Mashabiki wa Arsenal-Asanteni sana na Heri ya mwaka mpya

Heri ya mwaka mpya

Yakiwa yamebaki masaa machache kuuaga mwaka huu 2018 ningependa kuchukua nafasi hii na kusema asante sana kwa wote waliotuunga mkono katika mwaka huu wa 2108 na pia kuwatakia heri na fanaka katika mwaka mpya wa 2019.

Wakati naanzisha blog hii sikutegemea kupata wasomaji wengi kiasi hiki kwani sijawahi kuwa mwandishi wa habari, sijawahi kusomea au kuota kuandika, nikiwa shule nilikuwa natoroka somo la kiswahili.

Lakini pamoja na mapungufu mengi katika taarifa tunazotoa bado wewe kama mdau umeendelea kutuunga mkono na kwa hili tunasema asante.

Mwaka huu mambo hayakwenda kama tulivyopanga kwani mwishoni mwa mwezi wa nne tulipoteza habari zote zilizokuwepo mwanzo na kutokana na majukumu mengine ilichukua kama miezi miwili kuanza kuandika upya, katika kipindi hicho tulikuwa tunapokea ujumbe kutoka kwa wadau mbalimbali waliokuwa wanataka kujua nini kilitokea na walikuwa tayari kutoa msaada.

Kwetu sisi hilo lilikuwa ni jambo lililotutia sana moyo kuona ya kwamba kuna baadhi ya watu wanapenda tunachokifanya na wapo tayari kutusaidia.

Pia kuna wakati tunashindwa kuweka taarifa kila siku kutokana na kuwa na majukumu mengine kikazi ama kifamilia na kwa hilo tungependa kuomba msamaha, ila tunaahidi mwaka 2019 tutajitahidi lisitokee mara kwa mara.

Asilimia 79 ya wasomaji wetu ni watanzania, na kwa hilo tunasema asante Tanzania,pia asante sana kwa wasomaji wetu kutoka nchi nyingine ikiwemo Kenye, Marekani, Congo, Afrika ya kusini, Burundi na nyinginezo.

Mashabiki wa Arsenal-Asanteni sana na Heri ya mwaka mpya

Kwa upande wa majiji na mikoa, tumepata wasomaji wengi kutoka Dar es salaam wakifuatiwa kwa mbali na Nairobi,Mwanza na Zanzibar, asanteni sana na Mungu awabariki.

Mashabiki wa Arsenal-Asanteni sana na Heri ya mwaka mpyaHeri ya mwaka mpya 2019 msisahau kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita na kumuomba atuoongoze katika mwaka mpya ambao tunauanza ndani ya dakika chache.

#COYG

 

Comments

  1. Shukrani

Speak Your Mind

*