Koscienly kuanza kesho-Unai Emery

Kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery amedhibitisha ya kwamba nahodha Laurent Koscienly yupo fiti na ataanza katika mchezo wa kesho dhidi ya Qarabaq katika michuano ya kombe la Europa League.

Koscienly kuanza kesho-Unai Emery

Akizungumza na waandishi wa habari leo, kocha huyo alisema ya kwamba baada ya kupatiwa matibabu ya muda mrefu na kuanza mazoezi mwezi uliopita nahodha huyo yupo tayari kucheza katika kikosi cha kwanza.

Laurent Kocienly hajawahi kucheza katika mchezo rasmi chini ya kocha Unai Emery kwani amekuwa nje ya uwanja tangu mwezi wa tano mwaka huu baada ya kuumia katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Europa League dhidi ya Atletico Madrid.

Majeraha hayo yalimfanya akose mechi za mwisho wa msimu uliopita za Arsenal, pia alikosa fainali za kombe la Dunia ambapo timu yake ya taifa iliibuka mabingwa, na msimu huu tayari ameshakosa nusu ya msimu.

Mchezaji huyo tayari ameshacheza michezo miwili akiwa na timu ya vijana wenye umri wa miaka 23 na kufanya vizuri.

Alipoulizwa kaka mchezaji huyo atacheza mchezo wa ligi jumapili ijayo dhidi ya Saouthampton, kocha Emery alisema ya kwamba ni mapema mno kuamua jambo hilo kwani uamuzi utategemea na hali yake baada ya mchezo wa kesho.

Karibu tena nahodha wa Arsenal.

 

Tupia Maoni Yako Hapo Chini