Laurent Koscielny ajiunga na Bordeaux

Nahodha wa Arsenal, Laurent Koscienly ameachana rasmi na timu hiyo na kuamua kurudi kwao Ufaransa ambapo amejiunga na timu ya Bordeaux.

Laurent Koscielny ajiunga na Bordeaux

Beki huyo wa kati ameichezea timu ya Arsenal katika michezo 353 tangu ajiunge na timu kutoka Lorient mwaka 2010. Alikuwa katika kikosi kilichoshinda kombe la FA mwaka 2014, 2015 na 2017.

Koscienly amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kwanza cha Arsenal kwa miaka tisa, lakini majeraha ya mara kwa mara na kusogea kwa umri kuchechangia mchezaji huyo kufikia uamuzi wa kurudi kwao kumalizia soka lake.

Aliingia katika mgogoro na Arsenal baada ya kugoma kwenda Marekani kwa ajili ya kambi na mechi za kirafiki kiasi cha uongozi wa Arsenal kuamua awe anafanya mazoezi na kikosi cha watoto.

Baada ya timu kurudi kutoka Marekani, Kocha wa Arsenal, Unai Emery alijaribu kumsawishi mchezaji huyo amalizie mwaka wake wa mwishi uliobaki katika mkataba wake na Arsenal lakini mchezaji huyo hakutaka kubabi Arsenal.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Arsenal uliamua kumuuza kwa timu ya Bordeaux kwa dau lenye dhamani ya paundi milioni tano.

Pamoja na yote hayo bado hatuwezi kuusahau mchango mkubwa Laurent Koscienly alioutoa kwa Arsenal, magoli muhimu aliyofunga na kumbukumbu nyingine nyingi nzuri alizotupatia wakati wa miaka 9 kama mchezaji wa Arsenal.

Kila la heri LOLO

#COYG.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini