Rasmi-Arsenal yakamilisha usajili wa Matteo Guendouzi

Arsenal imeendelea na juhudi zake za kujipanga upya baada ya kumalilisha usajili wake wa tano msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa kinda Matteo Guendouzi.

Rasmi-Arsenal yakamilisha usajili wa Matteo Guendouzi

Matteo Guendouzi ambaye ni kiungo mfaransa mwenye umri wa miaka 19 anajiunga na Arsenal akitokea Lorient inayoshiriki katika ligi daraja la pili ya ufaransa.

Kinda huyo alianza maisha yake ya soka katika timu ya PSG kabla ya kutimka na kujiunga na chuo cha soka cha Lorient mwaka 2014.

Matteo aliichezea timu ya Lorient kwa mara ya kwanza mwaka 2016 akiwa na miaka 17 tu, ambapo baadaye alicheza michezo 30 katika msimu huo.

Mchezaji huyo tayari ameshaiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa kwa vijana wenye umri wa miaka 18,19 na 20.

Baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Tumefurahi sana ya kwamba Matteo anajiunga na Arsenal,Ni mchezaji mwenye umri mdogo lakini mwenye kipaji cha hali ya juu.Anaweza kuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye na tayari ana uzoefu wa kucheza michezo ya kikosi cha kwanza alioupata msimu uliopita akiwa na Lorient.Anataka kujifunza na atakuwa mchezaji wa muhimu katika kikosi cha kwanza”

Matteo atavaa jezi namba 29 akiwa na Arsenal.

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*