Chuba Akpom ajiunga na PAOK

Mshambuliaji mwenye asili ya Nigeria Chuba Akpom has  amejiunga na timu ya kigiriki PAOK Salonika katika mkataba wa kudumu.

Chuba Akpom ajiunga na  PAOK

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na chuo cha soka cha Arsenal akiwa na umri wa miaka 6.Aliichezea kwa mara ya kwanza timu ya vijana wenye umri wa miaka 18 akiwa na miaka 15, na alipewa mkataba wa kwanza akiwa na miaka 17.

Tangu mwaka 2013, Chuba Akpom ameshatolewa kwa mkopo katika timu kadhaa zikiwemo Brentford, Coventry City, Nottingham Forest, Hull City na hivi karibuni aliisaidia timu ya Brighton and Hove Albion kupanda hadi ligi kuu ya Uingeleza.

Mwezi wa kwanza mwaka huu,Chuba alijiunga na timu ya daraja la kwanza ya Ubelgiji ya Sint Truiden kwa mkopo.

Chuba Akpom aliichezea timu ya kwanza ya Arsenal katika michezo 12.

Kila la heri Chuba.

JOAO VIRGINIA ASHINDA EURO U19 NA URENO

Golikipa wa Arsenal,Joao Virginia alianza jana katika mchezo wa fainali za Uero 2018 kwa vijana wenye umri ya miaka 19 na kuisadia timu ya taifa ya Ureno kushinda kombe hilo.

JOAO VIRGINIA ASHINDA EURO  U19 NA URENO

Virginia ambaye amefanya vizuri katika timu za vijana za Arsenal kwa msimu uliopita,alianza michuano hiyo kama golikipa wa akiba,lakini alianza katika mchezo wa nusu fainali ambapo walishinda na kufanikiwa kuingia fainali.

Kinda huyo alianza katika mchezo wa fainali,mchezo huyo ulimalizika kwa sare na hivyo kwenda katika muda wa ziada ambapo wareno walifanikiwa kushinda.

Mwaka jana Uingeleza ilitwaa kombe hilo ambapo kinda mwingine wa Arsenal Josh Dasilva alitwaa medali ya ubingwa.

 

Lucas Torreira safarini kuelekea London

Kiungo mpya wa Arsenal, Lucas Torreira tayari ameshaondoka nyumbani kwao Uruguay,na kesho jumapili anatazamiwa kuwasili London, tayari kujiuna na kuanza mazoezi na Arsenal Jumatatu.

Mchezaji huyo ambaye alisajiliwa katika dirisha hili la usajili kutoka Sampdoria alikosa safari ya Singapore kwa mechi za kirafiki kutokana na kuwa likizo baada ya kushiriki katika mashindano ya kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Uruguay.

Lucas Torreira safarini kuelekea London

Lucas Torreira akiwa uwanja wa ndege tayari kukwea pia kuelekea London

Mchezaji huyo atajiunga na Xhaka na Stephan Lichtsteiner ambao nao walikosa safari ya Singapore kutokana na kucheza hatua ya mtoano ya kombe la Dunia.

Arsenal inategemewa jumapili hii kurudi London na jumatatu itaanza mazoezi tena kwa ajili ya kujiandaa kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Chelsea na Lazio itakayofanyika wiki ijayo.

Baada ya hapo timu itakuwa tayari imeiva kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na mashindano mengine.

Alex Iwobi akaribia kusaini mkataba mpya

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery amedhibitisha ya kwamba kiungo Alex Iwobi yupo mbioni kusaini mkataba mpya na wa muda mrefu.

Alex Iwobi  akaribia kusaini mkataba mpya

Alex Iwobi ambaye ni Mnigeria, ni zao la chuo cha soka cha Arsenal cha Hale End, na kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha Arsenal.

Inavyoonekana ni kwamba bosi mpya ameamua kuwapa nafasi vijana wa kiingeleza baada ya kuwapa mikataba mipya Calum Chambers na Ainsley Maitland-Niles.Hii itasaidia kuongeza idadi ya wachezaji wazawa katika kikosi cha Arsenal.

Iwobi ni mmoja ya wachezaji wa Arsenal wenye uwezo wa kucheza kama kiungo mshambuliaji na pia kama winga hivyo uwepo wake utasaidia sana kwani Arsenal haina mawinga wengi baada ya Theo Walcott,Alexis na Chamberlain kuondoka.

Pia kuna tetesi ya kwamba katika mkataba mpya mchezaji huyo atakuwa analipwa mara mbili zaidi ya mshahara anaolipwa sasa hivi.

