilika

Baba yake na Sokratis alisikika katika kituo kimoja cha redio nchini Ugiriki akisema ya kwamba mwanae ameshaini mkataba wa kuichezea Arsenal tangu jumanne iliyopita, bado hakuna taarifa ramsi kutoka upande wa Arsenal kudhibitisha usajili huo.

Lakini vyanzo vingi vilivyokaribu na Arsenal, na sasa kutoka gazeti la  L’Equipe ,tunaweza kusema ya kwamba Sokrais ameshasajili na atakuwa mchezaji wa Arsenal kwa msimu ujao.Ukiwa ni usajili wa pili baada ya beki wa kulia Stephan Lichtsteiner kudhibitishwa kuhamia Arsenal jumanne iliyopita.

Je Sokratis Papastathopoulos utakuwa ni usajili mzuri? tupia maoni yako hapa chini.

 

Tetesi, Arsenal yakamilisha usajili wa kinda la PSG Yacine Adli

Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery anaendelea na mipango yake ya kuijenga upya timu hiyo baada ya kuwepo na taarifa ya kwamba tayari ameshakamilisha usajili wa mchezaji mwingine kutoka PSG Yacine Adli.

Tetesi, Arsenal yakamilisha usajili wa kinda la PSG Yacine Adli

Baada ya jana kutangaza rasmi usajili wa beki wa kulia Stephan Lichtsteiner na kukiwa na tetesi za kwamba tayari usajili wa beki wa kati Socratis nao umekamilika,inaelekea kocha huyo ameamua kumchukua kinda huyo ili kuimalisha safu ya kiungo.

Katika taarifa iliyoandikwa na mitandao mingi na kuthibitishwa na mtandao wa goal.com. Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17.Ili kukamilisha usajili huo Arsenal imeilipa PSG fidia ya paundi  £223,000.

Inasemekana Yacine Adli alikataa mkataba mpya na PSG baada ya kushawishiwa na Emery na Mislitant ya kwamba ana nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri Arsenal kuliko akibaki Ufaransa.

Adli, amesaini mkataba wa miaka mitatu na iwapo atafanya vizuri ataongezewa miaka mingine miwili na kuufanya mkataba huo kuwa wa miaka mitano.

Mchezaji huo anayecheza kama kiungo mshambuliaji na pia kama winga wa kulia ameishazichezea timu za vijana za Ufaransa za umri wa mika 16, 17 na 18, ambapo amefunga magoli 13 katika michezo 23 aliyozichezea timu hizo za taifa.

Je unauonaje usajili wa dogo huyo tupia maoni yako hapa chini.

Arsenal yakamilisha usajili wa Stephan Lichtsteiner

Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji kutoka Juventus,Stephan Lichtsteiner. Mchezaji huyo ambaye alikuwa amemaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Italia anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Arsenal Unay Emery.

Arsenal yakamilisha usajili wa Stephan Lichtsteiner

Beki huyo wa kimataifa wa Uswisi anasajiliwa akiwa na uzoefu mkubwa kwani amekuwa nahodha wa nchi yake na pia ameshindwa ubingwa wa ligi kuu ya Italia mara saba katika miaka saba aliyoichezea timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye ni beki wa kulia mwenye uzoefu mkubwa  aliichezea Juventus katika michezo zaidi ya 250, pia ameichezea timu yake ya taifa katika michezo 99 pia amekuwa nahodha wa timu yake ya taifa tangu mwaka 2016.

Stephan Lichtsteiner ambaye atavaa jezi namba 12 katika kikosi cha Arsenal msimu ujao ni mtu wa kazi ambaye ataleta changamoto na uongozi katika timu hasa sehemu ya ulinzi ambayo ilionesha kuyumba sana katika msimu uliopita.

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery alisema “Stephan analeta uzoefu na uongozi katika timu yetu, ni aina ya mchezaji mwenye uwezo mkuwa na anajituma sana uwanjani,Stephan atatufanya tuwe bora nje na ndani ya uwanja ”.

Karibu katika chama la wana Stephan Lichtsteiner.

 

Tetesi za usajili Arsenal-Marouane Fellaini ahusishwa kuhamia Arsenal

Katika tetesi za usajili leo kuna taarifa ya kwamba Arsenal ina mpango wa kumsajili kiungo anayemaliza mkataba wake machester United, Marouane Fellaini.

Tetesi za usajili Arsenal-Marouane Fellaini ahusishwa kuhamia Arsenal

Katika taarifa iliyoandikwa katika mitandao tofauti na kuwaacha vinywa wazi mashabiki wengi wa Arsenal ni kwamba washika bunduki wa London wana mpango wa kumsajili Marouane Fellaini baada ya kukataa kusaini mkataba mpya na timu yake ya Manchester United.

Usajili wa mchezaji kama Fellaini haukutegemewa sana na watu wengi hasa ukizingatia ya kwamba Arsenal imezoea kucheza mpira wa pasi fupi na haraka tofauti na Fellaini ambaye hupenda kucheza mipira mirefu.

Kama ni kweli itakuwa ni dalili ya kwamba utawala mpya chini ya kocha Unay Emery una mpango wa kubadili mfumo wa uchezaji wa Arsenal.

