L’Equipe: Arsenal imekamilisha usajili wa Sokratis Papastathopoulos

Jarida la michezo la kifaransa  L’Equipe, linadai ya kwamba Arsenal imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos.

L’Equipe: Arsenal imekamilisha usajili wa Sokratis Papastathopoulos

Sokratis, beki mzoefi aliyeichezea timu ya taifa ya Ugiriki michezo 79, amekuwa akiichezea Dortmund tangu asajiliwe na timu hiyo mwaka 2o13 akitokea kwa wakali wengine kutoka Bundesliga, Werder Bremen.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka 5 aliyokaa katika timu hiyo inayotumia uwanja wa Westfalenstadion,beki huyo kisiki alikuwa mhimili mkubwa wa timu hiyo na kumfanya kuwa mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho.Kuondoka kwa Mats Hummels katika majira ya kiangazi ya mwaka 2016 kulimfanua Socratis kuwa kiongozi wa uwanjani wa timu hiyo

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alicheza michezo 43 katika mashindano yote msimu uliopita, akifunga magoli matatu katika kipindi hicho.

Kutokana na Dortmund kuyumba sana ndani ya miezi 6 iliyopita, kiwango cha mchezaji huyo nacho kiliyumba pia hali iliyosababisha kutaka kuhama ili kubadilisha hali ya hewa.

Kama matokeo ya kuteteleka kwa kiwango chake uwanjani kulikuwa na tetesi ya kwamba mchezaji huyo ameamua kuihama timu hiyo huku Arsenal Manchester United wakitajwa kuongoza mbio za kuiwania saini yake.

Usajili wakamilika

Baba yake na Sokratis alisikika katika kituo kimoja cha redio nchini Ugiriki akisema ya kwamba mwanae ameshaini mkataba wa kuichezea Arsenal tangu jumanne iliyopita, bado hakuna taarifa ramsi kutoka upande wa Arsenal kudhibitisha usajili huo.

Lakini vyanzo vingi vilivyokaribu na Arsenal, na sasa kutoka gazeti la  L’Equipe ,tunaweza kusema ya kwamba Sokrais ameshasajili na atakuwa mchezaji wa Arsenal kwa msimu ujao.Ukiwa ni usajili wa pili baada ya beki wa kulia Stephan Lichtsteiner kudhibitishwa kuhamia Arsenal jumanne iliyopita.

Je Sokratis Papastathopoulos utakuwa ni usajili mzuri? tupia maoni yako hapa chini.

 

Comments

  1. utakuwa mzuri

Speak Your Mind

*