Jack Wilshere ataka uhakika wa namba ili abaki Arsenal

Inasemekana ya kwamba kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere, ametaka ahakikishiwe nafasi yake kikosini na kocha mkuu wa Arsenal, Unay Emery ili asaini mkataba mpya na kubaki katika timu hiyo.

Jack Wilshere ataka uhakika wa namba ili abaki Arsenal

Katika habari iliyoandikwa na gazeti la Telegraph Mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika tarehe 30 ya mwezi huu, bado hajasaini mkataba mpya ingawa kuna taarifa ya kwamba Arsenal wamemuwekea mezani mkataba wa miaka 3 ambapo atakuwa akilipwa paundi laki moja kwa wiki na pia atapewa malipo mengine kwa kila michezo atakayokuwa akicheza.

Lakini kutokana na Arsenal kubadilisha kocha mkuu, Jack ambaye kwa msimu uliopita hakuwa na namba ya kudumu ana mpango wa kukaa chini na Emery ili kujua mipango ya kocha huyo na pia kuhakikishiwa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Jack Wilshere amekuwa mchezaji wa Arsenal tangu akiwa na miaka 9 na amekuwa ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Arsenal.Majeraha ya mara kwa mara yamesababisha mchezaji huyo mwenye kipaji cha hali ya juu kushindwa kufikia kilele cha mafanikio, hali iliyomfanya asiwe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uingeleza itakayocheza katika kombe la Dunia nchini Russia.

Je Jack Wilshere ahakikishiwe namba katika kikosi cha kwanza au aondoke na aletwe kiungo mwigine? tupia maoni yako hapa chini.

Mesut Ôzil aumia anaweza kukosa mechi ya ufunguzi kombe la dunia

Mchezaji kiungo wa Arsenal, Mesut Ôzil ameumia na kuna wasiwasi wa kwamba anaweza kukosa mchezo wa kwanza wa kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Mexico.

Mesut Ôzil aumia anaweza kukosa mechi ya ufunguzi kombe la dunia

Ujerumani wametangaza ya kwamba kiungo huyo wa Arsenal atakosa mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Saudi Arabia ambao unategemewa kufanyika hapo kesho ijumaa, hii inatokana na kuwa na majeraha goti. .

Ozil, mwenye umri wa miaka  29,alipata tatizo hiyo jumamosi iliyopita wakati Ujerumani ilipolala kwa magoli 2-1 dhidi ya Austria, na taarifa tulizonazo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa pia akakosa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia kati ya timu yake ya taifa ya Ujerumani na Mexico, mchezo ambao umepangwa kufanyika tarehe 17 ya mwezi huu.

Katika taarifa fupi kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa chama cha soka cha Ujerumani, ilidhibitishwa ya kwamba Mesut Ôzil alikosa mazoezi ya Alhamisi na hatacheza mchezo wa kujipima nguvu utakaofanyika ijumaa katika uwanja wa BayArena mjini Leverkusen.

“,Mesut Özil hakufanya mazoezi ya mwisho leo, ila alifanya mazoezi ya kukimbia.Hatacheza mchezo dhidi ya Saudi Arabia, akiwa na majeraha kidogo kwenye goti la kushoto,” chama cha soka cha Ujerumani kilisema kupitia ukurasa wake wa Twitter..

Özil alikosa michezo mingi ya mwisho ya msimu la ligi kuu ya Uingeleza kutokana na kuwa na majeraha ya mgongo wakati wa mchezo kati ya Arsenal na Atletico Madrid kugombea kombe la Europa League tarehe 3 ya mwezi wa tano.

Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia wataelekea Russia baada ya mchezo wao wa mwisho wa kirafiki hapo kesho baada ya kocha mkuu wa Ujerumani Joachim Low , kutangaza kikosi chake cha mwisho na kuwaacha wadau wengi wa soka kwa kumuacha mchezaji wa Machester City Leroy Sane.

 

Mechi kati ya wakongwe wa Arsenal na wakongwe wa Real Madrid

Leo kutakuwa na  mchezo kati ya wachezaji wakongwe wa timu ya Arsenal na wachezaji wakongwe wa Real.

Mchezo huo utakaofanyika leo katika uwanja wa Santiago Bernabeu utakuwa ni wa kwanza, kwani mchezo wa marudiano utakuwa tarehe 8 ya mwezi wa tisa mwaka huu.Mechi kati ya wakongwe wa Arsenal na wakongwe wa Real Madrid

Kikosi cha wachezaji wakongwe wa Arsenal

Seaman

Almunia

Campbel

Etame

Cygan

Winterburn

Eboue

Upson

Grimandi

Pires

Parlour

Petit

Silva

Rosicky

Limpar

Reyes

Anelka

Aliadiere

Kanu

Boa Morte

 

Kikosi cha wakongwe Real Madrid

Alfonso

Xabi Alonso

Amavisca

Álvaro Arbeloa

Julio Baptista

Emilio Butragueño

Roberto Carlos

Julio César

Luís Figo

Karembeau

Julio Llorente

Fernando Morientes

Raúl

Ronaldo Nazario

Pavón

Alberto Rivera

Fernando Sanz

Seedorf

Solari

Mchezo huo utaoneshwa moja kwa moja  na arsenal.com

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, mkongwe David O’Leary ndiye atakayekuwa kocha wa timu hiyo ya Arsenal kwa siku ya leo.

David O’Leary