Krystian Bielik ajiunga na Derby County

Beki wa kati wa Arsenal, Krystian Bielik amejiunga rasmi na timu ya Derby County kwa dau linalokadiliwa kufikia paundi milioni 10.

Krystian Bielik ajiunga na  Derby County

Beki huyo mwenye miaka 21, aliichezea timu ya Charlton Athletic, ambapo aliisaidia kupanda kutoka daraja la pili hadi daraja la kwanza.

Krystian alijiunga na Arsenal mwaka mwezi wa kwanza mwaka 2015 akitokea timu ya  Legia Warsaw na aliichezea timu ya wakubwa ya Arsenal kwa mara ya kwanza katika kombe la ligi mwezi wa 10 mwaka huo 2015 dhidi ya timu ya Sheffield Wednesday.

Mchezaji huyo ambaye ni sehemu ya timu ya taifa ya Poland alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichochukua ubingwa wa ligi daraja la pili kwa vijana wenye umri wa miaka 21 katika msimu wa 2015/16.

Tangu mwezi wa kwanza mwaka 2017, Krystian ameshazichezea kwa mkopo timu za Birmingham City na Walsall, kabla ya msimu uliopita kwenda  Charlton kwa mkopo ambapo alicheza kama kiungo mkabaji.

Alicheza vizuri katika michuano ya kuwania kombe la Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 lakini inaonekana ya kwamba hakua kwenye mipango ya mwalimu Unai Emery.

Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya Derby County ambapo Arsenal itapata kiasi cha pesa iwapo timu hiyo itamuuza ndani ya miaka hiyo mitano.

Kila la heri Krystian Bielik.

Speak Your Mind

*