Inategemewa ya kwamba mchezaji huyo atasaini mkataba huo mara baada ya timu kumaliza ziara ya mafunzo inayoendelea nchini Singapore.

Je unauonaje mpango huo wa kumpa Iwobi mkataba mpya? tupia maoni yako hapa chini.

Mesut Ozil ajiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani

Kiungo wa Arsenal,Mesut Özil, ametangaza kuachana na soka la kimataifa baada ya kutangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani.

Mesut Ozil ajiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani

Ozil ambaye alitupiwa gunia la misumari baada ya timu ya taifa ya Ujerumani kutolewa katika hatua ya makundi ameandika wakala mrefu unaoelezea matukio yaliyopekea kufikia uamuzi huo.

Katika wakala huo aliandika  “Kwa moyo mzito na baada ya kufikiria kwa muda mrefu baada ya matukio yaliyotokea hivi karibuni, sitaki kuendelea kuichezea nchi ya Ujerumani katika mechi za kimataifa baada ya kufanyiwa vitengo vya ubaguzi na kukosewa heshima.

“Nilikuwa navaa jezi ya ya timu ya taifa kwa furaha na heshima kubwa.

“Ilikuwa ni vigumu kufikia uamuzi huu kwa sababu mara zote nimejitolea kwa moyo wote kuwasaidia wachezaji wenzangu, makocha na watu wema wa Ujerumani.

“Lakini baada viongozi wa ngaji ya juu wa chama cha soka cha Ujerumani kutonitendea vyema, kudharau asili yangu ya Uturuki na kwa manufaa yao wenyewe na kuingiza siasa katika mambo ya soka nimeona ni bora nipumzike kwa sasa.

“Mimi ni mchezaji wa soka na sintokaa niangalie bila kujibu.

“Ubaguzi wa rangi haukubailiki”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameshaichezea Ujerumani katika michezo 92, ameifungia magoli 23 katika miaka 9 aliyoichezea timu hiyo.

Alikuwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichotwaa kombe la Dunia mwaka 2014, nchini Brazil.

Sisi kama mashabiki wa Arsenal tunaunga mkono uamuzi wa Mesut Özil,kwani tunaamini mwaka 2018 huwezi kumbagua mtu kwa ajili ya sehemu ya kuzaliwa,rangi ya ngozi yake au dini yake.

Tetesi-Arsenal kuwauza Danny Welbeck, David Ospina na wachezaji wengine

Wakati Arsenal ikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi na michezo mingine, kuna tetesi za kwamba Arsenal ina mpango wa kuwauza wachezaji kadhaa wakiwemo Danny Welbeck na David Ospina ili kupunguza ukubwa wa kikosi.

Tetesi-Arsenal kuwauza Danny Welbeck, David Ospina na wachezaji wengine

Mpaka sasa Arsenal ilikuwa imeelekeza nguvu zake katika kusajili wachezaji wapya na tayari imeshatumia paundi milioni 70 ili kupata saini za wachezaji Bernd LenoSokratis PapastathopoulosLucas TorreiraStephan Lichtsteiner na Matteo Guendouzi.

Sasa Arsenal imehamishia nguvu zake katika kuwauza wachezaji ili kupunguza ukubwa wa kikosi na pia kupata pesa kwa ajili ya mishahara na usajili wa wachezaji wapya.

Mtandao wa The Telegraph unahabarisha ya kwamba mshambuliaji Danny Welbeck na kipa namba tatu David Ospina ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kuondoka Arsenal katika dirisha hili la usajili.

Wachezaji hao inasemekana hawapo kwenye mipango ya kocha Unai Emery, pia wachezaji kama Lucas Perez, Carl Jenkinson,Chuba Akpom na Joel Campbell wanaweza kuuzwa ili kutengeneza pesa za usajili wa wachezaji wapya.

Welbeck anaingia katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake na Arsenal na Ospina kwa sasa ni chaguo la tatu baada ya Leo na Petr Cech.

Je ungependa mchezaji gani aondoke na nani abaki? tupia maoni yako hapa chini.

Mesut Özil apewa jezi namba 10

Rasmi Mesut Ozil amechukua jezi namba 10 kuanzia msimu ujao wa ligi.

Kiungo huyo wa kijerumani amechukua namba hiyo baada ya kuachwa wazi wa Jack Wilshere ambaye ameondoka Arsenal mwaka huu baada ya kuisha kwa mkataba wake.

Mesut Özil apewa jezi namba 10

Özil ambaye amekuwa mchezaji wa kutumainiwa wa Arsenal tangu ahamie kutoka Real Madrid mwaka 2013, ambapo tayari ameshaichezea timu katika michezo karibu na 200.

