Joel Campbell ajiunga na Frosinone

Hatimaye mchezaji Joel Campbell ameondoka Arsenal na kujiunga na timu ya seria A ya Frosinone, Arsenal walitangaza mapema leo.

Joel Campbell ajiunga na Frosinone

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani alijiunga na Arsenal akitokea Deportivo Saprissa ya nchini kwao Costa Rica, mwezi wa nane mwaka 2011 na ameichezea katika mechi 40 katika kipindi hicho.

Joel Campbell alizichezea timu nyingi kwa mkopo kama Lorient, Olympiacos, Vilarreal, Sporting Lisbon na aliichezea timu ya Real Betis, kwa mara mbili, mara ya mwisho ilikuwa katika msimu wa 2017/18 .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Costa Rica, ana miaka 26 na tayari ameishaichezea timu yake ya taifa katika michezo 79 na kufanikiwa kuifungia magoli 15. Katika kombe la dunia la mwaka huu lililofanyika nchini Russia aliichezea mara mbili.
Kila la heri Joel Campbell.

Speak Your Mind

*