Inaaminika ya kwamba bosi mpya wa Arsenal alikuwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji toka kipindi anaifundisha timu ya Paris Saint Germain, wawakilishi wa fellaini watakaa na maafisa wa Arsenal msimu huu na kujadili usajili huo.

Mimi binafsi sioni umuhimu wa kumsajili Marouane Fellaini, kwani umri unamtupa mkono na nafasi yake angechukua kiungo mwenye chini ya miaka 25 ili aweze kukaa kwenye timu kwa miaka mingi ijayo.

Je mashabiki wa Arsenal mnauonaje usajili wa manywele Fellaini? Unaona kuna kitu ataongeza kwenye timu au ni kujaza tu nafasi ambayo angeweza kuchukua mchezaji mwingine? tupia maoni yako hapa chini.

Tetesi za usajili Arsenal-Stephen N’Zonzi-Caglar Soyuncu-Corentin Tolisso-Ousmane Dembele

Dirisha la usajili likiwa limefunguliwa huku Arsenal ikiwa bado haijakamilisha usajili hata mmoja, wachezaji kadhaa wameendelea kuhusishwa na kusajiliwa Arsenal.

Katika tetesi za usajili wa  Arsenal subuhi ya leo nakuletea orodha ya wachezaji waouhusishwa na kuhamia Arsenal na mtazamo wangu kuhusu tetesi hizo.

Stephen N’Zonzi

Tetesi za usajili Arsenal-Stephen N’Zonzi-Caglar Soyuncu-Corentin Tolisso-Ousmane Dembele

Taarifa kutoka Hispania zinadai ya kwamba Arsenal ina mpango wa kumsajili kiungo mkabaji wa Sevila  Stephen N’Zonzi.

Mtandao wa Estadio Deportivo unaelezea ya kwamba kiungo huyo ana mpango wa kuihama timu hiyo na Arsenal imeonesha nia ya kumsajili.

N’Zonzi, ambaye alihusishwa na kuhamia Arsenal katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza inasemekana anaweza kuuzwa pwa paundi milioni 35.

Mtazamo wangu

N’Zonzi, ni kiungo mkabaji, na ninaamini Arsenal inahitaji kiungo mkabaji ambaye atacheza nyuma ya Ramsey na Ôzil, hivyo naamini kuna ukweli flani katika taarifa hizi.

Caglar Soyuncu

Inasemekana wawakilishi wa Arsenal walikuwepo uwanjani kumwangalia mchezaji huyo wakati Uturuki ilipocheza na Iran jumatatu iliyopita na pia walikuwepo ijumaa ambao Uturuki ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia.

Beki huyo wa kati alisema ya kwamba atajua nini cha kufanya akirudi Ujerumani baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Uturuki na Russia utakaofanyika tarehe 5 mwezi huu.

Arsenal ni moja ya timu kubwa kabisa Uingeleza na nafahamu ya kwamba wanataka kunisajili, baada ya kambi ya timu ya taifa tutakaa na kuongea, alisema mchezaji huyo wakati akiongea na vyomba vya habari.

Mtazamo wangu

Majeruhi ya Koscienly na kiwango kilichoyumba cha Mustafi ni sababu kubwa ya Arsenal kutafuta beki mpya wa kati, inasemekana ya kwamba timu yake ya  Freiburg inataka paundi milioni 35,naamini Arsenal itamsajili mchezaji huyo iwapo wajerumani hao wataamua kupunguza dau.

Corentin Tolisso

Baada ya kuondoka kwa Jack Wilshere na Santi Cazorla ni wazi kwamba Arsenal inahitaji kusajili kiungo wa kati.Mtandao wa CalcioInsider  unahabarisha ya kwamba kocha wa Arsenal Unay Emery ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo na mwenye umri wa miaka 23.

Corentin Tolisso

Mtazamo wangu

Tolisso ni mchezaji mzuri lakini sidhani ya kwamba Bayern Munich watakubali kumuachia kiungo huyo ambaye bado ni kijana mdogo, pia mchezaji huyo amekuwa na msimu mzuri uliopita sidhani kama atakubali kuhamia Arsenal kwa sasa.

Ousmane Dembele

Kuna tetesi za kwamba msaka vipaji mkuu wa Arsenal, Sven Mislintat, alifanya mazungumzo na Barcelona kuangalia uwezekano wa kumsajili kinda huyo wa kifaransaiwe kwa mkopo au usajili wa moja kwa moja.Pia taarifa hizo zinadai ya kwamba Mislintat amekuwa akifanya mazungumzo ya mara kwa mara na Dembele.

Mtazamo wangu

Iwapo Sven Mislintat na jopo zima la viongozi wa Arsenal watakamilisha usajili huu, utakuwa ni usajili mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Arsenal ndani ya miaka 10 iliyopita.

Dembele ni aina ya mchezaji ambaye kila shabiki wa Arsenal angependa tumsajili, dogo ana kipaji cha hali ya juu na sidhani kama Barcelona watakuwa wajinga na kumuachia.

Hizo ni tetesi za usaji wa Arsenal kwa siku ya leo, tukipata zingine hatutasita kukutaarifu, usisahau kuwajulisha na mashabiki wengine wa Arsenal juu ya ukurasa huu ili na wao wapata taarifa, Jumapili njema.