Katika kipindi hicho mchezaji huyo anayecheza kama kiungo mshambuliaji amefunga magoli 37 na kusaidia upatikanaji wa mengine 71, akiisaidia Arsenal kumaliza ukame wa makombe baada ya kushinda makombe matatu ya kombe la FA na ngao tatu za jamii katika kipindi hicho.

Katika taarifa rasmi ya Arsenal, mashabiki wote walionunua jezi zenye jina la mchezaji huyo zenye namba yake ya zamani 11 watatumiwa jezi mpya zenye namba 10 mgongoni bure.

Özil pia alikuwa kwenye kikosi cha Ujerumani kilichofanya vibaya katika kombe la Dunia linaloendelea nchini Urusi ambapo walitolewa katika hatua ya makundi na Özil kubeba gunia la lawama.

Bado haijajulikana mfumo mpya atakaotumia mwalimu Unay Emery na nafasi ambayo Özil atacheza, kwani alikuwa ni mchezaji muhimu sana katika kipindi cha kocha Arsene Wenger.

Baada ya kupewa namba hiyo mpya Özil alionesha kufurahia kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya kuandika ya kwamba kwake namba 10 ni zaidi ya namba kwani ina maana kubwa sana kwake.

Özil alisaini mkataba mpya mwezi wa kwanza mwaka huu na utamfanya awe mchezaji wa Arsenal hadi mwaka 2021.

 

Wachezaji watatu wa Arsenal kugombea GOLDEN BOY AWARD

Wachezaji watatu wa Arsenal wametajwa katika orodha ya wachezaji watakaogombe Golden Boy Award.Wachezaji hao ni Reiss Nelson, Stephy Mavididi na Jeff Reine-Adelaide ambao ni miongoni mwa majina wa wachezaji wengine 100 watakaogombea tuzo hizo.

Wachezaji watatu wa Arsenal kugombea GOLDEN BOY AWARD

Golden boy award ni tuzo zinazoandaliwa na jarida ya michezo la Italia la Tuttosport na hutolewa kwa wachezaji bora wanaocheza ligi za Ulaya wenye umri wa miaka chini ya 21, ambapo washindi hupatikana baada ya kupigiwa kura na waandishi wa habari za michezo.

Nelson, mwenye umri wa miaka 18,alikuwa na msimu wenye mafanikio katika timu ya Arsenal, ambapo alifanikiwa kucheza michezo 15 katika kikosi cha kwanza,pia aliisaidia timu ya vijana wenye umri wa miaka 23 kuchukua ubingwa wa Premier League 2.

Stephy Mavididi,yeye bado hajafanikiwa kuichezea timu ya wakubwa,msimu uliopita alienda kwa mkopo katika timu mbili, kwanza ilikuwa katika timu ya Preston North End inayoshiriki ligi daraja la kwanza na baadaye ilikuwa katika timu ya Charlton inayoshiriki ligi daraja la pili.

Jeff Adelaide yeye alienda Ufaransa msimu uliopita ambapo aliichezea timu ya Angers inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa ambapo alifanikiwa kucheza mechi 10 za kiushindani.

Jina la Eddie Nketiah halimo katika orodha hiyo

Mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu wa Arsenal aliyewahi kushinda tuzo hiyo,Cesc Fabregas,alishinda tuzo hiyo mwaka 2006 baada ya kufanya vizuri na kuisaidia Arsenal kuingia fainali ya ligi ya mabingwa mwaka huo.

Mwaka huu kinda la PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe anatarajiwa kushinda, Kylian Mbappe pia alishinda tuzo hiyo mwaka jana.

