Kombe la Carabao-Arsenal yapangiwa na Blackpool raundi ya nne

Arsenal imepangiwa kucheza na timu ya Blackpool katika mchezo wa raundi ya nne ya kuwania kombe la Carabao.Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Emirates kati ya tarehe 30 na 31 ya mwezi wa 10.

Kombe la Carabao-Arsenal yapangiwa na Blackpool raundi ya nne

Katika michuano hiyo kuna timu 9 za ligi kuu ya Uingeleza, timu 4 za ligi daraja la kwanza , lakini Arsenal wamebahatika kupewa moja ya timu mbili za ligi daraja la pili zilizobakia.

Katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe hilo dhidi ya Brentford, kocha wa Arsenal, Unai Emery alipanga kikosi kamili kikiwa na wachezaji wengi wakongwe na wazoefu ukiondoa kinda pekee Emile Smith Rowe.

Litakuwa ni jambo la kusubiri kuona kama Unai atapanga tena kikosi kamili dhidi ya timu hiyo ya daraja la pili.

Hiyo itakuwa ni mechi ya nne katika siku 10 au 11, huku Arsenal wakicheza na Liverpool siku chache baada ya mchezo huo (Liverpool watakuwa wamepumzika wiki nzima kutokana na kutolewa mapema katika kombe hilo).

Ratiba ya mechi zingine za kombe la Carabao

Manchester City vs. Fulham
Bournemouth vs. Norwich
Leicester vs. Everton/Southampton
West Ham vs. Tottenham
Middlesbrough vs. Crystal Palace
Chelsea vs. Derby County
Burton Albion vs. Nottingham Forest

Speak Your Mind

*