Ni wakati wa kuwafunga midomo Totenham

Leo Arsenal inacheza na wapinzani wao wa jadi Totenham Hotspurs katika muendelezo wa ligi kuu ya Uingeleza.Hii sio mechi ya kawaidia ya ligi kuu ya Uingeleza, hii ni vita,ni vita ya kugombea haki ya kutawala kaskazini mwa jiji la London.

Huu ni mchezo ambao hata kama mchezaji kafanya vibaya msimu mzima akifunga goli dhidi ya Spurs makosa yake yote husamehewa, fanya vizuri katika mchezo huu unakuwa shujaa ama fanya vibaya unakuwa adui.

Ushindi katika mchezo huu ni muhimu sana,lakini kwangu mimi naona hizi ni sababu tatu muhimu kwa nini nataka Arsenal washinde mchezo huu.

Pambano la kwanza la watani wa jadi Unai Emery akiwa kocha wa Arsenal

Ni wakati wa kuwafunga midomo Totenham

Kama nilivyosema hapo juu, shinda huu mchezo na unakuwa shujaa wa Arsenal, ushindi dhidi ya Spurs utamfanya aendelee kupendwa na kuungwa mkono na mashabiki wa Arsenal hasa wazaliwa wa London.

Kupanda katika msimamo wa ligi

Arsenal ikifanikiwa kuinfunga Totenham katika mchezo wa leo kwa idadi yeyote ya magoli,itafanikiwa kuwa juu ya timu hiyo na kufanikiwa kuwa katika timu nne za mwanzo katika msimamo wa ligi.

Kuwafunga midomo wachambuzi na mashabiki wa Spurs

Totenham ni moja ya timu zinazopendwa sana na wachambuzi wa soka, wanaweza kufanya kitu cha kawaida na wakasifiwa sana na wachambuzi hao.

Pia mashabiki wengi wa Totenham wamepandwa na viburi kwani leo nilikuwa napitia katika mitandao ya kijamii na wanaona kama tayari wameshashinda mchezo wa leo, tukiwafunga na kuwachezea soka la hali ya juu tutafanikiwa kuua ndege wawili kwa jiwe moja, tunakuwa juu yao kwenye ligi na tunawafunga midomo.

Hali ya mchezo

Totenham wamekuwa wakipata matokeo mazuri, walifanikiwa kuwafunga Chelsea na Inter Milan na wataenda katika mchezo huo wakijiamini.Kwa upande wa Arsenal wao wana mechi 18 bila kufungwa na watataka kuendeleza rekodi hiyo.

Nacho Monreal na Danny Welbeck hawatashiriki katika mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi,Laurent Koscielny yeye bado hajawa tayari kucheza, ingawa  Alexandre Lacazette  ambaye alikosa michezo dhidi ya Bournemouth na Vorskla yupo fiti na anaweza kucheza leo.

Kikosi kitakachoanza

Kikosi cha kitakachoanza kesho itategemea sana na aina ya mfumo atakaotumia mwalimu, Unai Emery huwa anatumia 4-2-3-1 , 4-3-3 na 3-4-3 (au 5-4-1 inategemea na unaonaje), bila kujali aina ya mfumo kuna wachezaji ambao naamini hawawezi kukosa katika mchezo huo.

Bern Leno, Hector Bellerin,Lucas Torreira, Granit Xhaka,Aubamayang ni nguzo ya Arsenal kwa sasa na sitegemei kuona wakikosa mchezo huo bila kujali aina ya mfumo utakaotumika.

Utabiri

Linapokuja suala la pambano la watani wa jadi ni vigumu sana kutabili, ila nina imani na timu hii hivyo nitasema Arsenal 2-1 Totenham Lucas Torreira kufunga goli lake la kwanza.

Je wewe una mtazamo gani kuhusu mtanange huu? tupia maoni yako hapa chini.

 

 

Speak Your Mind

*