Majina yote ya wachezaji wanaowania tuzo hizo

Trent Alexander-Arnold, Liverpool
Carles Alena, Barcelona
Jose Maria Amo, Sevilla Atletico
Angel Gomes, Manchester United
Mirko Antonucci, Roma
Houssem Aouar, Lyon
Giorgi Arabidze, Shakhtar Donetsk
Joaquin Ardaiz, Royal Antwerp
Ismail Azzaoui, Willem II
Musa Barrow, Atalanta
Fabian Benko, Bayern Munich
Sander Berge, Racing Genk
Justin Bijlow, Feyenoord
Bilal Boutobba, Sevilla
Brahim Diaz, Manchester City
Lorenzo Callegari, Paris Saint-Germain
Lazar Carevic, Barcelona
Daniele Collinge, Stuttgart
Patrick Cutrone, AC Milan
Dani Olmo, Dinamo Zagreb
Tom Davies, Everton
Matthijs De Ligt, Ajax
Abdou Diakhate, Fiorentina
Krepin Diatta, Club Brugge
Javairo Dilrosun, Hertha Berlin
Diogo Dalot, Manchester United
Moussa Djenepo, Standard Liege
Ritsu Doan, Groningen
Mamadou Doucoure, Borussia Monchengladbach
Odsonne Edouard, Celtic
Marcus Edwards, Tottenham
Sergei Eremenko, Spartak Moscow
Zackarias Faour, Osters
Francisco Feuillassier, Real Madrid
Phil Foden, Manchester City
Mamadou Fofana, Alanyaspor
Timothy Fosu-Mensah, Crystal Palace
Juan Foyth, Tottenham
Dennis Geiger, Hoffenheim
Giorgos Giannoutsos, AEK Athens
Ianis Hagi, Viitorul Constanta
Achraf Hakimi, Real Madrid
Amadou Haidara, Red Bull Salzburg
Kai Havertz, Bayer Leverkusen
Callum Hudson-odoi, Chelsea
Nanitamo Ikone, Montpellier
Alexander Isak, Borussia Dortmund
Arnel Jakupovic, Juventus
Dejan Joveljic, Red Star Belgrade
Herbie Kane, Liverpool
Yann Karamoh, Inter Milan
Teun Koopmeiners, AZ Alkmaar
Han Kwang-Song, Cagliari
Alban Lafont, Toulouse
Leandrinho, Napoli
Dimitris Limnios, PAOK
Justin Kluivert, Roma
Lincoln, Gremio
Jordan Lotomba, Young Boys
Davor Lovren, Fortuna Dusseldorf
Sandi Lovric, Sturm Graz
Mikhail Lysov, Lokomotiv Moscow
Arne Maier, Hertha Berlin
Dennis Man, Steaua Bucharest
Manu Garcia, Manchester City
Faitout Maouassa, Rennes
Mauro Junior, PSV Eindhoven
Stephy Mavididi, Arsenal
Kylian Mbappe, Paris Saint-Germain
Weston McKennie, Schalke
Jan Mlakar, Maribor
Nikola Moro, Dinamo Zagreb
Reiss Nelson, Arsenal
Lukas Nmecha, Manchester City
Martin Odegaard, Heerenveen
Abdulkadir Omur, Trabzonspor
Matej Oravec, Spartak Trnava
Reece Oxford, Borussia Monchengladbach
Pedro Pereira, Genoa
Pietro Pellegri, Monaco
Alejandro Pozo Pozo, Sevilla
Christian Pulisic, Borussia Dortmund
Jeff Reine-Adelaide, Arsenal
Panagiotis Retsos, Bayer Leverkusen
Rui Pedro, Boavista
Yusuf Sari, Marseille
Ismaila Sarr, Rennes
Malang Sarr, Nice
Borna Sosa, Dinamo Zagreb
Moussa Sylla, Monaco
Antonio Moya Vega, Atletico Madrid
Idrissa Toure, Werder Bremen
Dayot Upamecano, Red Bull Leipzig
Moussa Wague, KAS Eupen
Chris Willock, Benfica
Ben Woodburn, Liverpool
Rafik Zekhnini, Rosenborg
Andi Zeqiri, Lausanne
Baris Zeren, Galatasaray
Luca Zidane, Real Madrid

 

Kila la heri vijana.

 

Arsenal yatangaza orodha ya wachezaji wanaoachwa na makinda wapya

Arsenal imetangaza orodha ya wachezaji wanaoachwa na wale wapya watakaojiunga na chuo cha soka cha Arsenal, Hale End.

Arsenal yatangaza orodha ya wachezaji wanaoachwa na makinda wapya

Katika orodha hiyo ya wachezaji wanaoachwa yapo majina ya wachezaji waliomaliza mikataba yao kama Sant Cazorla, Per Metersacker na Jack Wilshere na pia lipo jina la kinda mwenye kipaji cha hali ya juu Vlad Dragomir ampaye alikataa kusaini mkataba mpya.

