Mike Dean alikosea-Mark Clattenburg

Mwamuzi wa kimataifa wa Uingeleza, Mark Clattenburg amesema ya kwamba mwamuzi wa mchezo wa jana kati ya Arsenal na Totenham alifanya makosa katika magoli yote mawili yaliyofungwa na Totenham.

Mike Dean alikosea-Mark Clattenburg

Akitoa ufafanuzi kuhusu magoli hayo,Mark Clattenburg alisema ya kwamba Mike Dean alipaswa kukataa goli la kusawazisha la Totenham kwani mfungaji wa goli hilo, Eric Dier alikuwa ameotea kabla ya Eriksen hajapiga mpira wa faulo.

Kuhusu penati, refa huyo ambaye kwa ni mkuu wa kitengo cha waamuzi cha shirikisho la soka la Saudi Arabia, alisema ya kwamba mchezaji wa Totenham, Son alijiangusha kwani beki wa Arsenal hakumgusa.

Marudio ya tukio hilo yalionesha ya kwamba ni kweli mchezaji huyo alijiangusha na kusababisha Mike Dean kuwazawadia Spurs penati iliyozaa goli lao la pili.

Pamoja na kubebwa huko, Arsenal walifanikiwa kufunga magoli matatu katika kipindi cha pili na kufanikiwa kushinda mchezo huo kwa jumla ya magoli 4-2.

Kesho kutwa jumatano Arsenal itakuwa katika uwanja wa Old Traford kucheza na Manchester United katika muendelezo wa ligi kuu ya Uingeleza.

Speak Your Mind

*