Henrikh Mkhitaryan aumia, kukaa nje wiki sita

Mchezaji kiungo wa Arsenal, Henrikh Mkhitaryan ameumia na atakuwa nje kwa wiki sita akipatiwa matibabu. Katika taarifa rasmi iliyotolewa na tovuti ya Arsenal, mchezaji huyo aliumia katika mchezo dhidi ya Totenham kugombea kombe la Carabao jumatano iliyopita.

Henrikh Mkhitaryan

Kuumia kwa Henrikh Mkhitaryan ambaye ni mmoja ya wachezaji wanaoonekana kuaminiwa na kocha Unai Emery ni pigo kubwa kwa Arsenal wakati huu wa kipindi cha sikukuu kwani timu inalazimika kucheza mechi kila baada ya siku tatu.

Mchezaji huyo anaungana na wachezaji wengine kama Danny Welbeck, Rob Holding na Dinos Mavropanos ambao ni majeruhi wa muda mrefu na watakosa mechi hizi muhimu.

Mkhitaryan alisajiliwa na Arsenal karibia mwaka mmoja sasa kutoka Machester United baada ya timu hizo kuamia kubadilishana wachezaji, Alexis Sanchez akienda Old Traford, huku Mkhi akija Arsenal.

Tunamtakia Mkhi aweze kupona haraka ili aweze kuisaidia timu.

#COYG

Speak Your Mind

*