Wachezaji waliomaliza mikataba yao

Wachezaji wafuatao watakuwa huru kuanzia tarehe 30 ya mwenzi wa 6 mwaka 2018:

Marc Bola

Santi Cazorla

Alex Crean

Vlad Dragomir

Aaron Eyoma

Yassin Fortune

Ryan Huddart

Chiori Johnson

Hugo Keto

Per Mertesacker

Tafari Moore

Jack Wilshere

Wachezaji vijana waliosaini mkataba wao wa kwanza na Arsenal

Daniel Ballard

Dominic Thompson

Robbie Burton

Wachezaji vijana walioongeza mkataba wa kuichezea Arsenal

Deyan Iliev

Tolaji Bola

Wachezaji wapya waliojiunga na shule ya soka ya Arsenal katika msimu huu wa 2018/19 

Ryan Alebiousu

Ben Cottrell

Matthew Dennis

Stanley Flaherty

Alfie Matthews

Bukayo Saka

Thomas Smith

Joshua Martin

 

Kwa wachezaji wanaoondoka tunawatakia mafanikio mema huko waendako na wale wageni karibuni sana katika chama la wana.

Calum Chambers kuongeza mkataba wa kuichezea Arsenal

Beki wa kati wa Arsenal, Calum Chambers anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu ili kuiendelea kuichezea Arsenal.

Calum Chambers kuongeza mkataba wa kuichezea Arsenal

Chambers anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa miaka 4,mkataba utakaomfanya awe mchezaji wa Arsenal hadi mwaka 2022.Hii ni kwa mujibu w taarifa iliyotolewa na mwandishi wa BBC Sports David Ornstein.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 inasemekana amemvutia kocha wa Arsenal, Unai Emery, na tayari yupo kwenye mipango ya kikosi cha kwanza kwa msimu ujao.

Chambers alicheza michezo 29 katika msimu wa 2014-15 ambao ulikuwa ni msimu wake wa kwanza Arsenal.Misimu mitatu baadaye (msimu mmoja alienda kucheza kwa mkopo Middlesbrough) amecheza michezo 30 katika kipindi hicho.

Kwa mtazamo wangu mimi ni kwamba Chambers ni beki mzuri ila anakosa uzoefu wa kucheza mara kwa mara, kwani alijiunga na timu kukiwa na mabeki wengi wazuri na alipotapa nafasi alifanya makosa mengi hali iliyomfanya atolewe kwa mkopo.

Kama Emery atarudisha hali ya kujiamini ya Chambers naamini atakuwa mhimili mkubwa katika ukuta wa Arsenal kwa miaka mingi ijayo.

Pia kuna taarifa za kwamba Unai Emery ana mtazamo mzuri kuhusu beki mwingine wa Arsenal Rob Holding, lakini anasubiri mpaka Arsenal icheze michezo ya kirafiki ili afikie uamuzi kama abaki ama atolewe kwa mkopo.

Ni muhimu sana kuwasainisha wachezaji hao kwani kwa sasa Arsenal ina uhaba wa wachezaji wazawa wa kiingeleza kitu ambacho ni muhimu sana kisheria (timu lazima iwe na wachezaji wasiopungua 8 ambao ni wazawa katika kikosi chake cha wachezaji 25).

Nacho Monreal ahusishwa na kuhamia Real Sociedad

Beki wa kushoto wa Arsenal, Nacho Monreal anatakiwa na timu ya Real Sociedad ya Hispania.Mtandao wa Noticias de Gipuzkoa unaandika.

Nacho Monreal ahusishwa na kuhamia Real Sociedad

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, kwa sasa yupo nchini Rusia akishiriki michuano ya kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania.

Monreal ambaye amekuwa moja ya wachezaji wachache wa Arsenal waliocheza vizuri katika misimu mitatu iliyopita (ambapo kwa ujumla timu ilifanya vibaya) anategemewa kufanya kazi chini ya mhispania mwenzake Unai Emery ambaye kwa sasa ndiye kocha mkuu wa Arsenal.

Lakini mtandao huo unaendelea kuhabarisha ya kwamba wawakilishi wa Monreal wamekubali mpango huo ila viongozi hao wa Real Sociadad wameambiwa waongee kwanza na Arsenal, na ili kuangalia uwezekano wa kufanya biashara kati ya timu hizo mbili.

Monreal amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa kwa hiyo Arsenal kama wanataka kupata pesa yeyote hawana budi kumuuza katika majira haya ya usajili au aondoke bure msimu ujao.

Pia inasemekana ya kwamba Real Sociedad wana mpango wa kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi kuliko ule atakaopewa na Arsenal.

Pia itakuwa ni nafasi ya pekee ya Nacho Monreal kucheza karibu na kwao kwani makao makuu ya Sociedad ni mwendo wa saa moja tu kwa gari kutoka sehemu aliyozaliwa Monreal, Pamplona.

Je mashabiki wa Arsenal, mngependa Monreal abaki ama aondoke aletwe beki kijana wa kusaidia na Sead?

Tupia maoni yako hapa chini.